DOKEZO TAKUKURU Mwanza tupieni macho mgogoro wa ardhi wa Abubakar Self

DOKEZO TAKUKURU Mwanza tupieni macho mgogoro wa ardhi wa Abubakar Self

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Kalebejo

Member
Joined
Sep 24, 2022
Posts
9
Reaction score
4
VIONGOZI WA KITENGO CHA ARDHI JIJI LA MWANZA LINATUUMIZA WANACHI WALALA HOI

Kada wa CCM Abubakar Hassan Self amemuomba Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Kuingilia kati mgogogro wake viwanja na Halmashauri ya Jiji la Mwanza uliodumu kwa miaka 35 kama mgogoro wa Eneo la Rwagasore lilivyotatuliwa.

Takribani Sasa ni Miaka 35 Tangu Kada wa CCM Abubakar Hassan Self Mwenyekiti wa serikali wa Nera kata ya Isamilo wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Kwa Vipindi sita , Amekuwa anahangaika na mgogoro wa Viwanja anavyokuporwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambavyo ni urithi wa wazazi wake vilivyopo kata ya isamilo jiji Mwanza

Hivyo kwa uhalali alionao anamuomba rais Samia Suluhu Hassan kutupia macho idara ya ardhi ya jiji la Mwanza kuwa limekuwa na tabia ya kupoka ardhi za wananchi na kuwauzia watu wenye vipato na wao kuhangaika mahakamani na hata hukumu ikitoka ya wananchi kupewa haki yao bado jiji limekuwa na ubabe wa kutotii maagizo

"Nakuomba Rais wangu mwenyekiti wa Chama usimamia nipate haki yangu "alisema Kada Abubakar self na kusema Mkuu wa Mkoa wa Mwanza adam malima ameanza kwa hatua hiyo ya kuchuguza ubadhilifu wa jiji la mwanza tunampongeza ila kwa sisi ambaye malalamiko yetu yapo kwa siku nyingi ni vigumu sana kuyatambua kutokana na jama za baadhi ya viongozi kufichwa ukweli

Kwa mfano wa kada wa CCM kuna wananchi wengi sana wamechukuliwa pesa zao katika mradi wa kuuza viwanja vya isamilo na luchelele ukichuguza wafanyakazi wa jiji ndio wamepata ukijiuliza kwanini walitangazia umma na hali tayari walikuwa wamegawana, na wakapokea pesa zao huu ni unyonyaji wa machi macho TAKUKURU TUNAOMBA MCHUNGUZE HILI SWALA WANANCHI WANALALAMIKA.
 
kilio cha kada wa ccm abubakar hassan self kupolwa ardhi na halmashauri ya jiji la mwanza
 

Attachments

  • KILIO CHA KADA CCM - APOLWA ARDHI NA MAMLAKA.mp4
    10.3 MB
Back
Top Bottom