DOKEZO TAKUKURU Wakamateni Sheikh, Alhad Mussa Salum, RITA, Mkurugenzi, Ardhi na Polisi kwa kuvunja Msikiti wa Mwenge kwa Mabavu

DOKEZO TAKUKURU Wakamateni Sheikh, Alhad Mussa Salum, RITA, Mkurugenzi, Ardhi na Polisi kwa kuvunja Msikiti wa Mwenge kwa Mabavu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

1663717843424.png

Picha maduka kiwanja cha Mwenge jijini DSM

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa​

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni​


Vibali vya Ujenzi​


KIBALI CHA UJENZI (BUILDING PERMIT)

TARATIBU ZA KUPATA KIBALI CHA UJENZI (BUILDING PERMIT)

1. KIBALI CHA UJENZI
Kulingana na Sheria ya Serikali za Mitaa Sura 288 (Urban Authorities) act (Cap. 288) (Development control Regulations, 2008, Mwongozo wa utoaji wa vibali vya ujenzi, 2018, si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya :-
  • Kutuma maombi kwa mamlaka ya mji husika.
  • Kuwasilisha michoro ya jengo na kumbukumbu husika.
  • Kupata kibali cha maandishi kinachoitwa Kibali cha Ujenzi.

2. KIBALI CHA AWALI:
  • Inashauriwa kupata kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi. Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (sketch plans scale) 1:00 1:200 akionyesha aina ya ujenzi atakaokusudia kufanya ili aweze kupata ridhaa ya kuendelea ha hatua za kuanzaa michoro ya mwisho.

Faida:
  • Kuokoa muda na gharama iwapo michoro ya mwisho itaonekana kuwa na dosari za kitaalam ambazo zitahitaji kufanyiwa marekebisho.
  • Kuwa na uhakika kuhusu mahitaji muhimu ya kuzingatiwa wakati michoro inaandaliwa.

3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA UJENZI
  • Baada ya michoro kukamilika, iwasilishwe ikiwa kwenye majalada kwa namna ambayo inaweza kufunguliwa na kusomeka michoro hiyo iwasilishwe kama ifuatavyo:-
  • Seti tatu za michoro ya jengo (Architectural drawings scale 1:100 & 1:50)
  • Seti mbili za michoro ya vyuma structural drawings (scale 1:50) kwa majengo ya ghorofa.

4. MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI:
Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:-
  • Namna jengo litalavyokuwa ”sections elevation”, "foundation”, “roof plan”, “site plan”.
  • Ramani ya kiwanja (location plan)
  • Namba na eneo la kiwanja kilipo
  • Jina la mmilikaji ardhi inayohusika
  • Jina la mchoraji, ujuzi na anwani
  • Ukubwa wa kiwanja kwa mita za mita za mraba
  • Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
  • Ujazo wa kiwanja (plot coverage).
  • Uwiano (Plot ratio)
  • Urefu wa jengo kwenda juu (Height)
  • Matumizi yanayokusudiwa
  • Idadi ya maegesho yatayokuwepo
  • Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks) na
  • Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo, au bomba la maji taka

5. VIAMBATANISHO:
  • Fomu moja ya maombi iliyojazwa kwa usahihi.
  • Hati ya kumiliki kiwanja au barua ya toleo au fomu iliyojazwa ya sehemu zisizopimwa.
  • Kumbukumbu nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo,
  • Makabidhiano n.k.
  • Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo.
  • Mabadiliko ya matumizi ya ardhi.
  • Ramani ya kiwanja iliyosajiliwa.

6. HATUA ZINAZOFUATWA WAKATI WA KUCHUNGUZA MAOMBI YA KIBALI
Zinafuata ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuchunguza michoro hiyo:-
Kuwasilisha michoro na kulipia gharama ya kibali cha ujenzi.
  • Uhakiki wa miliki
  • Kukaguliwa usanifu wa michoro
  • Kukagua kiwanja kinchokusudiwa kuendelezwa
  • Uchunguzi wa matumizi ya jengo na kuwepo kwa kiwanja katika ramani M/Miji (TP drawing)
  • Uchunguzi wa Maafisa Afya
  • Uchunguzi wa mipango ya uondoaji majitaka
  • Uchunguzi wa tahadhari za moto
  • Uchunguzi wa uimara wa jengo
  • Kuwasilisha kwenye kikao cha mipango Miji baada ya kukamilisha taratibu zote.
  • Hatimaye kuandika na kutoa kibali.

7. FAIDA ZA KUWA NA KIBALI CHA UJENZI
  • Kujenga nyumba ambayo imethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama.
  • Kuwa na mazingira bora kwa kuwa na mji uliopangwa.
  • Kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kutokea iwapo ujenzi umefanyika bila kibali ikiwa ni pamoja na kushtakiwa mahakamani kuvunjiwa na kulipa gharama za uvunjaji.
  • Kulipwa fidia iwapo jengo litabomolewa kwa sababu maalum.
  • Kuweza kupata mkopo kutoka Taasisi za fedha.

8. MUDA
  • Michoro itaidhinishwa ndani ya siku saba (7) toka mwombaji awasilishe maombi ya jengo la chini (mfuto). Na siku kumi nne (14) jengo la ghorofa. Aidha ndani ya muda huo mwombaji ataarifiwa sababu za michoro kutoidhinishwa kupata kibali cha ujenzi.

Bonyeza hapa kuona vibali vya ujenzi vilivyotolewa.

Source : Vibali vya Ujenzi | Kinondoni Municipal Council

IMG-20220526-WA0015.jpg


Picha: Mhe. Makala amefurahishwa na hekima za Manispaa ya Kinondoni kuamua kujenga msikiti wa kuabudia kwa waumini wa dini ya Kiislam kwenye eneo la mita za mraba 1000, baada ya msikiti wa sasa kuwa ndani ya eneo la stendi
 
Ndio maana yule Mzee semtumbi aliekuwa kang'ang'ania hati kuna muda alikuwa anauliza nini bodi isikope yenyewe ikajenga hayo maduka,alafu yakawa yanalipa hilo deni?hivi unajua pale kwa yale maduka tu kwa mwaka tu sidhan kama walikuwa wanakosa mil 100.na wewe kama ndio kati ya wale wanabodi,hivi mnadhani mngeshindwa kukopa hela na mkajenga wenyewe hayo maduka,kuliko kumpa mtu mkataba wa miaka 30 kweli?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Ile ni taasisi ya dini haiwezi kukopa kwa riba pia ili uwe na sifa ya kukopeshwa inabidi uwe na security inayozidi mara mbili pesa unayotaka kuikopa sasa uwekezaji unaowekwa pale unazidi 2 billion unapata wapi bond ya 4bilion?

Mkataba umeingiwa upande wa maduka pekee kumbuka Shule ya Secondary na Msikiti vinajengwa bure bila mkataba hata wa mwaka 1 kwahiyo manufaa yatapatikana kuliko hata maduka yanavyoingiza.

Mapato ya shule yanakadiriwa kuingiza 600milion kwa mwaka hayo yote yanaingia kwenye mfuko wa Taasisi kwahiyo kuwa na mkataba upande wa maduka ni faida kubwa hata ingekuwa mkataba wa miaka 100 na isitoshe kila mwaka upande wa maduka unaingiza pesa zaidi ya mapato yaliyokuwa yanapatikana awali kabla ya uwekezaji
 
Ndio maana yule Mzee semtumbi aliekuwa kang'ang'ania hati kuna muda alikuwa anauliza nini bodi isikope yenyewe ikajenga hayo maduka,alafu yakawa yanalipa hilo deni?hivi unajua pale kwa yale maduka tu kwa mwaka tu sidhan kama walikuwa wanakosa mil 100.na wewe kama ndio kati ya wale wanabodi,hivi mnadhani mngeshindwa kukopa hela na mkajenga wenyewe hayo maduka,kuliko kumpa mtu mkataba wa miaka 30 kweli?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Ile ni taasisi ya dini haiwezi kukopa kwa riba pia ili uwe na sifa ya kukopeshwa inabidi uwe na security inayozidi mara mbili pesa unayotaka kuikopa sasa uwekezaji unaowekwa pale unazidi 2 billion unapata wapi bond ya 4bilion?

Mkataba umeingiwa upande wa maduka pekee kumbuka Shule ya Secondary na Msikiti vinajengwa bure bila mkataba hata wa mwaka 1 kwahiyo manufaa yatapatikana kuliko hata maduka yanavyoingiza.

Mapato ya shule yanakadiriwa kuingiza 600milion kwa mwaka hayo yote yanaingia kwenye mfuko wa Taasisi kwahiyo kuwa na mkataba upande wa maduka ni faida kubwa hata ingekuwa mkataba wa miaka 100 na isitoshe kila mwaka upande wa maduka unaingiza pesa zaidi ya mapato yaliyokuwa yanapatikana awali
Jee huo utaratibu umo katika sheria kuwa mtu akigoma kutoa hati yake unakwenda kutenngeneza nyengine.Na nani anayekupa hiyo nyingine kabla kufutwa ya mwanzo.Ingekuwa ni hivyo majambazi wakitaka nyumba eneo fulani ukigoma kuwapa wanakwenda kutengeneza nyengine halafu unahamishwa.Ikiwa hilo lipo basi kuna kasoro kubwa na sheria ya ardhi lazima ibadilishwe isitoe mwanya kwa utovu wa nidhamu namna hiyo.
Ile ni hati ya Taasisi sio ya mtu binafsi taratibu za kuifuta zilifanyika na maombi ya hati mpya yakafanyika kwisha kazi
 
ninamaswali machache ,tafadhali njoo na majibu Ili tupate mwanga.

1:Mbona kwa mjibu wa Hilo Bango kinacho Jengwa ni Msikiti, na kituo kisicho julikana kitashughulika nanini.
Tajiri hapo Yuko wapi?

2:Mwenye kujenga (kujengewa)ni baraza la wadhamini wa Msikiti.
shida Ipo kwa kinacho Jengwa au wanao simamia ujenzi?

3:Imam wa Msikiti Yuko upande gani anaungana na wajenzi au upande wanao Pinga?
1. Kinachojengwa ni Msikiti,shule na maduka
2. Shida inaletwa na watu wanaohamasisha fujo katika misikiti ambao unakuta wala hawahusiki na lolote katika eneo husika
3. Imam yuko upande wa Wajenzi
 
Ile msikiti ni amali iliyo chini ya jumuiya ya Waislam wa Mwenge. Ninaufahamu. Sasa hili la kuubomoa wakati wenye msikiti hawajaridhia ndo tunarudi kule kule kwenye kudhulumu amali za waislam.

FaizaFoxy angalieni hizi mambo zisije kuleta mtafafuku zaidi
Wenye Msikiti wameridhia na ndio maana RITA wakaridhia, na Manispaa wakatoa kibali hayo mengine ni porojo tu za mitandaoni
 
Bakwata pia wasanii tuu
Bakwata iliundwa na nyerere kudhibiti waislam,baada ya kuivunja taasisi ya afrika mashariki ya waislam,bakwata huko nyuma pamekuwepo viongozi ambao hawakuwa waislam,ndiyo maana Kuna kipindi gari ya bakwata ilibeba bia pakazuka mgogoro
 
Maendeleo ni kwa faida ya uislam na kwa faida ya wanachama wanaomiliki msikiti huo.

Wanachama wote wa chama cha ushirika Mwenge wamekubaliana kufanya maendeleo hayo katika vikao rasmi , hao wapingaji nikujuze tu sio wanachama ndio maana wanaogopa kulipeleka hili jambo kwenye mamlaka zinazohusika

Maduka yanajengwa, Msikiti unajengwa wa ghorofa wenye uwezo wa kuchukua watu kuanzia 700 kuendelea na sehemu ya wazi imetengwa kwaajili ya parking na shughuli za hadhara

Kama usemavyo ndivyo, basi ni jambo la kheli, lakini napata mashaka kwanini ujenzi ,utangulie wa maduka kabla ya Msikiti wenyewe?

Mahitaji hapo ni Msikiti , frem ni kwa maendeleo ya Msikiti, Leo zinatangulizwa frem kabla ya Msikiti hili naro haliko sawa.

Swala lakusema kua walalamikali sio sehemu ya members wa ushirika wa Mwenge Bado linaitaji ufafanuzi.
[/QUOTE]
Ile Taasisi inamilikiwa na members wa Ushirika wa Mwenge wao ndio wenye haki ya kufanya maamuzi katika mali yao kupitia mikutano mikuu kwahiyo Katiba haimpi nafasi mtu ambaye sio member kuhoji kwakuwa yeye sio mmiliki
 
mtoa mada naomba unieleweshe kitu msikiti kuvunjwa, je akijenga maduka anajenga na msikiti mpyaa au anajenga maduka anatoa msikiti kabisa maana kuna jambo ambalo haliwezekani kama kubomoa msikiti hlf ujenge maduka tu ila kina jambo linawezekana kama kubomoa msikiti kujenga msikiti wa kisasa na maduka

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Salaam Wakuu,

Jamani tunaomba msaada, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum atatutoa roho.

Baada ya rais Samia kuingia Madarakani, wale watu wa pesa inaongea Wamerudi kwa kasi ya ajabu. Mtu mwenye pesa sasa anaweza kufanya chochote na usimfanye kitu.

Katika Mkoa wa Dar Es Salaam kuna Taajiri amewaweka mfukoni Watendaji wote wa Wilaya ya Kinondoni hawa Wakina Gondwe.

Kipindi cha nyumba, kuna Tajiri alitaka kununua Msikiti ili ajenge maduka, Bodi ya Wadhamini ya Msikiti Wakamkatalia. Ikabidi Tajiri huyo amtumie Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ambaye alitetengeneza Bodi mpya ya wadhamni wasio hata waumin wa Msikiti ili Waweze kumuuza Tajiri na Wakafanikiwa. Kumbuka Msikiti unamilikiwa na Taasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre. Hakuna aliyeshirikishwa kwenye Uteuzi wa Bodi Mpya.

Waumini Walilalamika RITA, Ardhi na kwa Mkurugenzi wa Kinondoni bila mafanikio.
View attachment 2359556
Wakashangaa Hati ya jengo wanayo wao lakini wakashangaa Msikiti unavunjwa na kuanza kujengwa Maduka. Walipojaribu kuzuia, Wakaitwa Polisi wa Oysterbay wakawakamata wote walioonekana kulalamika na kuwekwa ndani bila dhamana. Walikaa sana Polisi kwa kosa la kifanya fujo Msikitini. Aliyekua Msimamizi Mkuu wa Msikiti akafa kifo cha gafla kwani aliteswa sana na Polisi wakitaka aoneshe hati ya kiwanja ilipo kwani aliwanyima.

Je, Tajiri aliwezaje kununua sehemu na kujenga bila ya kuwa na hati?

Je, Kwanini Bodi ya Wadhamni iliundwa haraka bila kufuata kanuni?

Kwanini Polisi Wawashikile watu na kuwanyima dhamana hadi uzio uwekwe?

RITA WALIFIKA KUKAGUA MALI ZETU LAKINI HADI LEO HAWATUPI MREJESHO
View attachment 2359599
Kwanini RITA pamoja na kuja sehemu ya tukio, mbona hawajasitisha ujenzi?

Je kwanini Mkurugenzi alisimamisha ujenzi, lakini baada ya mhusika mkuu kufariki akaruhusu ujenzi uendelee?

Hawa waumini wanatishiwa kubambikizwa kesi ya Ugaidi.

Hapa chini naweka Ushahidi
View attachment 2359543
Hii hapa ni OB ya Polisi waliokamatwa kisa wanazuia Msikiti wao Usibomolewe. Huruma za Polisi ACP Ramadhan Kingai ndo zilifanywa Waachiliwe baada ya kuhoji sababu ya kuwashikilia bila dhamana wala kupelekwa mahakamani. Ni baada ya kuelezwa kilicho nyuma ya pazia.
View attachment 2359556
Hii ni barua iliyowataka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) na BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) kufika mbele ya Mkuu wa Wilaya ili atatue mzozo huu lakini hawajatokea kila Walipoitwa.
View attachment 2359570
View attachment 2359571
Hii ni kibali cha kusimamisha Ujenzi, wiki mbili baada ya alokuwa anatetea Msikiti usibomolewe kufariki, Wakakihuisha
View attachment 2359582View attachment 2359583View attachment 2359581
Na hiii ni hati halali waliyopewaTaasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre ambayo hadi sasa bado wanayo, ila mtu mwingine kaja kabomoa Msikiti na Kujenga Maduka chini ya Usimamizi wa Polisi. Hawana hata Umiliki.
View attachment 2359584View attachment 2359585
Na huu ni Uthibitisho wa Serikali za Mtaa kutoelewa kunachoendelea mtaani kwake
View attachment 2359588View attachment 2359587
Na haya ndo Maduka yanayojengwa sehemu ulipokuwa Msikiti Mwenge mbele ya Magorofa ya Jeshi barabara ya TRA

Tunaomba Serikali Sikivu ya Mama Samia iingilie Kati swala hili. Bado naamini Godwin Gondwe anao uwezo wa kutatua mgogoro huu japo haoneshi jitihada zozote kuhakikisha hili swala linaisha.

Mkuu wa Mkoa Makalla sababu ni rafiki yake na Sheikh Salum, kila siku anasema yupo busy.
Ni vyema kama unajiridhisha na taarifa yako ofisi za TAKUKURU ziko wazi na Mahakama inatoa haki zipeleke huko kuliko kuwahadaa watu mitandaoni
 
mtoa mada naomba unieleweshe kitu msikiti kuvunjwa, je akijenga maduka anajenga na msikiti mpyaa au anajenga maduka anatoa msikiti kabisa maana kuna jambo ambalo haliwezekani kama kubomoa msikiti hlf ujenge maduka tu ila kina jambo linawezekana kama kubomoa msikiti kujenga msikiti wa kisasa na maduka

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kunajengwa Msikiti mpya wa kisasa, shule ya kisasa na maduka ya kisasa
 
Haya maelzo mimi bado hayajaniingia akiilini ? Yan kuna mtu kanunua msikiti alafu anajenga maduka???? Au kanunua eneo la nje ya msikiti anajenga maduka.?? Sipati picha ni vitu bado aviiniingii akiilinii.mtu from no where aje auze msikiti unaotumiwa na watu alafu ajenge maduka.
 
apo sioni shida yoyote ile labda kama kuna watu wamenyimwa ulaji

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hiyo ndio sababu kuna watu wanaangalia maslahi binafsi kuliko ya Taasisi hao ndio wenye shida kwakuwa hawajapewa hela ndio wanazusha zogo mitandaoni wakati kama kuna kitu kimekiukwa mamlaka husika ziko wazi muda wote kwanini hawaendi kureport?
 
Haya maelzo mimi bado hayajaniingia akiilini ? Yan kuna mtu kanunua msikiti alafu anajenga maduka???? Au kanunua eneo la nje ya msikiti anajenga maduka.?? Sipati picha ni vitu bado aviiniingii akiilinii.mtu from no where aje auze msikiti unaotumiwa na watu alafu ajenge maduka.
Hawa watu sio wakweli wanajaribu kuwachafua watu maana Misikiti yote inasimamiwa na RITA na vibali vya uwekezaji kwenye maeneo ya misikiti vinatolewa na RITA kwahiyo hawawezi kufuta Msikiti halafu yajengwe maduka wanapotosha jamii waziwazi ila wenye akili wameshawajua dhamira yao
 
Wenye Msikiti wameridhia na ndio maana RITA wakaridhia, na Manispaa wakatoa kibali hayo mengine ni porojo tu za mitandaoni
Unapoona watu wazima wanalalamika hadi kupitia mitandao uache akili za kindezi, shuka pale ulizia kwa nini wanalalamika.
Wewe unaonekana wazi kabisa ni sehemu ya matatizo kila unapoenda
 
Unapoona watu wazima wanalalamika hadi kupitia mitandao uache akili za kindezi, shuka pale ulizia kwa nini wanalalamika.
Wewe unaonekana wazi kabisa ni sehemu ya matatizo kila unapoenda
Wazima kiumri au kiakili? Unaweza ukawa mtu mzima kiumri lakini ukawa mwehu hakuna mtu atakayepoteza muda wake kukusikiliza mtu mwehu
 
Back
Top Bottom