TAKUKURU waagizwa kuchunguza jengo la zahanati lililotumia Tsh. Milioni 75 na halina milango wala madirisha

TAKUKURU waagizwa kuchunguza jengo la zahanati lililotumia Tsh. Milioni 75 na halina milango wala madirisha

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1665607097833.png
Mwonekano wa jengo la zahanati ya Kijiji cha Mtakuja iliyopo Wilaya ya Ruangwa ambayo imeshatumia Tsh. Milioni 75 hadi sasa.

1665607248257.png

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU wilayani Ruangwa kufanya uchunguzi wa matumizi ya kiasi cha shilingi 102,080,357.14 zilizotolewa na Serikali kupitia TASAF ili kujenga zahanati ya Kijiji cha Mtakuja na kuwasilisha taarifa ya uchunguzi huo kwake kabla ya kuhitimisha ziara yake mkoani Lindi.

Ndejembi ametoa maelekezo hayo baada ya kukagua na kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Mtakuja, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Amesema hajaridhishwa na taarifa ya ujenzi huo kutokana na mapungufu yaliyomo ikiwa ni pamoja na kiasi cha Tsh. Milioni 27 tu zilizobaki kwenye akaunti kati ya Tsh. milioni 102 zilizotolewa na TASAF, hivyo hakitoweza kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Kutokana na mapungufu yaliyobainika Waziri Ndejembi amemuelekeza Kamanda wa TAKUKURU kuhakikisha anafanya uchunguzi maalum na kumchukulia hatua yeyote akatayebainika kuhusika na ubadhirifu wa fedha za umma.

HABARI LEO
 
Wapumbavu hao wanadhani na hizi gharama za ujenzi kupanda hiyo pesa ingelitosha kujenga zahanati yote...tena jumba lenyewe kubwa hivyo....wanaona wananchi mburula sana,kwamba tunabebeka na kisurisuri cha jpm
 
Hivi nchi hii huko vyuoni wanakofundishwa wataalam wetu kuna mtaala unaofundisha wizi!!?
 
Wameiba hapo wakishapiga kelele wezi wanajipanga..mbinu wanayotumia kukamata wezi kwa kupiga kelele ni ya zamani mno..
 
Hoja mfu na ya kijinga sana hii. Kwani milango ndiyo inaamua jengo ligharimu milioni 75?
 
Hii nchi buana.

Waziri mwenyewe anatafuta pa kupiga maisha yasonge.
 
[emoji16][emoji16][emoji16].yaani kwa kuangalia tu Hilo jengo.
WAMEPIGA.
 
Miaka nenda rudi ni kuchunguzachunguza hakuna kipya, kama wanachukia ufisadi mbona hawatungi sheria kali kukomesha ubadhirifu, wanatunga sheria za kijinga za tozo zisizosimamiwa vizuri
 
Mkitaka kuthibiti huu wizi.serikali nunueni material ya ujenzi wenyewe na mafundi tafuteni wenyewe.
Msiwape hao viongozi hela.
Na kila kitu kiandikwe.
Kuanzia ujenzi unaanza mpaka mwisho.
 
Wapumbavu hao wanadhani na hizi gharama za ujenzi kupanda hiyo pesa ingelitosha kujenga zahanati yote...tena jumba lenyewe kubwa hivyo....wanaona wananchi mburula sana,kwamba tunabebeka na kisurisuri cha jpm
TAKUKURU wanatumika vibaya siku hizi.kila kitu takukuru chunguza sijui hiyo taasisi imesheheni kiasi gani cha watalaamu.yaani kila fani wao wanao!ni ajabu sana.huku ni kuwadhalilisha watendaji waserikali.tuukatae huo upuuzi.tudai katiba mpya.
 
Ukaguzi watakiwa uwe wafanyika, wakandarasi walipe gharama zilizozidi.. hii itasababisha uhuni uishe
 
Back
Top Bottom