Takwimu kuhusu utalii Tanzania

Musia

Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
95
Reaction score
19
Wadau wa JF,
Naomba kuuliza je ninapotaka kufahamu kuhusu takwimu mbalimbali za utalii Tanzania nitazipataje? Hivi sasa nipo nje ya nchi kimasomo na takwimu hizo ni kwa ajili ya research. Hapa nataka kufananisha kati ya mikoa iliyoendelea kiutalii na ile ambayo iko nyuma (mfano Arusha na Mbeya) na tofauti inaletwa na nini. Kama kuna mtu/watu wenye ufahamu na hili naomba msaada wao tafadhali
 
kwakuwa unafanya research nakuomba ufuatilie ni vivutio gani vilivyoko mikoa iliyoendelea then ufuatilie kama mikoa isiyoendelea haina au la,japo vivutio vilivyoko arusha si necessarily viipsishe pia mbeya kiutalii.mbeya inaweza ikibuka bila serengeti national park,mlima kilimanjaro n.k.by the way,do u want to assess tourism development in,say,in mbeya and arusha or,say,assess tourism statistics between mikoa iliyoendelea na isiyoendelea?.....
 
Tembelea websites za Tanapa na TTB nadhani wanaweka hizo statistics!
 
utalii ume endelea sana Kaskazini kuliko southern circuit, kuna pande 4 za utalii ndani ya tanzania TTB wame ugawa utalii, pande ya western, eastern, southern and northern
 
Kimsingi nataka kufananisha Mbeya na Arusha kwa sababu nimeishi katika mikoa yote miwili. Najua kuhusu utajili wa vivutio vya utalii kwa upande wa Arusha kama mbuga za wanyama, utamaduni hasa wa Kimasai, Olduvai n.k. lakini Mbeya japo huwezi kuifananisha na Arusha binafsi kwa mtazamo wangu naona kuna uwezekano wa kutumia vivutio vilivyopo kuuendeleza utalii. Kwa mfano kuna Matema beach kule Kyela, Kimondo(meteorite), bonde la ufa, Lake Ngosi (juu ya mlima), kuna maporomoko n.k. Tatizo ni kwamba maneno ya mdomoni tu huwa hayana uzito kwenye research wataalam wanataka ushahidi wa takwimu za kuaminika.
Kuna wakati nitarudi huko kufuatilia lakini kwa sasa nahitaji kuandaa proposal kwanza kwa hiyo takwimu ninazoweza kuzipata online ndiyo zina msaada zaidi kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…