GE2025 TAKUKURU Geita yafuatilia tuhuma za Rushwa Kura za Maoni CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
aasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita imesema inaendelea kufuatilia kwa karibu vitendo vya rushwa vilivyodaiwa kutokea katika mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni ya wabunge na madiwani ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, James Ruge, amesema uchunguzi unahusu picha na video zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha baadhi ya wajumbe wanawake wakigawana fedha katika Jimbo la Geita, pamoja na tukio la wajumbe kuandaliwa chakula na vinywaji katika Jimbo la Chato Kaskazini, Kata ya Bukome, Kijiji cha Buzilayombo.

Baadhi ya video hizo pia zilimwonesha mmoja wa wagombea wa Jimbo la Chato Kaskazini, Cosmas Makongo, akilalamika kuhusu tuhuma za rushwa.

Soma Pia: Viongozi wa CCM Geita walalamikia kukithiri kwa rushwa kura za maoni

Hata hivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Chato, Charles Mazuri, amekanusha tuhuma hizo akisema chakula kilichoandaliwa kilitolewa na chama kutokana na umbali wa safari za wajumbe, na si kwa nia ya kuwanunua.

Bila rushwa hakuna anayestahili Geita inanuka rushwa saiv na mauaji
 
Hii TAKA-KUU iache unafiki. Haijaziona baiskeli na pikipiki za Samia zilizosambaa nchi nzima???
 
Back
Top Bottom