TAKUKURU: Jeshi la Polisi ni kinara wa Rushwa nchini

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) 2022/2023, imezitaja sekta zinazoongoza kwa vitendo vya rushwa nchini, huku Jeshi la Polisi likishika nafasi ya kwanza kwa asilimia 45.6 kati ya nne vinara.

Kwa takwimu hizi uadilifu wa Jeshi la polisi uko wapi hadi liaminiwe kulinda wananchi na mali zao.

Maadili ya Jeshi la polisi yako wapi hadi liaminiwe kufanya upelelezi wa ubakaji ili hali maofisa wake wanatuhumiwa kwa vitendo vya ubakaji,

Jeshi la polisi liaminiwe vipi na wananchi wakati linatuhumiwa kwa vitendo vya utekaji.

Ni dhahiri kwa vitendo hivi Jeshi la polisi linajipora lenyewe legitimacy ya kuwa mtunza amani nchini, aidha ni kutokana na elimu au mafunzo wanayopata au ni utovu wa nidhamu wa askari mmoja mmoja.

IGP, Mkurugenzi wa Mafunzo hamuoni aibu kuongoza taasisi ya aina hii inayolalamikiwa hadi na taasisi zingine za umma.

Nini kifanyike.
 
Police kuna hadi Canbalisim, hii ni hali ya viumbe wanao fanana kulana wao kwa wao, mfano kuku kumla kuku mwenzao, au Mbwa kula mbwa mwenzao.

Police wao kwa wao wanapigana rushwa vibaya mno, yaani wanachukua rushwa kwa raia kama haitoshi wanatoa rushwa wao kwa wao offisini.
 
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) 2022/2023, imezitaja sekta zinazoongoza kwa vitendo vya rushwa nchini, huku Jeshi la Polisi likishika nafasi ya kwanza kwa asilimia 45.6 kati ya nne vinara.

Kwa takwimu hizi uadilifu wa Jeshi la polisi uko wapi hadi liaminiwe kulinda wananchi na mali zao.

Maadili ya Jeshi la polisi yako wapi hadi liaminiwe kufanya upelelezi wa ubakaji ili hali maofisa wake wanatuhumiwa kwa vitendo vya ubakaji,

Jeshi la polisi liaminiwe vipi na wananchi wakati linatuhumiwa kwa vitendo vya utekaji.

Ni dhahiri kwa vitendo hivi Jeshi la polisi linajipora lenyewe legitimacy ya kuwa mtunza amani nchini, aidha ni kutokana na elimu au mafunzo wanayopata au ni utovu wa nidhamu wa askari mmoja mmoja.

IGP, Mkurugenzi wa Mafunzo hamuoni aibu kuongoza taasisi ya aina hii inayolalamikiwa hadi na taasisi zingine za umma.

Nini kifanyike.
Bora IGP, Huyo anayejiita kamishina wa mafunzo ndo balaa.
 
Takukuru nao wachunguzwe.Nakumbuka enzi za magu aliwaambia Takukuru kuwa kunamfanyakazi wao alikuwa mla rushwa sana lakini Takukuru ilimwogopa Hadi magufuli akaagiza ndiyo akakamatwa.Vyombo vyetu vya ulinzi vyote ni Wala rushwa
 
Jeshi la police lazima wataongoza kwa sababu wamepewa mamlaka makubwa sana kisheria na mbaya zaidi wananchi wengi hawajui haki zao hivyo polisi kuwaonea na kutaka rushwa wawaachie ndio imekua chaka lao.

Polisi wa bongo ukohoji haki zako anakwambia unajifanya unajua sana kuliko sisi, sio? Mbaya zaidi mfumo wa polisi wa kulindana umeota mizizi mirefu sana. Hadi polisi wawajibishane ni kazi kubwa sana.
 
Back
Top Bottom