Very bad! Soma tena ulichoandika halafu kirejee. Kitu kisicho na busara na kibaya kabisa kwa taasisi nyeti ya nchi hii. Tuviheshimu vyombo vyetu vya dola.🙏🙏🙏Tanzania kwamba kuna usalama wa taifa au waganga njaa
Mtu anawaza kujenga kwao, anawaza kusomesha watoto wake na ndugu, madeni utawaza kulinda nchi?
Wakubwa ndio wanakula, nchi yetu mishahara bado sana
Ameongea uongo?Very bad! Soma tena ulichoandika halafu kirejee. Kitu kisicho na busara na kibaya kabisa kwa taasisi nyeti ya nchi hii. Tuviheshimu vyombo vyetu vya dola.[emoji120][emoji120][emoji120]
Hata akishauri je, kitafanyika chochoteSidhani kama ni sahihi sana kuandika headline ya aina hiyo. Umeangalia hayo maeneo ya kisekta na line zake za uwajibikaji? Huwa nasikitishwa sana tunapotoa tuhuma za jumla kuhusu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wakati hadi sisi walima mchicha vijijini tunaona nchi imetulia. Mwisho, kama wewe una uchungu na nchi basi shauri what should he done...ndiyo uzalendo huo.[emoji120][emoji120][emoji120]
Soma tena kwa umakini utapata hoja yangu.Sidhani kama ni sahihi sana kuandika headline ya aina hiyo. Umeangalia hayo maeneo ya kisekta na line zake za uwajibikaji? Huwa nasikitishwa sana tunapotoa tuhuma za jumla kuhusu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wakati hadi sisi walima mchicha vijijini tunaona nchi imetulia. Mwisho, kama wewe una uchungu na nchi basi shauri what should he done...ndiyo uzalendo huo.🙏🙏🙏
Hasomagi,ushahidi mkataba/makuliano kati ya TPA na DP worldMtag mheshimiwa Rais moja Kwa moja Ili asikie na kusoma mwenyewe,hizi habari za kupelekewa ni za kidwanzi
Yeye mwenyewe alishasema huwa anapita humu
Imagine eti ukarabati wa uwanja wa Taifa wa mpira, gharama ni billion 31, na hakuna anayeshtuka.For sure taifa letu linahitaji kiongozi atakeyefumba macho na kufanya kitu kizito mnoooooooo
Yani unapata nafasi! Unafanya assassination kwa wapuuzi wote kama mzee wa mizizi na familia yake yote ili upuuzi usijirudie.
Sasa uchumi mbovu, Rushwa juu, nidhamu ya watumishi hakuna, hakuna ufanisi kwa mawaziri na rais wao lakini TISS wapo tu kama majuha!
Wanafurahi kuvaa nguo nyeusi na vidude vyao masikioni wanaona wameweza maisha ila kichwani weupe!
No vetting yani nothing special kuwapata hawa watu then tutegemee tutoboeee? Kweliiiiiiiii
Hapa tuna TISHI sio TISS
You shithole!Acha ubahili. Unaendekeza ubahili halafu unakuja lia lia hapa. Utakuja pata kitambulisho ukiwa umezeeka sana au umefariki wakuchukulie ndugu zako.
Maoni yako ni muhimu sana, ni idara nyeti sana ila kwetu imekosa maana.HII IDARA IFUTWE TUJE NA FORMAT MBADALA, WANAKOSA MAANA KABISA, WAMEKUWA MACHAWA CHAWA.
Movies zinawaharibu sana. Halafu tiss kazi zao sio maonyesho na kwakuwa hawaripoti kwako basi ukabaki kuamini uyaonayo ktk movies.Mkuu, mimi nimeangalia TV Series ya Homeland, The Americans, The Spy na kuona namna Secret Service wanavyokua wazalendo kwa nchi zao na namna wanavyopambana kupata habari za kiuchumi au hata kuharibu uchumi wa washindani wao ili nchi itoboe..dah yaani mpaka naona aibu kusema kuwa Tanzania tuna idara inaitwa usalama wa Taifa.
Alikuja Bill Gates hapa akawa Tanga kwenye ishu zake za Maralia, usalama wa Taifa hawajui kama yupo nchini. Alipopigwa picha na watu na zikasambaa mitandaoni ndio JPM akamwalika ikulu. Sasa mtu kama Bill Gates anaingia nchini na kuondoka bila kujikana, hapo tuna TISS kweli?
Kawaida inatakiwa TISS wajue leo Bakhresa au Mo Dewji amelala wapi, anafanya nini nk maana hawa jamaa ndio wanaorun uchumi wa nchi kwa biashara zao, wanazalisha ajira nyingi na wanachangia pato kubwa la nchi. Sasa cha ajabu unaambiwa Mo Dewji ametekwa nje ya gym na usalama wa Taifa wamelala kusubiri kusimamia mitihani.
Tuliambiwa na wamarekani hapa kuwa Jihad John (yule mchinjaji wa ISIS) akiwahi kuingia hapa nchini mara 2 kupitia JKNIA na TISS hawakujua. Sasa unafikiri kuna majasusi wangapi wanaingia nchini kwa njia hizi za wazi, Bandari au Airport na hawajulikani? Tunafahamu wanakuja kufanya vitu gani?
Lakini mbona wana viapo vya kulitumikia Taifa. ? Na viapo vya akina Justine Mahiga (RIP) ndio hivyo hivyo walivyoapa hawa. Inakuwaje leo hatuna watu kariba ya kina Mahiga RIP...Wanatakiwa wabadilishiwe na jina maana wanalinajisi Taifa letu kwa kuitwa usalama wa Taifa. Wanatakiwa waitwe usalama wa serikali Ili nchi yetu ibaki salama na genge hili.
Kwa ujinga woote unaofanyika wao wanasaidia nini sasa kulilinda Taifa kama ndo kwanza wanalewa na kushiba mvinyo na rushwa za wazungu????
"...mkono wa chuma..."Bwana Mwesigwa kada wa UVCC/afisa wa TISS aliwahi kuchaguliwa kuwa mkurugenzi wa TPDC.
Kila siku huwa narudia kusema humu ndani, ila naonekana kama kichaa. Bila kuiondoa kinguvu ile MIZEE YA COLD-WAR kwenye mfumo hatuwezi kufika popote kama taifa.
Binafsi, huwa napenda mbinu aliyoitumia Xi Jinping baada ya kuingia madarakani. Alivunjilia mbali idara ya ujasusi (The 610 Office) yenye maofisa 15,000 iliyokuwa inatumiwa na Raisi Mstaafu Jiang Zemin na genge lake la Shanghai (The Shanghai Clique) kuongoza nchi kwa mlango wa nyuma. Intelijensia imevunjwa na Jiang Zemin na mtoto wake fisadi wakatikwa kizuizini. Bila kufanya hivi napa Tanzania kwa bwana yule hatuwezi kufika nchi ya ahadi.
Xi Jinping akaenda mbali, akamshughulikia Waziri Zhou Yonkang ambaye alikuwa anaongoza (The 610 Office) na kikosi maalumu chenye askari 8,00,000 ambao wanatumika kuidhibiti Tibet na Xinjiang. Huyu jamaa alipoona Xi amekuwa Raisi na ameanza kugusa wakubwa kama Bo Xilai, akaanza kuvikusanya vikosi vya maelfu ya makomandoo wakisingizia mazoezi, kumbe wanataka kufanya yao kimyakimya. Bahati mbaya wakawaiwa na kukatwa vichwa.
Huyu Bo Xilai ni mtu aliyekulia ndani ya mfumo kwasababu baba yake alikuwa ni kigogo wa serikali ya Raisi Mao. Ilitegemewa yeye ndiyo aje kuwa Raisi wa China, lakini akakosa. Jamaa alikuwa na nguvu kubwa mno, maana ndani ya china alitumia mifumo ya kijasusi kujijenga kisiasa. Ilifika kipindi alikuwa anadukua hadi mawasiliano ya Raisi aliyepo madaraka Hu Jintao, na kupeleka taarifa kwa Jiang Zemin ambaye ndiye alikuwa The God-Father wa genge la Shanghai. Unamdukua Raisi na kumtishia kweli, ??? HAIWEZEKANI HATA KIDOGO.
Mpaka sasa, Xi Jinping ameshughulikia maofisa na makada wa Uchina wasiopungua milioni 5 ambao walihusiana na Jiang Zemin, Zhou Yonkang na Bo Xilai. Majasusi wote ambao walikuwa wanijifanya ni watiifu kwa genge la Raisi Mstaafu walipigwa risasi hadharani, kunyongwa, kufungwa au kupelekwa Laogai (The Gulag). Bila kufanya hivi sidhani kama angetawala hata mwaka mmoja.
Huku kwetu ni kinyume kabisa, waliohujumu nchi na wahaini, wanajengewa makasri ya mabilioni ya fedha, huku wake na watoto zao wanapewa ubunge na uwaziri. Kiufupi tu, kuna changamoto kubwa mno ambayo bila kutumia mkono wa chuma haiwezi kuisha.
Lakini mbona wana viapo vya kulitumikia Taifa. ? Na viapo vya akina Justine Mahiga (RIP) ndio hivyo hivyo walivyoapa hawa. Inakuwaje leo hatuna watu kariba ya kina Mahiga RIPWanatakiwa wabadilishiwe na jina maana wanalinajisi Taifa letu kwa kuitwa usalama wa Taifa. Wanatakiwa waitwe usalama wa serikali Ili nchi yetu ibaki salama na genge hili.
Kwa ujinga woote unaofanyika wao wanasaidia nini sasa kulilinda Taifa kama ndo kwanza wanalewa na kushiba mvinyo na rushwa za wazungu????
Ila kumbuka na wao wamo kati ya hao wanasiasa, hata kati ya mawaziri na wakuu wa vitengo , idara, ...Wanakwamishwa na viongozi. Wai hupeleka taarifa kwa viongozi wao na viongozi ndio wafanya maamuzi. Shida ni kwamba viongozi ndio wana siasa? Unatarajia nn?
Lakini mbona wana viapo vya kulitumikia Taifa. ? Na viapo vya akina Justine Mahiga (RIP) ndio hivyo hivyo walivyoapa hawa. Inakuwaje leo hatuna watu kariba ya kina Mahiga RIPWanatakiwa wabadilishiwe na jina maana wanalinajisi Taifa letu kwa kuitwa usalama wa Taifa. Wanatakiwa waitwe usalama wa serikali Ili nchi yetu ibaki salama na genge hili.
Kwa ujinga woote unaofanyika wao wanasaidia nini sasa kulilinda Taifa kama ndo kwanza wanalewa na kushiba mvinyo na rushwa za wazungu????
Ila kumbuka na wao wamo kati ya hao wanasiasa, hata kati ya mawaziri na wakuu wa vitengo , idara, ...Wanakwamishwa na viongozi. Wai hupeleka taarifa kwa viongozi wao na viongozi ndio wafanya maamuzi. Shida ni kwamba viongozi ndio wana siasa? Unatarajia nn?
Mambo ya ajabu kweli!Barabara ya mwendokasi Mbagala inamashimo mengi sana, hivi sasa wameanza kupiga viraka.
Hapo namba mbili kumbe mambo yapo hivyoNi usiku mnene. Naamua kuandika DOKEZO hili.
Kwa uchungu wa yanayoendelea katika nchi yangu.
Katika mada hii, nitaomba wachangiaji kujadili kwa uwazi kabisa, na kuongezea mifano mingine baada ya hii nitakayokuwa nimeiweka hapa.
Lengo ni Nia njema kabisa kurekebisha pale tulipokosea na kusaidia WaTz ambao wanakosa kufaidi matunda ya nchi yao.
Hapa chini ni jinsi ambavyo mambo ya ovyo yanafanywa wazi na TISS wala hawafanyi kazi yao iliyotukuka.
1. NIDA na Utoaji wa NAMBA/Vitambulisho vya Taifa.
Hili jambo ni kubwa sana. Mimi nimelithibitisha. Na wote wanaofika kuhudumiwa katika ofisi zote za NIDA nchi nzima wanasema wazi.
Iko hivi, huwezi kufanikisha kupata namba ya NIDA ikiwa huna kiasi fulani cha fedha. Na huwezi kupata ile ID ikiwa huna kiasi kikubwa zaidi cha fedha.
Yani utaenda utafuata taratibu zote na kuwa na viambatanisho vyote, lakini huwezi kupata kimojawapo kati ya hivyo bila fedha. Kiufupi hadi mlinzi wa getini anajua hilo.
Baadhi ya Ofisi za NIDA DSM kupata namba ya NIDA inaanzia sh. 150,000/-. Kupata ID ni kuanzia sh. 500,000/-
Lakini kadri utakavyoongeza dau maana yake utawahishiwa zaidi mchakato wako.
Kwanza hakuna huduma pale, zaidi ukifika upangwe foleni na walinzi, ukiingia unakuta mtu anachat tu, hadi jioni uambiwe njoo tena kesho.
Haya yana muda mrefu yanafanywa wazi kabisa. Hatari hii ni kwamba sasa hata mgeni je, akiwa na milion zake mbili si anapewa zake ID kama MTz??
Mh. Rais wetu ni msikivu, je, ulishasikia amepewa ripoti hii akashindwa kuifanyia kazi?!
Nani wa kumpelekea ripoti kama sio TISS?
2. Mradi wa mwendokasi Mbagala
Huu mradi nendeni mchunguze, ni mbovu na umejengwa chini ya viwango vibaya mno.
Uchunguzi unaonesha baadhi ya miundombinu kuanza kuharibika hata kabla ya matumizi rasmi kuanza.
Wasichokijua ni kwamba hii miradi ya miundombinu ya barabara huwa na zaidi ya miaka 20 ya uhai kabla ya marekebisho.
Sasa ukifika pale ukakuta baadhi ya beacon zimeanguka, kumeguka, n.k, Unajiuliza shida ni nini? Bajeti ndogo ya ujenzi? Lakini hilo linakataa kwa sababu hizi fedha ni mkopo tumepata kutoka Benki ya Dunia (WB), hawawezi kutenga fedha chini ya inayotakiwa.!
Sasa vile vituo vya abiria ndio utacheka kabisa. Mabati ni chini ya viwango, hizo frame walizichomelea ni chini ya viwango, uchomeleaji wenyewe ni wa dizaini za fundi maiko.
Hata wakibisha, nawahakikishieni, barabara ya mwendokasi ya Posta KIMARA itadumu, na hii ya Mbagala itakuja kuharibika mapema kabla yake. Tuko hapa mtakuja kuthibitisha panapo uhai.
Sasa kwa hali hii, utasema Rais wetu alivyo msikivu, ana hii ripoti mezani kweli? Na hatujasikia akichukua hatua zozote?
3. UHABA wa petrol sasa hivi nchini.
Hapa siandiki sana.
Fahamuni kwamba mafuta yapo. Si mlisikia hata Waziri anasema hakuna upungufu wa petrol. Si amesema mara nyingi tu!
Sasa Mimi na wewe tuulizane, Waziri anasema yapo, vituoni ukifika hakuna, yapo wapi? Eeh...
Jamaa wana mafuta, ila hawatoi kuyauza. Wanasubiri bei mpya za August, zipande usiku wa leo tarehe 31/07/2023 ndio wataanza kutoa mafuta.
Sasa "syndicate" ya namna hii, hapo unasema TISS wapo na wananchi, au wametuma ripoti Rais hajachukua hatua?!
Achaneni na mambo ya ooh Dola $ kuadimika, hiyo inaathiri uagizaji wa mzigo mpya. Sio stock iliyopo ambayo huagizwa miezi mitatu au zaidi nyuma.
4. Nauli za mabasi za LATRA.
Hivi mnajua mabasi yote ya mikoani katika stendi zote za mikoani wanachaji nauli zaidi ya zile zilizoidhinishwa na LATRA?!
USHAHIDI upo.
Hapa namaanisha hata LATRA na mapolisi wanalijua hilo. Je, ni fungu wanapewa au kuamua kuacha tu unyang'anyi huu uendelee?!
Nasisitiza iko hivyo, stendi zote, mikoa yote.
Nenda Dsm, Mwanza, Morogoro, Iringa, Dodoma, Tabora, Kagera, Mbeya, Arusha, Tanga, Mtwara, Kigoma, n.k, kote huko wana 'overcharge'.
Sasa kama watu wa mabasi wanaona nauli zilizopangwa ni ndogo, haziwapi faida, si bora LATRA ipitishe hizo hizo wanazolipishwa wananchi ili ifahamike moja.
Je, unataka kusema ripoti za haya zipo mezani kwa mh. Rais ila jinsi alivyo anajali watu wake kweli asichukue hatua.?!
Narudia ripoti hii ni kwa nia njema ya kujenga Taifa letu.
Ukweli huduma za umma zimezorota kiasi kikubwa, tusifiche tatizo na wananchi wengi wanaumia sana na hili.
Naomba kuhitimisha hapo kwa leo.
Karibuni wachangiaji kwa mengi zaidi.
Hauamini kama Bill Gates alikuja Tanzania? Hauamini kama Mo Dewji alitekwa na kuachiwa na watekaji bila watekaji kujulikana? Hauamini kama Jihad John ametua JKNIA mara 2??Movies zinawaharibu sana. Halafu tiss kazi zao sio maonyesho na kwakuwa hawaripoti kwako basi ukabaki kuamini uyaonayo ktk movies.