DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yote niliyoandika ni kweli. Na ushahidi ninao mwingi tu.

Siandiki uongo hapa, ili iweje.

Hilo la nauli, sijataka kuandika linavyofanyika. Nimefanya "due diligence" kidogo. Kwa hiyo ukiwa hujafuatilia jambo, usiseme tu eti uongo.

Hiyo barabara ya mwendokasi Mbagala, ishu sio hicho kipengele cha kuja kurudiwa, hii barabara imeanza kuharibika hata matumizi bado .

Na vituo n.k ni substandard.

Barabara ya KIMARA iko imara na inatumika mwaka wa 7 sasa, hii inameguka, mashimo, unasema kipengele cha kurudiwa?! Shit
 
Asante kwa ushahidi huu.

Cc: ChoiceVariable ,

Mie nina ushahidi wa mbinu nyingi tu wanazotumia ku overcharge nauli.

Sasa ndio maana nikashauri kama hawa wa mabus wanaona nauli zilizopangwa ni ndogo, haziwapi faida, basi zipandishwe, kwani ndio hizo hizo abiria wanazolipishwa juu ya LATRA.
 
Bila ushahidi ni porojo za chuki,weka ushahidi wa jinsi watu wanalipishwa nauli kinyume na bei ya Sumatra

Hiyo Barabara yenu iwe chini ya kiwango au vinginevyo contractor atarudia Wala Halima ubishi

Mwisho ukipenda cheap ndio madhara yake hayo unalazimisha bei ya chini ndio uwe tayari na matokeo yake mkandarasi asilaumiwe Bali yule Rais wenu aliyekuwa analazimisha bei za chini ndio alaumiwe.

Hata hiyo njia 8 Serikali imelazimika kufumua Baadhi ya sections na kuongeza activities plus pesa vinginevyo nayo ingekuwa kituko
 
TISS nayo wapewe waarabu tu yaishe. Maana sababu zilizotajwa kuwa hasa zimefanya bandari wapewe waarabu, hata TISS wanazo
 
Sasa kwani gari ni Shabiby tuu? Harafu kama bei za Sumatra mnazijua Kwa nini ulipe zaidi?

Huu ni ujinga mwingine wa kutegemea Serikali Kwa Kila kitu wakati mtu wa kwanza kulinda haki Yako ni wewe raia.
 
Shida hujadili mada, unarukia rukia watu tu .

USHAHIDI wangu siwezi kuuweka hapa. Nina sababu za kufanya hivyo, na it's proven mathematically.
Natumia akili na elimu yangu.
 
Shida hujadili mada, unarukia rukia watu tu .

USHAHIDI wangu siwezi kuuweka hapa. Nina sababu za kufanya hivyo, na it's proven mathematically.
Natumia akili na elimu yangu.
Acha porojo wewe,ingekuwa hivyo watu wangeshalalamika.ila.kama ulipigwa na kampuni Moja ni wewe imekula kwako usitake ku generalise
 
Hapo kwenye NIDA ni hatari kweli. Kazi ipo. Na sasa hivi nchini hapa wamejazana waNigeria kibao, usikute tayari wana vitambulisho vya taifa kabisaa.
 
Hayo yote kamwe Nchi hii hayawez shughulikiwa effectively!!! Zipo report kibao za kifisadi miaka sasa lkn zinafunikwa na maisha yanaendelea!! Nchi hii mpaka upatikane utawala thabiti na katiba inayong'ata nje ndan!!!
 
Hapo kwenye NIDA ni hatari kweli. Kazi ipo. Na sasa hivi nchini hapa wamejazana waNigeria kibao, usikute tayari wana vitambulisho vya taifa kabisaa.
Wa Rw, wenye hela wanaovihitaji washapewa.
 
Hayo yote kamwe Nchi hii hayawez shughulikiwa effectively!!! Zipo report kibao za kifisadi miaka sasa lkn zinafunikwa na maisha yanaendelea!! Nchi hii mpaka upatikane utawala thabiti na katiba inayong'ata nje ndan!!!
Sasa tunafanyaje, tunatokaje hapa..
 
Nauli hazipandishwi hovyohovyo... kuna policies maalum za kiuchumi ambazo huwa applied na hupelekea vitu mbalimbali nchini kupanda bei au kushuka.
 
Hapo kwenye NIDA ni hatari kweli. Kazi ipo. Na sasa hivi nchini hapa wamejazana waNigeria kibao, usikute tayari wana vitambulisho vya taifa kabisaa.
Wanavyo... nina ushahidi wa bwana mmoja anaitwa "KEVIN ANTRUM"..., ni rafiki yangu. Mmarekani mwenye asili ya Puerto rico. Kahamia hapa na familia yake, ni daktari Aga khan, alipapenda Tanzania kwa sababu aliletwa kwa ajili ya field zile za madaktari mnabadilishana. Wa hapa wanaenda kule, wa kule wanakuja hapa kwa muda. Jamaa akanogewa akahamia hapa na mkewe na watoto wao wawili. Kanunua Hekalu Bahari beach na namba yake ya Vodacom imesajiliwa kwa jina lake. Nilichoka! Na kuna wabongo asilia wanasota mwaka wa 10 huu hawana vitambulisho... waafrika bana πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ™ŒπŸΎ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…