Hapa mkoani Singida, Afisa Habari mmoja mwanaume anatuchezea michezo ya nyumba mbele. Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida tunateswa sana na huyu Afisa Habari anayekata posho zetu juu kwa juu na kutaka sisi tufanye kazi ya bila kulipwa wakati malipo ya kazi husika yanatoka.
Mfano hivi karibu limeonekana karatasi lenye majina ya Waandishi wakiwa wamelipwa laki moja moja. Wakati uhalisia ni kuwa hakuna kazi ya mkoani ambayo Waandishi wamelipwa laki moja moja.
Afisa Habari huyu amekuwa akikata posho za Waandishi anawasainisha 30k huku amewaombea 50k. Mtu huyu amekuwa kichomi kwetu kwa kutubania hadi kwenye taasisi zingine.
Mfano imekuja taasisi ambayo wanalipa posho wao wenyewe anachokifanya yeye anawaambia Waandishi wape 30k hawalipwagi zaidi ya hiyo. Kwakweli Mkuu wa Mkoa tunaomba ikiwezekana mtu huyu apangiwe kazi nyingine.
Anatuchosha sana. TAKUKURU mchunguzeni mtu huyu asikae hapa akawa anashibia majasho ya watu.