TAKUKURU Songwe yamrejeshea mkopaji nyumba ya TSh165 milioni

TAKUKURU Songwe yamrejeshea mkopaji nyumba ya TSh165 milioni

kisheria apaswi kulipwa kwa sababu kwanza hapo kafanya makosa mengi.

Moja ni kufanya biashara ya kukopesha kinyume na sheria kwa kukosa leseni benki kuu.

Ukwepaji wa kodi, kwa kuwa biashara iyo haitambuliki, maana hayo mapato haramu hayatotozwa kodi.

Kwa kupokea na kutumia hayo mapato ya riba kinyume na sheria, inaweza kutafsiriwa kama utakatishaji wa fedha.

Kwa iyo kurudisha tu iyo dhamana (nyumba ) iliyokwa rehani wamemsaidia tu mkopaji maana anastahili adhabu nyingi.

Ikitokea mtu anashida alafu akakuambia umkopeshe pesa na atakurudishia zaidi ya iyo kwa kuda mfupi ama mrefu kwa kukupa dhamana yoyote usikubali kwa maana akilalamika kwenye vyombo husika utakosa yote pamoja na kuingia matatani.

Ika watu hukopeshana mitaani na sio taasisi za kifedha wanatumia mikataba wa kimaandishi tu, kuna kosa gani
 
Hatima ya mdai vipi? Maana yupo kwenye makubaliano bado alipwe chake, na mtu uanwezaje kukopa pesa ya milioni 15 ukaweka dhamana nyumba ya milion 165 hizi ni akili ama
Yaani nikama akili za kushikiwa au kurogwa sio bure
 
Mkopo unaohusisha nyumba unaupeleka kienyeji duu!
 
Ika watu hukopeshana mitaani na sio taasisi za kifedha wanatumia mikataba wa kimaandishi tu, kuna kosa gani
kukopeshana ni jambo la kawaida lakini riba ikihusika hiyo ni biashara kama biashara zingine inapaswa kufanyika kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.
 
Kwaa hiyo haki ya mkopwaji hapo ni ipi?
Kwa kuangalia hapo anaonekana kama alidhulumu wakati ilikuwa ni makubaliano ya watu wenye akili timamu. Wameshamliza, na maboresho aliyofanya je?
 
kukopeshana ni jambo la kawaida lakini riba ikihusika hiyo ni biashara kama biashara zingine inapaswa kufanyika kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.
Mkuu vipi nikisaini contract ya kumkopesha mtu, kisha nikaenda kwa registrar ingawa ni hela nyingi na muda mfupi labda tufanye kakopa 10M na tumekubaliana alipe 15M within 15 days.

Kisheria akinishtaki nina hatua?
 
Mkuu vipi nikisaini contract ya kumkopesha mtu, kisha nikaenda kwa registrar ingawa ni hela nyingi na muda mfupi labda tufanye kakopa 10M na tumekubaliana alipe 15M within 15 days.

Kisheria akinishtaki nina hatua?
hayo makubaliano yatakua ni batili kwa sababu hauna leseni ya kufanya biashara ya kukopesha fedha.

hapo kwenye faida ya milioni 5, kuna kodi ya asilimia 10, kwa mujibu wa income tax act ( ambayo utakua umeikwepa) na kosa la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha

namna pekee ya makubaliano hayo kuwa sahihi ni kama ungekopesha milioni 10 na kutarajiwa kulipwa milioni 10 (bila riba)
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Songwe imeokoa nyumba yenye thamani ya Sh165milioni iliyochukuliwa baada ya mmiliki kushindwa kurejesha mkopo wa Sh15milioni mali ya Jacob Masebo (62).

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe, Damas Suta amesema, Masebo alikopa Sh15milioni miaka 11 iliyopita kutoka kwa Richard Kalonge, ambapo alipaswa kurejesha TSh33 milioni baada ya siku 18 ambazo hata hivyo mkopaji alishindwa kurejesha hali iliyosababisha mkopeshaji kunyang'anya nyumba ambayo iliwekwa kama dhamana.

Suta amesema Kalonge alipoichukua nyumba hiyo yenye ghala kubwa moja, maghala madogo mawili na vyumba vitatu vya maduka, aliibadilisha jina na kutengeneza hatimiliki ya kudumu kwa jina lake, jambo alilosema ni uonevu kupitia mikopo umiza.

"Tulipomhoji Kalonge alisema nyumba hiyo imekuwa ikimwingizia Sh3 milioni kila mwaka zinazotokana na kupangisha," amesema Suta.

Naye Mkuu wa wilaya Mbozi, John Palingo amewasihi wananchi kuwa makini wanapofanya makubaliano yoyote kwa kuelewa vizuri mkataba ulivyo ili waepuke kuingia mikataba yenye makubaliano yenye utata.

Kwa upande wake Jacob Masebo amesema alilazimika kuchukua mkopo huo baada ya kukosa mkopo alioomba benki na kwamba alitaka fedha hizo ili akamilishe ujenzi wa jengo hilo.

"Sielewi kilichotokea, niliomba mkopo benki walituma wataalamu wa uthaminishaji lakini baada ya muda mrefu waliniambia mkopo umeshindikana," amesema Masebo.


Mwananchi
Duuuh hongera pccb kwa kumsaidia huyo jamaa
 
MASEBO ndiyo mndali tiiiii[emoji38] ila akina KALONGE pia ni wandali ila hawa ni watu waliotoka ileje wakakimbilia Mbozi tena wa huko Itaka wanakolima sana kahawa, wanyakyusa huitwa KANDONGA, kama sijamix[emoji38]
Daaa hapo Itaka Nilkaa Sana Enz za Jkt nimewamis watu wa kule''' maana walkua washamba mnoo
 
Hahahaaa, mkuu acha kutudharau wanyiha bc 🤣🤣🤣
Ila hujakosea, wale jamaa sijui wapoje, tofauti na wasukuma sioni. Yani yakiwa na hela kipindi cha mavuno hususani ya kahawa mwezi wa saba hivi yanakuwaga na viburi, utasikia "Naweza kukupiga alafu nikulipe"😁😁
Ushamba wao, yanaweza kwenda mlowo pale mjini au vwawa mjini yakiingia dukani mwako sema asante Mungu. Utasikia, "Nahitaji nguo yenye bei kubwa kuliko nguo zote" au nipe redio ya bei kadhaà, au nipe nguo kama ya fulani ambaye hayupo pale na muuza duka hamjui, et alinunua bei kadhaaa🤣🤣,
So ulichosema ni sahihi coz nawafahamu vzr wale jamaa na ni karibu na home kwetu.
Daaa hapo Itaka Nilkaa Sana Enz za Jkt nimewamis watu wa kule''' maana walkua washamba mnoo
 
Back
Top Bottom