TAKUKURU yamkamata mtumishi wake Zainabu Mohamed Jabir kwa kuomba rushwa ya Tsh milioni 50

TAKUKURU yamkamata mtumishi wake Zainabu Mohamed Jabir kwa kuomba rushwa ya Tsh milioni 50

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Unaweza kudhania ni hadithi, lakini ndio ukweli wa mambo.

-
AFISA WA TAKUKURU AKAMATWA KWA KUOMBA RUSHWA YA SHILINGI MILIONI 50

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo, napenda kuufahamisha umma kwamba, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imekuwa ikiendelea na utekelezaji wa majukumu yake ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini, kama yalivyotamkwa na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Kupitia majukumu haya, tumekuwa tukiuhabarisha umma juu ya mafanikio mbalimbali yanayotokana na utekelezaji wa majukumu haya ikiwa ni pamoja na kuwahabarisha juu ya watumishi wa umma wanaokamatwa kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.

Kama mtakavyokumbuka, wiki iliyopita kupitia ofisi yetu ya TAKUKURU mkoa wa Arusha tumewakamata Askari Polisi 7 waliodaiwa kudai rushwa ya Shilingi Milioni 200 kutoka kwa Mfanyabiashara mmoja wa jijini Arusha na kupokea shilingi milioni 100, lakini pia kupitia ofisi yetu ya TAKUKURU mkoa wa Manyara, tulimkamata Mwendesha Mashitaka wa Mkoa wa Manyara kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya Shilingi Milioni 5 kutoka kwa watuhumiwa wa makosa ya Jinai.

Ndugu waandishi wa Habari,
Kupitia taarifa hii ya leo, tunaujulisha umma kuwa tumemkamata Mtumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU aitwaye ZAINAB MOHAMED JABIR, kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa – Kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Mtumishi huyu aliomba rushwa kiasi cha shilingi Milioni 50 kutoka kwa mtu mmoja (Jina limehifadhiwa) kwa madai ya kumsaidia mtu huyo katika tuhuma dhidi yake ambazo zinachunguzwa na TAKUKURU. Uchunguzi dhidi ya tuhuma hii unaendelea na utakapokamilika hatua stahiki zitachukuliwa.

Ndugu Waandishi wa Habari,
Vilevile, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, napenda kuzungumzia kuhusu uwepo wa tabia ya baadhi ya watu wanaofanya UTAPELI kwa kujitambulisha kwa vyeo tofauti tofauti ikiwemo Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU.

Matapeli hawa wamekuwa wakipiga simu na kujitambulisha kuwa wao ni Maafisa wa TAKUKURU wakiwaeleza watu hao kwamba tuhuma zao zipo TAKUKURU na kwamba wanawaita TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano.

TAKUKURU inawapongeza wale wote walioweza kubaini kuwa watu hawa ni MATAPELI na kutoa taarifa TAKUKURU mara moja. Hata hivyo, tunaendelea kusisitiza wananchi kutokubali kutapeliwa na mtu yeyote. Unapopokea simu ya aina hii tafadhali fika katika ofisi ya TAKUKURU iliyoko karibu nawe kwani TAKUKURU ina ofisi katika mikoa yote na Wilaya zote Tanzania Bara.

Ndugu Waandishi wa Habari,
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, tunaendelea kuwashukuru wananchi na wadau wengine wote ambao wamekuwa wakishirikiana nasi katika kufanikisha jukumu hili la kuzuia na kupambana na rushwa nchini kwa kutuletea taarifa za wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.


IMETOLEWA NA:

DOREEN J. KAPWANI
AFISA UHUSIANO
KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
 
Duh huyo mwanamke ni jasiri sana,angekua maeneo kama Tanga sidhani kama angekamatwa. Huku ukimpeleka mtu Takukuru utashangaa anakueleza yote uliyoyasema huko.

Mh. Rais wazingue Takukuru Tanga ingawaje bosi wao alisimamishwa lakini mapandikizi yake yapo kibao. Ngoja niishie hapo maana naelekea kutaja majina ya wale vijana pale tena wote me na ke
 
Basi kama ndio hivyo, Takukuru ya Tanga ndio kuna mimalkia na mibalkia kibao.
Wanafanya kinyume cha kudhibiti yaani wanaendekeza au kuibariki rushwa. Wananunulika na ukifika wanakuambia hii kesi achana nayo
Mkuu una uhakika?
 
Unaweza kudhania ni hadithi, lakini ndio ukweli wa mambo.

-
TAKUKURU imemkatama mfanyakazi wake, Zainabu Mohamed Jabir kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya TSh.50 milioni kutoka kwa mtu mmoja ili kumsaidia katika tuhuma dhidi yake zinazochunguzwa na taasisi hiyo.
Safi Sana,hastahil
 
Utakuta ana kadi ya CCm huyu
Unaweza kudhania ni hadithi, lakini ndio ukweli wa mambo.

-
TAKUKURU imemkatama mfanyakazi wake, Zainabu Mohamed Jabir kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya TSh.50 milioni kutoka kwa mtu mmoja ili kumsaidia katika tuhuma dhidi yake zinazochunguzwa na taasisi hiyo.
 
Hawa ndio wanafanya mwenendo wa kesi nyingi kuwa haieleweki.
 
Kweli akili za umasikini ndio hizo hata aishi maisha mazuri na mshahara mzuri ila kwa kuwa unaanza na maadili mabaya nyumbani na mpaka umaenda shule kwa kuanza kuiba penseli haya ndio matokeo

Mwizi habadiliki hata umpe nini na hii tabia ni % kubwa sana wanayo
 
Back
Top Bottom