TAKUKURU yafanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya viongozi na watumishi

TAKUKURU yafanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya viongozi na watumishi

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya viongozi na watumishi wa taasisi hiyo.

Mabadiliko hayo yamehusisha watumishi 6 wa TAKUKURU, watano kati yao wakitokea kwatika vituo vya kazi jijini Arusha.

====

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupapambana na Rushwa, TAKUKURU amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa watumishi sita, watano kati yao wakiwa wa vituo vya Mkoa wa Arusha. Uhamisho huu ni wa kawaida kuimarisha utendaji


Watumishi waliohamishwa ni pamoja na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Frida Wikesi, amehamishiwa makao makuu. James Ruge, Afisa Uchunguzi Mkuu aliyekuwa Makao Makuu amehamishiwa kituo cha Kaimu Mkuu Arusha

Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Arumeru, Zawadi Ngailo, amehamishiwa Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Arusha. Degratias Peter, Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Siha amehamishiwa ofisi ya Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Arumeru

Aidha, Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Monduli, David Shirima amehamishiwa ofisi ya Mkuu TAKUKURU Wilaya ya Siha. Afisa Uchunguzi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mariam Mayaya amehamishiwa ofisi ya Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Monduli
photo_2020-06-27_14-20-15.jpg
photo_2020-06-27_14-20-20.jpg
 
Naona haya ni baada ya onyo la mkuu wa nchi.
Watu wanakaa tu mpaka wakemewe na kuonywa ndo wanachukua hatua.

Ona sasa, walikuwa wanamtumikia Ghambo, sasa yamekwakuta.
 
Yani mpaka Rais aibue ndo wachukue hatua serious kweli? Ivi ofisi ya DG takukururu si ina resources zote za kufatilia kujua kama watendaji wake wana fit izo positions kuna mambo yanashangaza sana sasa mpaka Inteligency ya mkuu ndio iibue madudu ile hali watu wanalipwa maofisini Huyu jamaa kwa vile ni Mjeda tu ila hatoshi apo
 
Tabia ni tabia tu hata huko wakizoea wataendelea na tabia zao mbofu mbofu.
 
Back
Top Bottom