LGE2024 Takwimu za uandikishaji uchaguzi wa serikali za mitaa huenda zimepikwa kupitiliza!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Serikali leo imetangaza kuwa zaidi ya nusu ya watanzania wamejiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024. Takwimu zilizotolewa na waziri siku ya leo zimesema zaidi ya watanzania milioni 31 wameandikishwa! Takwimu hizi zinamaanisha, karibu kila mtanzania aliyetakiwa kujiandikisha ili kushirikishi uchaguzi huu ameandikishwa!

Bila kupepesa macho na kumumunya maneno huu ni uongo wa wazi kwa 100%, na hapa nitafafanua na mbinu zilizotumika kutengeneza takwimu hizo za uongo.

1. Uchaguzi wa serikali za mitaa kiasili haujawahi kuwa na mwamko wowote tangu kuwepo kwake. Hivyo idadi yoyote kubwa ya kuandikisha watu ni lazima iwe na utata. Sio halisi.

2. Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwisho ulijaa utata uliopitiliza na uliokatisha tamaa watu wengi kukataa kushirikishi. Hakuna muujiza wa kisiasa ungeweza kuligeuza hilo kwa haraka.

3. Watu wengi hujiandikisha ili kupata vitambulisho kuliko kwenda kupiga kura. Uchaguzi wa serikali za mitaa hauna vitambulisho, automatically mwamko wa kujiandikisha hauwezi kuwepo kwa watanzania wengi wa kawaida.

4. Idadi ya watu wanaokwenda kupiga kura kwenye chaguzi zote katika kipindi cha miaka 15 katika maeneo mengi imekuwa ikipungua kufikia chini ya 60% ya watu wote waliojiandikisha (sehemu nyingine ni chini ya 40%), ni jambo lisilowezekana katika mazingira hayo hayo idadi ya watu kujiandikisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa (uchaguzi usio na msisimko wowote) kuwa zaidi ya 90%.

5. Muda wa kujiandikisha umekuwa ni mfupi sana, sio rahisi kwa kila mkazi wa mtaa husika kuwepo eneo la mtaa wake ili kuweza kujiandikisha.

6. Watanzania wengi hawana ufahamu wa kutosha kutofautisha kuhusu zoezi hili la uandikishaji kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, zoezi la uboreshaji daftari la kudumu (zoezi ambalo lilifanyika kabla) na zoezi la uandikishaji kushiriki uchaguzi mkuu. Wengi wanaamini vile vitambulisho vya kura vinatosha kushiriki uchaguzi zote, popote na wakati wote.

7. Uchunguzi wa kawaida karibu maeneo yote ya uandikishaji mwamko ulikuwa uko chini mnoo, hakukuwa na watu, msururu wala msukumo.

8. Karibu kila mtu wa kawaida akimuuliza mwenzako (hata wewe msomaji unaweza kumuuliza jirani yako hapo ulipo) anakiri wazi hajajiandikisha na hakuwa na mpango wa kujiandikisha. Ni watu wachache sana wanakiri kujiandikisha, tena wale wenye misukumo mikubwa ya kushiriki siasa moja kwa moja.

9. Mbinu kubwa iliyofanywa na walimu (baada ya kupewa maagizo fulani ya vitisho!) ambao ndio walikuwa wanashiriki katika zoezi la kuandikisha ni kuletewa orodha ya majina kutoka kwenye kaya moja moja mtaani na wengine kujiongeza na kwenda kuyasaka wenyewe majina mitaani au kukaa chini na kubuni majina hewa. (Ndio mbinu hiyo iliyotumiwa na maafisa wa afya kuja na takwimu za utoaji chanjo ya Covid (UVIKO) kipindi kile ambapo waziri afya alikuja na takwimu za kuonyesha zaidi ya 90% ya watanzania walipewa chanjo)

10. Mtindo wa siku zote wa wajumbe wa nyumba kumi kumi za CCM kuchukua reja za wanachama wote wa CCM wa vitongoji vyao na kuyapeleka yaandikishwe na kujazia majina mengi hewa ili kuongeza idadi kama kawaida safari hii imetumika pia.

Kwa leo naashia hapa.
 
Kuna muda huwa nawaza hivi CCM wanatuaje watanzania? Au wanatuchukuliaje watanzania?
 
Umenena vzr sana, alafu kipindi hiki unaenda tu kujiandikisha kituo chochote bila kitambulisho. Yaani juma anaweza kujiandikisha vituo vyote vya kata yoyote alafu siku ya uchaguzi akazunguka kila kituo kupiga kura.
 
Sensa ya watu na makazi mwaka 2022 inaonesha zaidi ya nusu ya watanzania ni watoto wa miaka 0 hadi 15.Maana yake kati ya watu milioni 61(kwa makadirio),watu zaidi au milioni 30 ni watoto.Sasa iweje waandikishwe wapigakura milioni 30?Kwa hesabu ipi?Tunamdanganya nani?Tunataka kumfurahisha nani?Na tunataka kuonesha tuna uwezo wa akili ulio kwenye viwango vya aina gani?🤣🤣🤣🤣🤣
 
Maafisa kata wamepewa targets kufikisha idadi fulani ya waandikishwa kwa mbinu yeyote.

Nafikiri kuna mkakati wa siri unakuja wa ballot rigging.
 
Mimi mwenyewe na hadi ninapoishi hakuna aliyejiandikisha ...
 
Afu watakwambia wamepifa kampeni sana za kujiandikisha yaani pale jamaa wanaona walikuwa wanatuandaa kumbe hata sisi tulikuwa tunawachora tu.

Nadhani waandaaji wa hizi tawimu pamoja na kamati nzima ya mipango ya uandikishaji ina wapuuzi tu wanaohisi waTz ni wajinga. Ni bora wangeandika uhalisia then waendelee na wizi wao wa kura ili kupunguza sifa ya ujinga wa kitakwimu.
 
Mimi sikujiandikisha. Na sababu ya kutojiandikisha ni moja tu! Sina uhakika kama kura yangu itaheshimiwa iwapo nitashiriki zoezi la kupiga kura.
 
Maajabu yapo mwakani 2025,data zitapikwa had ziungue kuhusu kura na upigaji wake!! Siasa yetu imetuletea laaana asee.
 
Mimi sikujiandikisha. Na sababu ya kutojiandikisha ni moja tu! Sina uhakika kama kura yangu itaheshimiwa iwapo nitashiriki zoezi la kupiga kura.
Viongozi Wajinga wanachaguliwa na watu wasiopiga kura kama wewe, hupaswi kulalamika chochote, tulia kimya.
 
Na kwa nini hao viongozi wajinga wanachaguliwa na watu wasiopiga kura? Je, na nyinyi mnaopiga kura huwa mnaleta mabadiliko gani? Mbona bado washindi wanaotangazwa ni wale wale?
Unafikiri naweza kushawishika kirahisi kushiriki kwenye zoezi ambalo halina tofauti na mchezo wa maigizo? Am very sorry for that! But the answer is NO!

Uwepo wa Katiba Mpya na Tume Huru ya uchaguzi, ndiyo vitakomesha haya maigizo. Kinyume na hapo, endeleeni kujiandikisha na kushiriki kwenye hilo zoezi la kupiga kura! Na baada ya hapo, mje mlalamike kuibiwa kura na wateule wa Raisi na ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama tawala (DED/Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi)!
 
Back
Top Bottom