TAKUKURU, Polisi waja na muarobaini wa rushwa za barabarani wakishirikiana na wadau

TAKUKURU, Polisi waja na muarobaini wa rushwa za barabarani wakishirikiana na wadau

Vibao vya speed limit ya 50/km ndio chanzo kikuu cha hawa mabwana kudai virushwa vya kipumbavu.

Hivi vibao vimeshapitwa na wakati. Wangeweka hata most places speed limit iwe 80km/hr. Unakuta eneo lipo wazi barabara imenyooka ila speed limit ni 50. Na hawa ndio vinajibanza hayo maeneo kuvizia dereva atembee hata na 52km/hr wamtishie kumpiga fine au waombe kitu kidogo.

Kwahiyo TAKUKURU acheni unafiki, serikali ndio inawapa jeuri ya kuomba rushwa hawa jamaa na sio kwamba wao wenyewe ndio wanaamua.
 
LESIRIAMU,
Kiutumishi kina maadili ya utumishi TAKUKURU wakipitia huku watawabana wengi. Pili kuna ngazi za mishahara za watumishi zimenainishwa kwenye circular. Ajabu utakuta Mtumishi wa Umma anashindana na mfanyabiashara.

Gari kubwa injini Ina 4200cc.3500cc 2400cc hawana hofu tinted ya kutosha. Nyumba kubwa fensi hatari unajiuliza maadili yako wapi na unajiuliza huyu mtumishi ana biashara gani kwenye ofisi za umma.

Suala la rushwa mmomonyoko wa maadili Na Ni kukosa uzalendo na kazi yako. Turudishe maadili tuanze sasa na ofisi ya maadili na utumishi wapo kwanini hawakushirikishwa?
 
Huku horohoro kwetu...yaaani mpakani kenya-tanzania wasomali ndio illegal transit route wanakimbilia south africa, sasa traffic akichungulia akiwaona hao jamaa Basi wote mnaomba passport, sasa hao jamaa hawana...

Basi traffic na konda wanaenda nyuma ya Basi wakirudi kazi imeisha safari inaendelea.....

Kwa rushwa hii tumekuwa njia ya kupitisha haramu na la Shabaab pia.
 
Tuchekelee tu ila wakianza kusimamia sheria ya kulipa kiwango chote 30,000 naomba tuchekelee pia maana we una makosa zaidi ya moja unatozwa kisela buku 5 unasepa.

ANYWAY HII NCHI KWA SASA NI KUUMIZANA MPAKA TUTIE ADABU.
 
Punguza trafiki barabarani ndio suluhisho kamili, tuache utani jamani.
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) leo imefanya maongezi ya kimkakati na Wadau mbalimbali wakiwemo Sekta Binafsi, Sekta za Umma, Asasi za Kiraia, Taasisi za Dini, Vyombo vya Habari, Viwanda vya Uchapaji na Uchapishaji, Kampuni za Simu, Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri, Wasanii, Madereva wa Vyombo vya Moto na Wananchi kuelezea Kampeni inayotarajiwa kuzinduliwa ya kupunguza ama kutokomeza kabisa rushwa Barabarani.

TAKUKURU imeeleza kuwa Kampeni hiyo imepewa jina la ‘UTATU’ ikimaanisha ni muunganiko wa pande Kuu tatu: TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Wadau

Imedaiwa kuwa lengo kuu la kampeni ni kuzuia rushwa za barabarani ambayo imebainika ni kisababishi kimojawapo cha ajali zinazotokea barabarani; tatizo ambalo limekuwa likikemewa sana na viongozi mbalimbali wa Serikali. Aidha imesema UTATU huo unatakiwa kuweka mikakati ya pamoja na endelevu ya kutibu tatizo la ajali badala ya kulaumiana na kunyoosheana vidole.

Kampeni hiyo imejiwekea mambo malengo mahususi manne, ikiwa kila lengo linatakiwa kutekelezwa na kila mdau kwa nafasi yake:
  • Kudhibiti vitendo vya rushwa miongoni mwa wasimamizi wa sheria za barabarani
  • Kuandaa mkakati wa kuzuia vitendo vya rushwa barabarani
  • Kushirikisha Umma kuzuia vitendo vya rushwa barabarani
  • Matumizi ya TEHAMA kudhibiti vitendo vya rushwa barabarani
Kuhusu matumizi ya TEHAMA kudhibiti vitendo vya rushwa barabarani, TAKUKURU imesema tayari limeanza kutekelezwa kwa kutengeneza mfumo utakaotumika kuchukua matukio ya vitendo vya rushwa kwa kutumia simu ya mkononi (Mobile App).

Mfumo huo (Mobile App) utakaozinduliwa pamoja na Kampeni hii ya UTATU, utapakuliwa kutoka Play Store au App Store ya simu ya mkononi kisha mtu ataweza kupiga picha za video, mnato au sauti na kuzituma TAKUKURU.

Baadhi ya Majukumu ya Wadau wa Kampeni hii yametajwa kuwa:

Wasimamizi wa sheria na miundombinu ya Barabara (TANROADS, TARURA, LATRA na wengine)
Wanalo jukumu la kusimamia ubora wa miundombinu na Vyombo vya Usafiri ikiwa ni pamoja na
  • Kuboresha sheria, kanuni na miongozo
  • Kuboresha miundombinu ya barabara na mizani
  • Kusimamia usajili wa Vyombo vya Usafiri
  • Kuhakikisha alama za usalama barabrani zinaonekana vizuri
  • Kutoa taarifa za vitendo vya rushwa barabarani
Wasanii wa fani mbalimbali
  • Wana jukumu la kuhamsisha watumiaji wa barabara kupitia Sanaa zao zinazosisimua na kuburudisha huku ujumbe wao ukisaidia kubadili mitazamo ya watumiaji wa barabara kuacha vitendo vya rushwa
  • Wanatarajiwa kutoa michango yao ya kuandaa Sanaa zitakazohusiana na kampeni ya UTATU

AZAKI wao wametajwa kuwa wahamasishaji ambapo majukumu yao yatakuwa:
  • Kuhamasisha wananchi kutuma taarifa za vitendo vya rushwa barabarani
  • Kuhamasisha wananchi waache uoga wa kutoa taarifa za rushwa
  • Kutumia mtandao wao kutoa taarifa za vitendo vya rushwa
  • Kuhamasisha wananchi kuacha kutoa rushwa kwa masimamizi wa sheria za usalama barabarani
Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri ambao majukumu yao ni
  • Kusimamia Vyombo vya Usafiri ili kutoruhusu magari mabovu kuingia barabarani
  • Kuajiri madereva wenye sifa na kuwalipa vizuri
  • Kuacha kutoa Rushwa ili wapate leseni bila kufuata utaratibu
  • Kuwachukulia hatua madereva wazembe
  • Kuwasimamia madereva kuacha kutoa rushwa kwa wasimamizi wa sheria za usalama barabarani
Wamiliki wa Vyombo vya Habari ni kundi lingine ambalo katika Kampeni hii majukumu yake yamebainishwa kuwa
  • Kuelimisha wananchi kupitia Vyombo vyao vya Habari
  • Kusaidia kutoa nafasi kwenye Vyombo vya Habari na kurusha matangazo kuhamasisha kampeni
  • Kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa

Wamiliki wa Viwanda vya Uchapishaji na Uchapaji wao wataweza kushiriki kwa:
  • Kusaidia kuchapa machapisho ya kuhamasisha kampeni
  • Kutoa taarifa za vitendo vya rushwa
Vingozi wa dini wao wana majukumu muhimu ya
  • Kufundisha maadili kwa waumini wao ili wasitoe rushwa kwa wasimamizi wa sheria za usalama barabarani
  • Kutumia Vyombo vya Habari vinavyomilikiwa na dini zao ili kuhamasisha kampeni
  • Kutoa taarifa za vitendo vya rushwa

Katika mkutano huu, wadau walioshiriki kutoa maoni wamedokeza haya:-

Kwanza, wamesema Rushwa ni mtazamo wa ndani ya Polisi na nje ya Polisi, watu wanaona Polisi ni fursa. Kwenye vitengo vinavyoongoza kwa rushwa ni pamoja na kwenye kutoa leseni, ukaguzi wa barabarani. Polisi walio kwenye Pikipiki maarufu kama ‘tiGO’ na madereva wa magari ya Kirikuu wanaodai kuwa wakipita ni lazima wasimamishwe na kuombwa rushwa

Aidha, wengine wamehoji kwanini TAKUKURU hawapo barabarani? Huku wengine wakisema ni bora adhabu ziongezwe kwenye makosa ya barabarani na adhabu ya fedha iondolewe kabisa.

Wengine wakiwemo Viongozi wa Dini wametoa maoni kuwa hofu ya Mungu ndio suluhisho pekee la tatizo la rushwa kwa wananchi wanaweza kuwaepuka TAKUKURU na Polisi ili wasikamatwe kwenye masuala ya rushwa. Pia, Polisi wakiwa na hofu ya Mungu wanaweza kukataa rushwa na kuwakamata wanaotaka kutoa na hivyo kuzuia rushwa.

Lakini, kuhusu App TAKUKURU waliyozungumzia wadau wamesihi sana kuwa kunatakiwa kuwe na elimu ya awali itakayotolewa kwa Wananchi kabla ya kuanza kutumia App hiyo na pia kuwapa muda Wananchi kuielewa.

Wametaka pia Makamanda wa Polisi na watumishi waboreshewe maslahi kwa kuwa hiyo inaweza kuwa njia mojawapo ya kuzuia rushwa.
Hongereni kwa kukaa kikao hicho na mkalipana na posho kuzungumzia zimwi ambalo hamuwezi kuliua nchi hii. Suala la rushwa Polisi ni kama KPI (key perfomance indicator) kwao, imefika hatua polisi wao kwa wao wanashindana kupaua msauzi, wanashindana kununua magari na kugawana magari na pikipiki zilizo kaa muda mref kituoni baada ya kukamatwa, wamachomoa vipuri kwny magari hayo na vipuri hivyo. Imefika hatua katika nchi hii ni bora ukutane na jambazi mwenye silaha ukimpa hela na simu anakuachia huru, ila ukikutana na polisi watakuchukua hela zote na watakubambika kesi na kesi yoyote hata ya mauaji. Imefika hatua sasa polisi wanapasiana taarifa za wahalifu ili kila polisi aende akachukue hela kwa muhalifu wanamgeuza shamba la bibi maisha yake yote,(ukiwa na duka la vipodozi utalea polisi wote wa eneo ulipo mpaka mkuu wao). Imefika hatua mwananchi akiingia kituo cha polisi anaweza ugua ugonjwa wa moyo kwani atakayo kutana nayo mule ataambiwa ameua. Imefika hatua ukikutwa na simu ya mtu unabambikiwa na kesi ya mauwaji. Gereza zimejaa mahabusu na wafungwa walio onewa kisa hawakutoa rushwa, ama hawana connection na watu wakubwa . Katika nchi hii Polisi wa kawaida tu Koplo au Inspekta anaweza kuwa na kipato cha juu kuliko afisa mwandamizi wa kada nyingine serikalini. Polisi akila rushwa hata TAKUKURU hawahangaiki nae hii nchi inasikitisha sana nadhani kuna siri kubwa serikali inayo juu ya watu hawa.
 
Roving Journalist,
Kwa matrafki barabarani serikali iweke faini 10,000 badala ya 30,000 kwa kosa.Mtu akikamatwa na kosa iwe ni rahisi kulipa elfu kumi serikalini na akapewa na risiti yake. Hii elfu 30 ndo mzizi wa tatizo inafanya polisi kujiona miungu watu na wanakubambika makosa watakavyo wao na ukweli ni kwamba elfu 30 ni kubwa na inakaribisha mazungumzo ya rushwa na serikali kupoteza mapato yake kwa hawa wapuuzi.
 
Maisha ya Polisi wala rushwa yatakuwa magumu sana

Binafsi siamini hivyo. Hivi kuna polisi asiyekula rushwa? Polisi usalama barabarani mbona wanachukua rushwa hadharani? panda daladala ndipo utaona wengi wa trafiki wana magari binafsi ambayo yamepatikana kwa fedha za rushwa.
 
Back
Top Bottom