A
Anonymous
Guest
Hapa Halmashauri ya Wilaya Karagwe, Mkoa wa Kagera kuna changamoto kubwa ya kukosekana kwa uadilifu na uwajibikaji unaofanywa hasa na Walimu Wakuu wa Shule pamoja na Ma-Afisa Elimu katika ngazi ya Shule za Msingi.
Inapotokea kuna tenda Mkandarasi anapata inayohusu Shule fulani, ili uweze kupata tenda hiyo unatakiwa ukubali ufanye kazi kisha kabla ya kupata malipo yako, wewe Mkandarasi uwape Walimu Wakuu na Afisa Elimu ‘kitu flani’ ili malipo yako yaweze kupitishwa.
Wakandarasi wanapokamilisha mradi au unapokuwa katika hatua fulani nzuri ukihitaji malipo, yanatakiwa yapite katika ngazi Tatu ikiwemo kwa Afisa Elimu na Mwalimu Mkuu.
Licha ya kuwa tenda kwa sasa zinatangazwa na Shule moja kwa moja na wale Wakandarasi wanazungumza na Walimu Wakuu lakini ukihitaji malipo wanakwambia “Afisa Elimu amekataa kusaini kwa kuwa hakuna fungu lake.”
Wale Wakandarasi wakienda kwa Afisa Elimu anawaambia “Mimi sijawapa tenda, nendeni kwa Walimu mliozungumza nao.”
Mkurudi kwa Mwalimu Mkuu anawaambia ukweli na kuwaonesha nyaraka kuwa mzigo haujasainiwa kwa kuwa Afisa Elimu bado “hajafurahi”.
Wakandarasi wakisema walipwe kisha watoe ‘kifuta jasho’ jamaa wanagoma kabisa, mara kadhaa wameamua kutoa mifukoni mwao ili kuona kama hilo litafanyika, wakishafanya hivyo tu malipo yanafanyika fasta.
Unakuta tenda zenyewqe sio za hela kubwa lakini hapohapo unatakiwa kugawana nao kitu ambacho kinawaumiza Wakandarasi.
Kwa umoja wetu tumeona sehemu sahihi ya kufikisha ujumbe wetu Serikalini hasa kwa TAKUKURU, Wizara ya Elimu, TAMISEMI pamoja na kwa Rais Samia Suluhu ni kupitia hapa Jamii Forums ili hatua zichukuliwe kwa kuwa wanaoumizwa na hali huyo ni wengi.
Kwa ufupi Watumishi wa Serikali hao wajuu wanatuumiza sana sisi Wakandarasi wadogo, na ukigoma kutoa ushirikiano kwanza kama unadai haupati hela zako na kama umeshalipwa ukaonekana unachonga haupati dili tena.
Risiti za malipo yote tunazo, tunasubiri TAKUKURU waoneshe ushirikiano tutawapa, pia kuna muda wanataka wapewe kifuta jacho mkononi tumewapiga picha pia, zote tuko tayari kuziwasilisha kwa Mamlaka wakizihitaji.