Katika miaka 240 tangu kuasisiwa kwa taifa la Marekani, ni miaka 16 tu ambayo Marekani haikuwa katika vita. Baada ya kumalizika kwa Vita Baridi, Marekani ilitarajiwa kuacha kufanya vita nje ya nchi, lakini nchi hiyo ilianzisha vita mara kwa mara zaidi kuliko awali. Takwimu zinaonesha kuwa katika zaidi ya miaka 30 iliyopita tangu kumalizika kwa Vita Baridi, Marekani imeanzisha vita 251. Ripoti ya Norton pia imeeleza kuwa vita za Marekani zinalenga nchi mbalimbali duniani, haswa nchi za Latin-Amerika, na Afrika.
Marekani imedai mara kwa mara kuheshimu na kulinda “utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria”, lakini nyaraka hizo zimeonesha kikamilifu kuwa Marekani ni nchi inayopenda vita, na inafanya umwamba bila ya kujali utaratibu wa kimataifa. Marekani inapaswa kusahihisha makosa ya kuanzisha vita duniani, kuacha kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine haswa kwa njia ya kijeshi, na kutoendelea kuwa mzushi mkuu wa vita duniani.