TAKUKURU yawaonya matapeli wanaojifanya maofisa wake

TAKUKURU yawaonya matapeli wanaojifanya maofisa wake

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Kagera inawachunguza matapeli wanaojifanya ni maofisa wa taasisi hiyo kwa kuwapigia simu za vitisho wananchi kisha kuwaomba fedha.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa Takukuru mkoa, John Joseph alipotoa taarifa ya utendaji ya miezi mitatu hiyo.

“Kuna taarifa tumezipata ila bado tunazifanyia uchunguzi kuwa kuna matapeli wamekuwa wakijifanya ni maofisa wa Takukuru ambao wanawarubuni wananchi kwa kuwapigia simu na kuwatishia kisha kuwaomba fedha," amesema Joseph.

Mkuu huyo ametoa rai kwa yeyote anayefanya utapeli huo ndani ya Mkoa wa Kagera kuacha tabia hiyo mara moja na kwamba wote wanaofanya hivyo watasakwa kwa nguvu zote na watakaobainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ili liwe fundisho na kwa wengine wanaofikiria jambo kama hilo.

Wakati huohuo, amesema kwa miezi mitatu iliyopita wamepokea malalamiko 182 yakiwamo 102 yalihitaji ushauri, manne yaliyohamishiwa idara nyingine ambayo hayakuhusu masuala ya rushwa, na saba ya makosa ya uadilifu ambapo waajiri wa watuhumiwa walishauriwa kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za watumishi wa umma na ajira.

Aidha, amesema wamechunguza mashauri 36 na kufungua kesi nane zenye watuhumiwa tisa ambao watano kati yao wanatoka Wilaya ya Bukoba huku Karagwe, Biharamlo na Kyerwa zikiwa na mtuhumiwa mmojammoja na taarifa 33 zinaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Amesema mashauri 13 yamehukumiwa mahakamani, mashauri manane watuhumiwa wametiwa hatiani, mashauri matano watuhumiwa wameachiwa huru na Takukuru haikuridhika hivyo inajipanga kukata rufaa huku mashauri 49 yakiendelea kusikilizwa mahakamani.

Mwananchi
 
Huyu Joseph nae alitajwa kwenye list ya wavutaji naona uongozi umembeba Hamduni fanyia kazi maoni ya wananzengo
 
Back
Top Bottom