Uchaguzi 2020 TAKUKURU yapiga marufuku wapiga kura kwenda kula pilau kwa washindi wa Uchaguzi, yasema ni kupokea rushwa ya chakula

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita, Leonidas Felix, amepiga marufuku wapigakura kwenda kula pilau kwa watakaoshinda katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Felix alitoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana, na kusema wapigakura kula kwa kiongozi aliyeshinda ni kupokea rushwa ya vyakula, ambayo itawafanya wakose nguvu za kuwahoji shughuli za kuwapelekea maendeleo.

Aidha, alisema kula chakula kwa wagombea waliyoshinda ni kumalizana mkataba kati ya mgombea na mpigakura. Kwa sababu kufanya hivyo kiongozi aliyeshinda hawezi kujishughulisha kuwapelekea maendeleo kwa sababu wamemalizana kwenye pilau.

Felix alisema kwa sasa wapigakura waamishe akili zao za kuwaza kula pilau badala yake wahudhurie kwenye mikutano ili kusikiliza ilani za wagombea waweze kufanya uchaguzi sahihi ifikapo Oktoba 28, mwaka huu.

Aidha, aliwataka wapigakura kutunza vitambulisho vyao vya kupigia kura na wasiruhusu watu wasio wema kuvinunua na watakaobaini wakifanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Alisema wapiga kura watambue dhama ya kura yao ni haki anayohitaji, utulivu anaohitaji, amani anayohitaji na maendeleo anayohitaji katika maeneo yao wanayoishi.

Aidha, aliwataka wapigakura pindi waonapo wagombea na wapambe wao wanaofika majumbani mwao kwa kuwapatia zawadi mbalimbali watoe taarifa katika ofisi za TAKUKURU zilizopo karibu nao.

Chanzo: IPP Media
 
Mngedili na swala uchaguzi haki na salama,hayo ya ubwabwa tukivuka mto tutadili nayo mbeleni
 
Ndizi Za Kula Pilau Nimenunua Mwenyewe Unanizuiaje?!!

Ndani Ya CCM yetu si kosa kufanyiana takrima ya vitu...rejea kauli ya mh.Jakaya Kikwete kipindi kileee PCCB ikiwa chini ya Mzee Edward Hosea....
 
Awamu hii ya tano TAKUKURU imejikita zaidi kwenye rushwa ya chakula . Nia yao siyo njema hata kidogo pesa mtaani za rushwa hakuna mnaingia kwenye ubwabwa na pilau ilimradi tukondeane tukose raha tufe 😂😂😂
 
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita, Leonidas Felix, amepiga marufuku wapigakura kwenda kula pilau kwa watakaoshinda katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Felix alitoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana, na kusema wapigakura kula kwa kiongozi aliyeshinda ni kupokea rushwa ya vyakula, ambayo itawafanya wakose nguvu za kuwahoji shughuli za kuwapelekea maendeleo.

Aidha, alisema kula chakula kwa wagombea waliyoshinda ni kumalizana mkataba kati ya mgombea na mpigakura. Kwa sababu kufanya hivyo kiongozi aliyeshinda hawezi kujishughulisha kuwapelekea maendeleo kwa sababu wamemalizana kwenye pilau.

Felix alisema kwa sasa wapigakura waamishe akili zao za kuwaza kula pilau badala yake wahudhurie kwenye mikutano ili kusikiliza ilani za wagombea waweze kufanya uchaguzi sahihi ifikapo Oktoba 28, mwaka huu.

Aidha, aliwataka wapigakura kutunza vitambulisho vyao vya kupigia kura na wasiruhusu watu wasio wema kuvinunua na watakaobaini wakifanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Alisema wapiga kura watambue dhama ya kura yao ni haki anayohitaji, utulivu anaohitaji, amani anayohitaji na maendeleo anayohitaji katika maeneo yao wanayoishi.

Aidha, aliwataka wapigakura pindi waonapo wagombea na wapambe wao wanaofika majumbani mwao kwa kuwapatia zawadi mbalimbali watoe taarifa katika ofisi za TAKUKURU zilizopo karibu nao.

Chanzo: IPP Media
Yaani mwiko ni pilau tu. Ugali, laga, au ngawira ni ok? Takukukukurukukuru kakara!

Sent from my XT1097 using JamiiForums mobile app
 
Tutaenda kula nyama choma na bia kuna shida hapo ?
 
"Sisi wana ccm tulianza kula pilau wakati tunaitwa kwenye mikutano"
Wanasema walijua hawatashinda hivyo bora wale mapema
IMG_20200701_203659.jpg
IMG_20201011_074035.jpg
 
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita, Leonidas Felix, amepiga marufuku wapigakura kwenda kula pilau kwa watakaoshinda katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Felix alitoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana, na kusema wapigakura kula kwa kiongozi aliyeshinda ni kupokea rushwa ya vyakula, ambayo itawafanya wakose nguvu za kuwahoji shughuli za kuwapelekea maendeleo.

Aidha, alisema kula chakula kwa wagombea waliyoshinda ni kumalizana mkataba kati ya mgombea na mpigakura. Kwa sababu kufanya hivyo kiongozi aliyeshinda hawezi kujishughulisha kuwapelekea maendeleo kwa sababu wamemalizana kwenye pilau.

Felix alisema kwa sasa wapigakura waamishe akili zao za kuwaza kula pilau badala yake wahudhurie kwenye mikutano ili kusikiliza ilani za wagombea waweze kufanya uchaguzi sahihi ifikapo Oktoba 28, mwaka huu.

Aidha, aliwataka wapigakura kutunza vitambulisho vyao vya kupigia kura na wasiruhusu watu wasio wema kuvinunua na watakaobaini wakifanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Alisema wapiga kura watambue dhama ya kura yao ni haki anayohitaji, utulivu anaohitaji, amani anayohitaji na maendeleo anayohitaji katika maeneo yao wanayoishi.

Aidha, aliwataka wapigakura pindi waonapo wagombea na wapambe wao wanaofika majumbani mwao kwa kuwapatia zawadi mbalimbali watoe taarifa katika ofisi za TAKUKURU zilizopo karibu nao.

Chanzo: IPP Media
Vipi hawajaongelea kuhusu kucheza one love ikulu?
 
Back
Top Bottom