TAKUKURU mnalala kwa makusudi: Ufisadi miradi ya ujenzi uko wazi na mnajidai hamuuoni!

TAKUKURU mnalala kwa makusudi: Ufisadi miradi ya ujenzi uko wazi na mnajidai hamuuoni!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,653
Reaction score
31,010
Huu mkeka wa ufisadi umepamba moto miaka ya karibuni bila kuchukuliwa hatua,
TAKUKURU ina fuatilia vidagaa, na ni kwa vile wakubwa wanahusika katika hii grand corruption.

Ujenzi sasa hivi ni sekta inakaribia kubomoka kabisa kutokana na corruption inayowahusu Wachina, Taasisi za ujenzi, hasa TANROADS na wizara ya fedha.
Watu serikalini wamejitoa ufahamu na wanaiba bila kipimo.

Mambo iko hivi;
Mradi unabuniwa, anatafutwa mchina wa kiongozi maana tayari imeshasukwa.
Mchina anapewa tenda ya mradi na anadai na kupewa malipo ya awali (Advance Payment)
hiyo Advance Payment anapewa yote Kiongozi na ana kaa kimya kama maji ya mtungi, na hakuna kitu kinaanza site.
Baada ya miezi kupita ndio kelele za danganya toto zinaanza, mara kutembelea mradi na makelele mengi, mchina kimya , analeta kifaa kimoja au viwili site.
Watamfanya nini wakati wamekula hela yake?

Hela ya mradi hailipwi kwa wakati toka serikalini, tena wakati mwingine mwaka mzima.
Mchina anaenda kukopa serikalini kwao, baada ya mradi kuchelewa sana.
Kule anakopa kwa riba ya 3% kwa dhamana ya mradi.

Mchina anapiga kazi lakini mradi uncheleweshwa kwa kausudi, maana huko ndiko hela iliko.Mchina akimaliza kazi sasa ndio maloloso ya ufisadi yanaanza.
Mchina anaambiwa ni haki yako kudai ucheleweshwaji wa malipo yake toka serikalini.
Hapo ndio mabilioni yanapigwa.
Kumbuka ile 15% Advance Payment iliyotolewa kwa wakubwa, yoote inarudi, na iliyobaki watu wanagawana wahusika wa mradi.
Watu hapo wanakula kwa urefu wa kamba zao, na hawajavunja benki yoyote.
Pesa inaliwa kilaiini!

No wonder jirani yangu mwajiriwa wa serikali wizara ya fedha , tuko huku mashenzini, anajenga jengo la ghorofa nne lenye nyumba nane, mbili kila floor!

Ndio mambo ya ujenzi hayo
 
Chura aka kizimkazi Hana nguvu na amezidiwa na mafisadi. Ivyo watanganyika tusipo amka cjui itakuaje cku zijazo. Yy anachoweza kufanya kwa ufasaha ni KUTEUA na KUTENGUA tu na masafari.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Chura aka kizimkazi Hana nguvu na amezidiwa na mafisadi. Ivyo watanganyika tusipo amka cjui itakuaje cku zijazo. Yy anachoweza kufanya kwa ufasaha ni KUTEUA na KUTENGUA tu na masafari.
Kazi ni kipimo cha utu
Kwa kweli Mama Samia ameonyesha udhaifu mkubwa kupigana na institutionalised corruption.
Watu wanakula pesa ya kodi zetu kwa kutumia taratibu za kifedha, taratibu zinazo ruhusu wizi.
 
Back
Top Bottom