Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Iringa, imetangaza msimamo mkali dhidi ya wagombea wa nafasi za kisiasa wanaojihusisha na utoaji wa ahadi za uongo wakati wa kampeni, wakisema kwamba tabia hiyo si tu ya kupotosha umma, bali ni aina ya rushwa ya kisiasa inayodhoofisha misingi ya demokrasia na uwajibikaji.
Soma > Je, Ahadi za Uongo Wakati wa Kampeni za uchaguzi Zina Adhabu Kisheria?
Kwa mujibu wa TAKUKURU Iringa, wagombea wote wa nafasi za ubunge na udiwani wanatakiwa kuzingatia kikamilifu ahadi zilizoainishwa kwenye ilani rasmi za vyama vyao, na si kutumia maneno matamu au matarajio yasiyotekelezeka kama chombo cha kushawishi wapiga kura.
Je, unakubaliana na msimamo wa TAKUKURU kwamba kutoa ahadi za uongo wakati wa kampeni ni aina ya rushwa ya kisiasa?