Talaka Ghali zaidi Duniani (Jeff Benzos vs MacKenzie Bezos)

Ziggy Sobotka

Member
Joined
Feb 13, 2019
Posts
19
Reaction score
36
Ndoa ya Billionea namba moja duniani mwanzilishi na mmiliki wa Kampuni ya mauzo mtandaoni ya Amazon Jeff Benzos na mkewe MacKenzie Bezos imeingia mchanga baada ya wanandoa hao kuamua kila mmoja afanye yake.
Wameshafungua jarada Mahakamani kwaajili ya kuivunja rasmi ndio hiyo iliyodumu kwa miaka 25 na kufanikiwa kupata watoto wanne (4).
Mahakama inategemea kumzawadia MacKenzie Bezos asilimia 4% ya hisa za kampuni ya Amazon zinazikadiliwa kuwa na thamani ya Dollar Billion 35 za Kimarekani na kumfanya kuwa Billionea wa nne kwa ukwasi (utajiri) kwa Wanawake huku Billionea wa kwanza kwa wanawake ni Françoise Bettencourt Meyers, aliyerithi kutoka kwa mama yake Liliane Bettencourt raia wa ufaransa.
Talaka hiyo kati ya Mkurugenzi huyo wa Amazon na mkewe imezua mjadala mitandani.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huyu ndio amejua kudanga sasa

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
Unamfahamu vizuri au umejisikia tu kusema hivyo?!!!
Sio wa mchezo mchezo kama unavyomdhania, inshort hajadanga.
 
Hii!!!! Kama walichuma wote sioni tatizo halafu wazungu wajanja sana sasa ww Mwafrica mwenzangu jaribu uone.... Mwanamke atakufilisi
 
Unamfahamu vizuri au umejisikia tu kusema hivyo?!!!
Sio wa mchezo mchezo kama unavyomdhania, inshort hajadanga.
Namfaham kuanzia plate number had chassis

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
 
Huyu Bezos si toka mwanzo walimsifu hajasaini mkataba wa kutomlipa mtalaka wake yamemkuta sasa!!..
 
Kuachana na mwanamke pasua kichwa hata akiondoka na mali zote ni bora kuliko kuwa na mali na changamoto ya mwanamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…