TAKUKURU isiongozwe na Askari. Inahitaji katiba ya Dkt. Hosea kuifufua

TAKUKURU isiongozwe na Askari. Inahitaji katiba ya Dkt. Hosea kuifufua

Hakijawahi kua perfect toka kimeundwa, Yes. But ubutu wa sasa unazidi Kwa mbali ubutu wa zamani. Sasa kimezidi kua butu mno.
Ni butu toka siku ya kwanza na siyo kosa lao bali viongozi wa wakuu.
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imekabidhiwa mikononi mwa wanajeshi na Askari. Kazi hii aliifanya Magufuli kwa lengo la kumwezesha kutoa amri ya kutimiza malengo yake .

Baada ya JPM bado aliteuliwa Afisa wa Polisi kuongoza taasisi hii. Madhara ya uteuzi ule ni kwamba taasisi imeacha misingi yake na sasa inasikiliza amri kutekeleza majukumu yao. Ni taasisi inayosubiri mwanasiasa aseme kamata na siyo taasisi yakujieneza kwa jamii kubaini wizi na kuchukua hatua.

TAKUKURU inapaswa kuwa na mifumo mizuri ya kubaini viashiria vya rushwa kwenye taasisi na kisha kukutana na mkuu wa taasisi husika kumwelekeza visharia na risks zilizopo anazopaswa kuzifanyia kazi.

TAKUKURU haipaswi kukamata inapaswa kuita mtuhumiwa kwa mahojiano. Haipaswi taasisi yakisubiri wizi utokee bali iwe taasisi yakuona wizi kabla hakutendeka na kudhibiti isitokee.

Kwa ufupi TAKUKURU ilipaswa kuangaika na mapapa siyo dagaa.....dagaa walipaswa kudhibitiwa kwa kuwabaini kabla ya kuiba ili wasifanikiwe kuiba.

Nashauri mamlaka za uteuzi ziondoe TAKUKURU polisi na kuirudisha kwa RAIA wenye integrity. Haiwezekani watumishi wa TAKUKURU wafanye kazi ndani kwao wanapofikia nafasi ya ukurugenzi mkuu waletewe mtu kutoka nje ya taasisi na anayeletwa akapata uungwaji mkono. Tukubali kwamba hizi taasisi wapo watu wamesota miaka na miaka wakifanya kazi wafikie nafasi ya juu, tuwape nafasi badala ya kuwaletea watu kutoka nje.

Rushwa imekithiri kwa sababu wanaopambana na rushwa leo walikulia kwenye rushwa. Kila wakitaka kuchukua hatua wanakumbuka maovu yao.
Tatizo hapo kwenye kupambana, mapambano kuna wakati yanahitaji mbinu ngumu kidogo siyo soft.
Hao raia wa kawaida watapambana vipi bila kuwa na ukakamavu?
Ila tatizo lako nimeona ni cheo mkuu,wewe piga kazi Mungu atakuinua usiangalie wanadamu. Halafu wewe hukusomea Ukurugenzi, hizo ni ziada relax!
 
Hakijawahi kua perfect toka kimeundwa, Yes. But ubutu wa sasa unazidi Kwa mbali ubutu wa zamani. Sasa kimezidi kua butu mno.
Wewe ni mmojawapo wa kuifanya TAKUKURU ionekane haifanyi vema. Takukuru siyo wapiga ramli,wanahitaji msaada wa raia wema kuripoti rushwa ili wazuie.
Je,katika kuombwa kwako rushwa umewahi kuripoti???
 
Mzungu haombwi rushwa ndio maana miradi yao walau inakuwa imara TZ
 
Ndugu zangu siyo SIRI hamduni hana uwezo na ueledi wa kuliongoza dude kubwa kama TAKUKURU, halifahamu na pia ni limbukeni wa majukumu. Huwezi kuamini hiyo Taasisi Kwa sasa inakamata watoto wadogo wadogo Tena Kwa mipango mikubwa na baadhi ya wajinga wenzie. Tunaomba tukubie Hamduni,hautatukuzwa mpaka mbinguni ila utashushwa mpaka kuzimu kwasababu hujui uyatendayo
 
Ndugu zangu siyo SIRI hamduni hana uwezo na ueledi wa kuliongoza dude kubwa kama TAKUKURU, halifahamu na pia ni limbukeni wa majukumu. Huwezi kuamini hiyo Taasisi Kwa sasa inakamata watoto wadogo wadogo Tena Kwa mipango mikubwa na baadhi ya wajinga wenzie. Tunaomba tukubie Hamduni,hautatukuzwa mpaka mbinguni ila utashushwa mpaka kuzimu kwasababu hujui uyatendayo
Mla rushwa tu huyo polisi mama anayumbishwa ndo maana CAG nae anafelishwa anaibua madudu yakienda PCCB yanafunikwa ulaji wa pipozi
 
Takukuru sio raia wa kawaida; wana mafunzo ya kijeshi na ndio maana wanaongozwa na Mwanajeshi/askari.

Saivi kozi yao wanapigia Chuo cha Taaluma ya polisi(MOSHI)kwahiyo haiwezekani ikawa taasisi lelemama lazima iongozwe kijeshi.
Huo Upuuzi umeletwa na Magufuli
Hizo Taasisinzinafaa kuwa na watu wenye ajili za Hali ya juu Sana
PCCB ikifaa iwe Kama SFO ya Uingereza
Sasa Polisi Kilaza atafanya nini cha Maana ?
Jiwe alianza kuweka Maaskari ili aweze kuwa command anavyotaka yeye
 
Back
Top Bottom