Elections 2010 TAKUKURU yamtia nyavuni Felix Mrema - Arusha mjini

Elections 2010 TAKUKURU yamtia nyavuni Felix Mrema - Arusha mjini

Nchi inakwenda kwa alijojo, msukule wa magogoni unaona unataka kukatwa hivyo umeanza chokochoko. Muda upo tutaona kama huu msukule kweli unaweza kuwababaisha walipa kodi hadi hivi sasa msukule 2 Walipa kodi 0.
 
Chaguzi zote zilikuwa hivo hivo, hawa ni danganya toto. TAKUKURU nitaiamini kama watakuwa wame mhoji Rukuvi make ndiye alikuwa wa kwanza kugawa pikipiki, Rostam, Karamagi. May be hawa ni wana mtandao?


Namecalling tafadhali anaitwa Lukuvi! :focus:
 
PCCB endeleeni :fish2: wote hadi waishe tunataka uchaguzi safi mwaka huu

Ndugu yangu suijidanganye. PCCB wanamaliza na CCM baada ya kura za maoni then wanahamia kwa wapinzani kuelekea October. Tutalia na kusaga meno, maana mkakati ni kwamba baada ya kura za maoni hakuna mwana CCM atakayeguswa tena kazi itahamia kuwakomoa wapinzani. Ukikutwa bar unakunywa soda na wapambe wako big deal hasa kama utakuwa tishio kwa CCM.
 
Mambo ya CCM kutumia fedha kwa kujipatia uongozi yanaendelea kujidhihirisha. Kwa sasa PCCB ina mshikilia Mh.Mrema na mabalozi kadhaa kwa tuhuma za rushwa.....nitawaletea habari kamili baadaye kwani mpaka sasa bado wanahojiwa.
Wanabodi, nikiwa ni miongoni mwa tuliotoa tongo tongo kidogo kwenye fani ya sheria, hawa PCCB wanacheza makida makida tuu, hizo evidence wanaojidai dai kuzikamata kama viashiria vya rushwa ni very weak avidence. Kezi zote watakazozifikisha mahakamani, nadhani zitafuta siku hiyo hiyo ya kuandikishwa, na kwa kuanzia, sidhani kama DPP atatoa kibali zifunguliwe, hakuna kesi zozote hapo, ni kuchafuliana majina tuu na hii ndio picha ya ukweli jinsi CCM mzima ilivyo, na ambao hawajashikwa, msijipe matumaini kuwa wao ndio wasafi, ni wachafu tuu, tena wengine wachafu zaidi,

Cha muhimu ni kwa wananchi kuhamasishwa na kuelimishwa ili wasiendelee kulea uchafu huu kwa gharama ya T-shirt na kofia na shibe ya siku moja, Octoba 31 waseme no kwa uchafu huu na wachague usafi!.
 
Kezi zote watakazozifikisha mahakamani, nadhani zitafuta siku hiyo hiyo ya kuandikishwa, na kwa kuanzia, sidhani kama DPP atatoa kibali zifunguliwe, hakuna kesi zozote hapo, ni kuchafuliana majina tuu na hii ndio picha ya ukweli jinsi CCM mzima ilivyo, na ambao hawajashikwa, msijipe matumaini kuwa wao ndio wasafi, ni wachafu tuu, tena wengine wachafu zaidi,
Halafu washtakiwa watafungua kesi za madai na serikali itaingia bonge la hasara....?
 
Kwa kweli nimeanza kuhisi kuwa TAKUKURU wanafanya kazi ya wanamtandao ili kuhakikisha kuwa the likes of Mwakembe, Sita, selelii nk hawarudi Bungeni. Mbona inasemekana huyu Batilda anatembeza mlungula huku "A" town kama hana akili nzuri, PCCB wako wapi wamkamate?. Halafu naona pia kuna harakati za makusudi za kumrudisha papa wa ufisadi (Richman from Monduli - Lowasa) kwenye kabinet ya JK. Wote walio kinyume chake wanapnekana kushulikiwa ktk mchakato wa kura za maoni ndani ya chama cha mafisadi!
 
Tunatawaliwa KIJESHI
tunatawaliwa na WAKOLONI WEUSI
tunatawaliwa na WANAFIKI, WAONGO NA WAZUSHI

hii ndiyo CCM niijuayo. hakuna usafi zaidi ya UMANGIMEZA
 
Malaria sijui yuko wapi leo aje atoe mchango wake tuusikie kuhusu waccm wanavyokamatwa na takukuru

Malaria Sugu yuko Nzega, kumkampenia Bashe (msomali) ili kuhakikisha anamg'oa Selelii. Lengo lao kuu ni kuwa ng'oa wale wapiganaji dhidi ya Ufisadi. Kuwa makini Jemedari Mwakyembe + Mama Anne Kilango + James Lembeli, Takakuru no Takukuru are following you, kisa mko against ufisadi (RA + JK + EL + Hosea).

Hongereni sana wana-mtandao, najua mtaweza kuwang'oa wote ila iko siku nguvu ya UMMA itawaondoa nanyi pamoja na JK wenu.
 
Haya habari nyingine ndiyo hizo.. Inadaiwa mbunge wa Arusha Mjini Felix Mrema naye amekamatwa tangu jana usiku na TAKUKURU kwa kudaiwa kuhusika na vitendo vya rushwa (japo kama kawaida hajakamatwa akitoa) yaani amekutwa na "paraphenalia ya rushwa" vitu kama:

bahasha zenye fedha
kadi feki za CCM
shahada za kura n.k

Daily News

AS more CCM aspirants for the race to parliament have fallen on the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) trap, the party has said it was highly impressed, so far, by efforts in fighting the vice in the ongoing election campaigns.

CCM Secretary General Yussuf Makamba said in Dar es Salaam on Thursday that the party would be surprised if PCCB would not detain any of their members in this campaigning season.

Mr Makamba said this in reaction to a number of incidents whereby senior government officials and seasoned politicians were nabbed on suspicion of bribing party members to win votes.

Meanwhile, PCCB has said that the anti-corruption crusade in the campaigns targets no one.

In an exclusive interview with the ‘Daily News' in Dar es Salaam on Thursday, PCCB Director General, Dr Edward Hosea, said politicians who have been nabbed should keep quiet as there was incriminating evidence on the allegations.

"Can these people have the nerve to claim that such evidence was fabricated against them? They are just looking for excuse, but the reality is that one should not give or take bribe," he said.

Meanwhile, MARC NKWAME from Arusha reports that the incumbent Member of Parliament (MP) for Arusha Urban Mr Felix Christopher Mrema, was nabbed by the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) on Wednesday night allegedly for bribing party members.

The head of PCCB in Arusha region, Mr Akida Ayoub, confirmed here that Mr Mrema was arrested along 21 other CCM members in a residential house at Olamuriaki area at Sombetini about an hour before midnight.

The suspects were interviewed for seven hours and released on bail at about 6.00am on Thursday. The MP has since resumed his party nomination campaigns but his phone remained off-air all day.

"PCCB earlier on got a tip-off about suspicious meeting of party members that night and when officers went round the suspected house they came across a meeting which confirmed an unusual set-up," said Mr Ayoub.

The ‘suspicious environment' which PCCB claimed to have found include the meeting of 22 people in a house late at night, seven ten-cell leaders at the same venue and three envelopes con¬taining 115,000/- equally in each of them.

"We also found 25 CCM membership cards inside a bag which was in the person of the area party secretary, Ms Shamsi Cyril Mwacha, who was among the people gathered in the house¬hold," said Mr Ayoub, adding that there were some other suspects outside the building but escaped after seeing strangers arriving.

Some of the CCM cards bore neither holders' names nor photos even though they were signed and stamped. The MP, however, was found with nothing.

The ten-cell leaders arrested along the MP were; Paul Mollel, Jacob Mweta, Boniface Mweu, Cyprian Mwamba, Abdallah Gege, Mama Sara, and Shamsi Mwacha, who is the party secretary for Kirika CCM branch and who was allegedly found with the said envelopes as well as the CCM cards.

Others who got nabbed by the PCCB are Bakari Issa, Abdalla Juma Omar, Shaibu Hassan Waziri, Asha Juma, Monica Michael Nzota, Kolumba Hassan Mariri, Julius Yohana Laizer, Alex Kisioki, Waziri Kibuno, Dickson Miambi, Elias Kileo, Peter Ongiri and Fatuma Mohammed Al.
 
Wanashindwa nini kuwaacha hawa wanaowakisia kuwa wana lengo la kutoa rushwa kwa kuwafanyia timing na kuwajulisha police ili wakamatwe wakiwa wanatoa rushwa hizo??!
 
Wanashindwa nini kuwaacha hawa wanaowakisia kuwa wana lengo la kutoa rushwa kwa kuwafanyia timing na kuwajulisha police ili wakamatwe wakiwa wanatoa rushwa hizo??!

hilo siyo lengo lao, lengo ni kutoa onyo tu.. vinginevyo wakiwakamata officially wataharibu upigaji kura j'pili. Ndiyo maana hadi hivi sasah akuna anayepelekwa mahakamani. Maagizo ni kutumia "preventive measures" kuwaambia tu kuwa wanajua kinachoendelea.
 
Wanashindwa nini kuwaacha hawa wanaowakisia kuwa wana lengo la kutoa rushwa kwa kuwafanyia timing na kuwajulisha police ili wakamatwe wakiwa wanatoa rushwa hizo??!

Kuna sababu mbili, moja serikali ipate kuonekana inadhamiria kweli kulishughulikia swala la rushwa, pili kwa kuwa wote wanafanya hivyo, kuhakikisha hakuna ushahidi wa kutosha kumtia mwenzao katika matata ya kisheria...yote danganya wadanganyika!

Lakini walau tumeshuhudia kwamba ni kweli kunakuwepo na rushwa, sasa wao kwa wao, je itakapokuja nusu fainali? Labda pengine si shida kubwa kwao wakati huu maana wapinzani sidhani watakuwa na hela ya kushindana na hawa wezi wazoefu
 
Ndugu yangu hii habari iko kwenye Hoja /hABARI MCHANGANYIKO CHUNGULIA KULE UTAONA
 
hilo siyo lengo lao, lengo ni kutoa onyo tu.. vinginevyo wakiwakamata officially wataharibu upigaji kura j'pili. Ndiyo maana hadi hivi sasah akuna anayepelekwa mahakamani. Maagizo ni kutumia "preventive measures" kuwaambia tu kuwa wanajua kinachoendelea.

Hii taasisi inaleta maudhi kwelikweli... kama Kirongaya alivyosema, kwenye thread ya kukamatwa mama Sitta; ni bora sasa TAKUKURU waanze tu kutoa kadi za chama chao cha kisiasa watu tujiunge!! What a bogus instrument is turning out to be!!
 
Hawa bana wanatuzuga tu wanataka tufikiri CCM inafanya kweli waongo bana.. mtachomana sana mwaka huu lakini wembe umepatikana
Hakuna cha TAKURURU wala TAKA LALA hapa CCM msituchanganye akili zetu eti tuwaone leo mnafanya kweli. Hii inaitwa danganya toto nyie
chomaneni kutakapokuwa kunakucha mtaona mmebakiza vitanda vya kulala lakini nyumba kwishney..
 
Mie ningependa kujua ukikamatwa unataka/unatoa rushwa unazuiwa kugombea ama ndio basi tu unahojiwa alafu unaachiwa uendelee na kampeini?
 
Ni ajabu na kweli!
Hii kamata kamata ina mashiko yoyote kwenye vita dhidi ya rushwa?
Kama hadi sasa tumesikia majina mkubwa katika chama tawala - kuanzia DC, waziri hadi Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya sheria wakikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na vitendo vya rushwa, mbona ni ishara mbaya sana! Inaonyesha aina ya viongozi tutakaokuwa nao.Mungu apishilie mbali!
 
Yaani kwa Tshs 115,000 tu wajumbe wanauza kura zao na kumpigia kura za maoni Mbunge fisadi..!!!

Kumbe Tanzania kununua uongozi ni bei ndogo hivyo?
 
Back
Top Bottom