TAKUKURU yautambua mchango mkubwa wa JamiiForums katika kuendeleza mapambano dhidi ya Rushwa nchini

Serikali imechelewa sana kutambua umuhimu wa mitandao kuibua madudu ya watendaji nchini.
Steriotype thinking ya waajiriwa na wanasiasa nchini kufikiri mitandao ni ya kuipinga serikali sasa inabidi ibadilike.
pongezi kwa TAKUKURU kwa kutambua umuhimu wa jinsi ya kupata tetesi za uhujumu au rushwa nchini.

Big up General Mbung’o na TAKUKURU.
 
Mkuu, nadhani haufuatilii. Hakuna kesi ambayo Takukuru wameishitaki Taasisi ya Jamii Forums, Mfanyakazi wake wala Mwanachama wa JamiiForums.

Hao Takukuru wanafanya usanii tu hapo hamna kitu. Wagombea wa ccm zaidi ya nusu walitoa rushwa wazi wazi na habari nyingi ziliwekwa humu jukwaani lakini hakuna lolote walifanya. Hizi ni baadhi ya taasisi zinazokula hela za walipa kodi bila tija yoyote. Hizi porojo zao wawape watu wasiokuwa na ufahamu wowote.
 
Kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Hawa watu hawaaminiki kabisa , sipokei pongezi zao , Mara watupongeze mara nyuma ya pazia wanatuwinda , tushike lipi ?
Mimi nitaanza kuwaamini siku wakimkamata au kumkemea Magufuli kwa kutoa na kuhamasisha Rushwa wazi wazi tena mchana kweupe.
 
Atua kubwa Sana kwa JF hakina Mungu ni mwema
 
Vipi kuhusu ile kadhia ya Maxence Melo?. Wanauchukuliaje uonevu ule? Kwani hukumu yake ilitokana na matumizi mabaya ya madaraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…