Uchaguzi 2020 Takwimu zinaongea wazi kwa CCM kushinda 2020

Uchaguzi 2020 Takwimu zinaongea wazi kwa CCM kushinda 2020

Rais Magufuli ameshushwa na Mungu kuja kutumikia Watanzania
Sio Mungu, kama Mungu ameshatuletea aliyemponya risasi 16 Tundu Antiphas Lissu!!

Huyo wa Magufuli ni mungu, tena mungu wa chato!!
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Eti mchagueni au jitayarisheni ku suffer huyu Rais wa Tunusia sijui walimuokota wapi
 
Hizo takwimu UCHWARA ulizoweka? Umeshasikia manung’uniko ya Wafanyakazi, Wakulima na Wafanyabiashara kuhusu miaka mitano iliyopita?

mbona unakataa takwimu tena?
 
Rais Magufuli ameshushwa na Mungu kuja kutumikia Watanzania
Alishushwa lini na akitokea wapi? Je ni huyu huyu Magufuli wa mwaka 1995, Magufuli wa mwaka 2000, Magufuli wa mwaka 2005 na Magufuli wa mwaka 20015 au mwingine?

Je ni huyu huyu Magufuli wa Mkapa na Magufuli wa Kikwete? Je ni huyu huyu Magufuli wa Gadafi kiongozi wa Kuwait hapana wa Iraq, Magufuli wa fent ford, Magufuli wa nyumba za serikali, Magufuli wa boti chakavu, Magufuli wa wasiojulikana au Magufuli wa Chato? Acheni kufuru ndugu zangu!
 
Tak
Uchaguzi ni takwimu, mikakati na mipango ambayo inaonekana wazi kwa macho. Hizo takwimu, mikakati na mipango ndio huwavuta wapiga kura kufanya maamuzi yao kwenye sanduku la kura.

Uchaguzi sio kampeni tu au kwenda kupiga kura lakini ni muunganiko wa matukio ya mikakati iliyowekwa kwa muda mrefu na hiyo ndio huwapa mwanga wa kwenda kufanya maamuzi...
Takwimu hii iko poa na haijadanganya hata kidogo.

Kwa jinsi hiib nidhahiri kuwa CCM wananafasi kubwa ya ushindi kulinganisha na vyama pinzani
 
Kilichofanyika na kuonekana pale Mwanza jiji la wasukuma pale!!!! Hiii wagosha!!!

Ningelikuwa ni Mimi mpinzani nayeomba nafasi ya uraisi, ilikuwa ni kusema, wewe Mzee bhana, malizia miaka yako tano basi, tena Kwa Moyo mweupe na kicheko juu, halafu tunaanza Kampeni za wabunge tu!
Kwa takwimu hizi ni sahihi kusema kuwa wapinzani wanajisumbua kugombea nafasia ya uraisi
 
Uchaguzi ni takwimu, mikakati na mipango ambayo inaonekana wazi kwa macho. Hizo takwimu, mikakati na mipango ndio huwavuta wapiga kura kufanya maamuzi yao kwenye sanduku la kura. Uchaguzi sio kampeni tu au kwenda kupiga kura lakini ni muunganiko wa matukio ya mikakati iliyowekwa kwa muda mrefu na hiyo ndio huwapa mwanga wa kwenda kufanya maamuzi...
Jinsi ccm na magufuli wao walivyovurugwa na Tundu Lisu hadi hizo takataka zote ulizoziorodhesha wamezisahau badala ya lile shangingi linakwambia Askari wao hawezi kushindwa kuua kwa risasi zaidi ya tatu
 
Takwimu hii iko poa na haijadanganya hata kidogo
Kwa jinsi hiib nidhahiri kuwa CCM wananafasi kubwa ya ushindi kulinganisha na vyama pinzani
Takwimu inayounganisha Tume ya Uchaguzi, polisi na vyombo vya dola au siyo?
 
Jinsi ccm na magufuli wao walivyovurugwa na Tundu Lisu hadi hizo takataka zote ulizoziorodhesha wamezisahau badala ya lile shangingi linakwambia Askari wao hawezi kushindwa kuua kwa risasi zaidi ya tatu
Hapana
Kwa mtu mwenye professional yake katika kitu Fulani kimsingi kumdhalilisha sio vizuri.

Hakuna mtu aliyefurahishwa na kitendo alichofanyiwa tundu lissu na ndio maana viongozi wengi was serikali walijitoa na kwenda kumfariji alipokuwa amelazwa pale Nairobi, lakini pamoja na hayo kuitumia Kama sababu ya kuitukana serikali wakati maswala kama haya hutokea sehemu nyingi na tofauti na sio serikali ianyokuwa inatekeleza Mambo hayo.

Sio vizuri kuupotosha umma kuwa umefanyiwa unyama na serikali sio sahihi na hata mm sikubaliani nayo
 
Uchaguzi ni takwimu, mikakati na mipango ambayo inaonekana wazi kwa macho. Hizo takwimu, mikakati na mipango ndio huwavuta wapiga kura kufanya maamuzi yao kwenye sanduku la kura. Uchaguzi sio kampeni tu au kwenda kupiga kura lakini ni muunganiko wa matukio ya mikakati iliyowekwa kwa muda mrefu na hiyo ndio huwapa mwanga wa kwenda kufanya maamuzi....
Mwaka huu Chama cha Mapinduzi kitapata ushindi mnono.
 
Hapana ndg nadhani haujaielewa vizuri hii post
Jaribu kuosoma tena utaielewa vizuri tu
Mbona Kama vile hii post imejaribu kujifafanua vizuri tu.
Sema ni kwa vile tupo kwenye upepo wa uchaguzi ila kimsingi Mambo yote yaliyo elezwa kwenye hiyo post ni sahihi na ipo sawa kabisa tukiacha uchama Wala ushabiki wa timu
 
Uchaguzi ni takwimu, mikakati na mipango ambayo inaonekana wazi kwa macho. Hizo takwimu, mikakati na mipango ndio huwavuta wapiga kura kufanya maamuzi yao kwenye sanduku la kura. Uchaguzi sio kampeni tu au kwenda kupiga kura lakini ni muunganiko wa matukio ya mikakati iliyowekwa kwa muda mrefu na hiyo ndio huwapa mwanga wa kwenda kufanya maamuzi...
Kutia hofu wafanyabiashara na kuwafugia kwa kizingizo cha kodi
 
wanaku bali kiana ccm oyeee
1599493751743.png
 
Hizi hoja zimeshabuma mzee. Tunataka kuwa huru. Tunataka serikali inayojali watu wake. Siyo hii isiyokuwa na ubinadamu iliyojaa ubaguzi
Wewe ni Uhuru gani unaotaka au unataka umun'gunywe,ninani hana Uhuru nchi hii,kumchora magu masoud kipanya anamchora,kumtukana tundulisu anamkejeli kila siku, kunya hamsimamiwi,mnatembea mpaka saa sita usiku,disko mnakesha sasa kipi mnataka MTU akivunja sheria ya maadili aachwe ndio maana ofisi za serikali wamepewa aina ya mavazi yatakiwayo,shuleni,bungeni,vyuoni sisi tuna maadili yetu kuheshimiana sisi sio wazungu wanaoishi kama kambale au wanyama wa porini,Kyle kila kitu kimeruhusiwa.
 
Uchaguzi ni takwimu, mikakati na mipango ambayo inaonekana wazi kwa macho. Hizo takwimu, mikakati na mipango ndio huwavuta wapiga kura kufanya maamuzi yao kwenye sanduku la kura. Uchaguzi sio kampeni tu au kwenda kupiga kura lakini ni muunganiko wa matukio ya mikakati iliyowekwa kwa muda mrefu na hiyo ndio huwapa mwanga wa kwenda kufanya maamuzi.

Kwa rekodi hizi zilizowekwa kwa miaka 5 tu ya awamu ya 5 inatosha kwa Rais Magufuli kutetea kiti chake Oktoba 28 mwaka huu tena kwa kishindo.

1. Sera ya Elimu bila malipo ambayo Serikali ya Rais Magufuli hutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 20 kila mwezi kwa ajili ya ada kwa wanafunzi kutoka darasa la kwanza mpaka kidato cha nne, kutoa fedha za ukarabati wa samani mashuleni, posho ya madaraka kwa walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu kata kila mwezi toka 2016. Hii ndio imesaidia kuongeza uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kutoka wanafunzi Million 1 mwaka 2015 mpaka zaidi ya Wanafunzi Million 1.6.

2. Ujenzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo katika Ziwa Victoria na ujenzi wa chelezo; ukarabati wa meli ya MV Victoria na MV Butiama ambapo katika kipindi cha mwaka 2015/16 hadi Aprili, 2020 jumla ya shilingi Bilion 111.7 zimetumika. Kwa kasi hii, hakuna mbadala wa ushindi kwa CCM. Fikiria tu huko nyuma kusafirisha mzigo wa ndizi wa tani 1 kutoka Kagera mpaka Mwanza ilikuwa zaidi ya Laki 1 lakini baada ya kumwagwa kwa Meli Ziwa Victoria leo mzigo huo unasafirishwa kwa elfu 27 tu.

3. Ujenzi wa Daraja la juu la Mfugale (Dar-es- Salaam), daraja la Furahisha (Mwanza) na daraja la Magufuli (mto Kilombero) umekamilika; ujenzi wa barabara ya pete (Ubungo interchange) umefikia asilimia 77 kwa shilingi bilioni 247; Aidha, ujenzi unaendelea kwa daraja la New Selander (Dar- es-Salaam) kwa shilingi Bilioni 270. Daraja la Kigongo- Busisi shilingi Bilioni 699.2. Takwimu zinaongea zenyewe.

4. Uboreshaji na upanuzi wa Bandari kuu za Tanga, Dsm na Mtwara kwa Shilingi zaidi ya Trilioni 1.2. Ujenzi wa Bandari ya Kigoma na Kalema umeshatengewa fedha 2020/21. Hapo unazungumza upanuzi wa bandari unaoenda kuongeza idadi ya bandari zetu kupokea mizigo na kusafirisha kwenda nchi mbalimbali tena zingine zaidi ya 8 kama Congo, Rwanda, Uganda na nyingine zikitumia bandari zetu kupata mizigo yao

5. Ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa ya Kimataifa (SGR) wa Kilomita 300 Dar-es-Salaam–Morogoro. Mradi uliofikia zaidi ya asilimia 78. Kipande cha Morogoro hadi Makutupora Kilomita 422 mradi umefikia asilimia 30 ya kazi. Lengo ni kukamilisha mradi huu ifikapo Juni 2021 kwa gharama ya Shilingi Trilioni 7.5. Wananchi wataichagua CCM ili kazi iendelee. Hili halina mjadala wala mbadala.

6. Usambazaji wa Umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umefikia Vijiji kwa asilimia 80% na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kwa kusambaza Umeme vijijini ambapo hadi Aprili 2020 shilingi trilioni 2.27 zimetumika na kufanikisha jumla ya vijiji 9,112 kati ya 12,268 vya Tanzania Bara kuunganishwa na umeme kutoka vijiji 2,118 tu mwaka 2015. Namba hazidanganyi, Ushindi kwa CCM hauitaji mjadala.

7. Ujenzi wa mradi mkubwa wa kufua umeme (Mwalimu Nyerere Dam) utakaozalisha Mg 2115 kwa sasa umefikia asilimia 40. Ujenzi una gharama ya Shilingi Trilioni 6.5. Mpaka mradi utakapoanza kufanya kazi nchi hii itakuwa na Umeme wa kutosha mpaka kuwa na ziada. Hapo fikiria Sekta ya viwanda itakavyong'aa.

8. Ujenzi wa miradi ya maji Vijijini na Mijini tumefikia asilimia 84 Mijini na asilimia 70.1 Vijijini. Kazi imefanywa na Serikali ya CCM. Hili nalo linahitaji Mjadala?

9. Kuimarisha huduma za afya kwa kujenga Zahanati, Vituo vya Afya, kujenga Hospitali za Wilaya, Mikoa, Kanda na za Kitaifa, huduma za Madawa na Vifaa Tiba. Tumejenga Zahanati 1,198 Vituo vya Afya 487, Hospitali za Wilaya 71, Hospitali za Rufaa za Mikoa 10, na Hospitali za Kanda 03 za Kusini – Mtwara, Magharibi – Tabora na Kanda ya Ziwa - Burigi.

10. Ufufuaji wa Shirika la Ndege kwa kununua ndege kumi na moja (11) ambazo zinatoa huduma mikoa yote yenye Viwanja vya Ndege na nje ya nchi.

11. Marekebisho ya Sheria ya madini yamefanyika sambamba na kuanzisha masoko ya madini 28 na vituo 12 vya ununuzi wa madini katika maeneo ya uchimbaji na hivyo kuongeza makusanyo ya Serikali, kupungua biashara haramu na utoroshaji madini kwenda nje. Mwezi Machi hadi Septemba, 2019 jumla ya kilo za dhahabu 4,680.28 zenye thamani ya shilingi bilioni 432.49 zimezalishwa na Serikali kukusanya shilingi bilioni 30.27.

12. Ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa shilingi Bilioni 800 kwa mwezi mwaka 2015 hadi wastani wa shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi katika kipindi cha Julai 2019 hadi Aprili 2020 na hii imekuja baada ya kuminya na kuziba mianya ya wakwepa kodi, mafisadi na misamaha holela ya kodi.

13. Hadi Aprili 2020 jumla ya viwanda vipya 8,477 vikiwemo vidogo, vya kati na vikubwa vimeanzishwa katika maeneo mbalimbali nchini na hivyo kuwezesha ongezeko la ajira viwandani za viwandani zipatazo 482,601. Takwimu zinasema na hazidanganyi.

Kimsingi yako mambo mengine kama vile mapambano dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma, uboreshaji wa miundo mbinu ya Elimu, kuongezeka kwa uwajibikaji na uwazi miongoni mwa watendaji wa Serikali na Urejeshaji na usimamizi wa mali za Ushirika zilizokuwa zimechukuliwa kinyume na utaratibu, kama vile, NYANZA, SHIRECU, KNCU, Mamlaka ya Mkonge Tanzania.

Sambamba na hayo yote, Benki ya Dunia, WB, tarehe 1 Julai 2020 imeiorodhesha Tanzania katika orodha ya nchi za uchumi wa kipato cha kati. Haya ni matokeo ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati iliyoongeza ajira kwa Watanzania wengi, Uongozi thabiti wa Rais John Pombe Magufuli katika kudhibiti matumizi ya fedha ya umma pamoja na kupambana na wale wanaotaka kufuja fedha ya umma.

Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania ililenga kuifikisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025 lakini nchi imewezeka kufikia uchumi wa kati 2020. Hili linaongeza sababu za kwanini, Ushindi Mkubwa wa CCM 2020, Hautakuwa na Mjadala wala Mbadala!

Bwanku M Bwanku
Umesahau kuweka number za simu upate teuzi.....TAKATAKA kama hizi ndio mwenyekiti wenu anazitaka
 
Back
Top Bottom