Kwani TAKUKURU wamemaliza jukumu lao la kupambana na Rushwa? hadi kuhamia kwenye jukumu la kumasisha watu kupiga kura
-------------
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 wa kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imewahamasisha watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaoweza kutetea maslahi na maendeleo yao
Akizungumza wakati akifungua mafunzo ya utoaji elimu dhidi ya rushwa kwa viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu na mahitaji maalum mkoani humo, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, Bw. Christopher Mwakajinga, amesema ushiriki wa kundi hilo katika uchaguzi si hisani bali ni haki yao ya msingi inayotokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
“Ushiriki wa watu wenye mahitaji maalum kwenye uchaguzi ni haki ya kikatiba, si fadhila. Ni lazima tuweke mazingira huru na sawa ili waweze kuitumia haki yao ya kupiga kura,” amesema Mwakajinga
Chanzo: Zanzibar_mpya