beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita, Leonidas Felix, amepiga marufuku wapigakura kwenda kula pilau kwa watakaoshinda katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Felix alitoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana, na kusema wapigakura kula kwa kiongozi aliyeshinda ni kupokea rushwa ya vyakula, ambayo itawafanya wakose nguvu za kuwahoji shughuli za kuwapelekea maendeleo.
Aidha, alisema kula chakula kwa wagombea waliyoshinda ni kumalizana mkataba kati ya mgombea na mpigakura. Kwa sababu kufanya hivyo kiongozi aliyeshinda hawezi kujishughulisha kuwapelekea maendeleo kwa sababu wamemalizana kwenye pilau.
Felix alisema kwa sasa wapigakura waamishe akili zao za kuwaza kula pilau badala yake wahudhurie kwenye mikutano ili kusikiliza ilani za wagombea waweze kufanya uchaguzi sahihi ifikapo Oktoba 28, mwaka huu.
Aidha, aliwataka wapigakura kutunza vitambulisho vyao vya kupigia kura na wasiruhusu watu wasio wema kuvinunua na watakaobaini wakifanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema wapiga kura watambue dhama ya kura yao ni haki anayohitaji, utulivu anaohitaji, amani anayohitaji na maendeleo anayohitaji katika maeneo yao wanayoishi.
Aidha, aliwataka wapigakura pindi waonapo wagombea na wapambe wao wanaofika majumbani mwao kwa kuwapatia zawadi mbalimbali watoe taarifa katika ofisi za TAKUKURU zilizopo karibu nao.
Chanzo: IPP Media