Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
Rais SSH na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania
Kwa mujibu wa utafiti wa Kitengo cha takwimu cha Taifa wa mwaka 2020, yaani NBS, takwimu za uhalifu nchini Tanzania zinaonyesha kuwa katika makosa ya jinai dhidi ya bnadamu, uhalifu wa mauaji unaongoza tangu 2016 hadi 2020.
Takwimu hizo ni kama ifuatavyo: Mwaka 2016 yalitokea mauaji ya watu 3,318; Mwaka 2017 yalitokea mauaji ya watu 3,026; Mwaka 2018 yalitokea mauaji ya watu 2,655; Mwaka 2019 yalitokea mauaji ya watu 2,619; na Mwaka 2020 yalitokea mauaji ya watu 2,225. Kwa hiyo, tangu 2016 hadi 2020 yalitokea mauaji ya watu 10,525.
Picha ifuatayo inaonyesha takwimu za mauaji na uhalifu mwingine pia. Mbali na mauaji makosa mengine yanayofanyika sana ni ubakaji, ulawiti, na kuvunja nyumba na kuiba.
Chanzo: NBS, 2020 Tanzania Main Land in Figures (p,70)
Kwa hiyo, kuna haja ya serikali kuchukua hatua za makusudi dhidi ya uhalifu huu. Napendekeza mambo yafuatayo yafanyike:
1. Kutunga sheria ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Uhalifu dhidi ya Uhai, kama ambavyo tuna mahakama ya kazi, mahakama ya ardhi, na mahakama ya biashara.
2. Kutenga bajeti kwa ajili ya kuendesha Mahakama ya ya Uhalifu dhidi ya Uhai.
3. Kuanzishwa kwa dawati maalum la Uhalifu dhidi ya Uhai katika vituo vyote vya polisi nchini Tanzania, likiwa na uwezo kamili wa kifedha kwa ajili ya operesheni za kuzuia, kukamata na kudhibiti wauaji. Dawati hili liratibiwe na kitovu kimoja cha kitaifa chenye nguvu ya kitekinolojia ikiwemo kumiliki magari, helikpota, na ndege za kijeshi.
4. Kanzisha gereza maalum kwa ajili ya watu wanaotekeleza makosa ya mauaji, na kulitengea bajeti maalum kwa ajili ya kupambana na wahalifu wanaofungwa huko.
Yaani, Mahakama ya Uhalifu Dhidi ya Uhai, Dawali la KIpolisi Kuhusu Uhalifu Dhidi ya Uhai, na Gereza la Wahalifu Dhidi ya Uhai, viwe ni vyombo vya kudumu kwa ajili ya kukuza na kuhami uhai nchini Tanzania.
Kwa ajili ya kulipa uzito jambo hili, Vyombo hivi viratibiwe na "Baraza la Taifa Kwa Ajili ya Kulinda Uhai (BATAKU)," yaani "National Advisory Council On LOngevity(NACOLO)."
Kwa ujumla, Baraza hili lipewe uwezo na wataalaam watakaokuwa wanaishauri seriklai kuhusu masuala yafuatayo, kati ya mengine:
- Biotechnology
- Bioethics
- Cloning
- Death
- Drugs, Children, & Behavior Control
- Human Dignity
- Manslaughter
- Memory Boosting/Suppression
- Mood Control
- Murder
- Nanotechnology
- Organ Transplantation
- Stem Cells