Talaka, ni suluhu ya migogoro ya ndoa?

Nakubaliana na wanaosema talaka ni suluhisho la "last resort". Njia nyingine zikishindwa, badala ya kuendelea kuishi katika hali ya kutegana; akikosea nammaliza; basi talaka ndo njia inayopendekezwa na wataalam wengi. Talaka haiepukiki kwenye mahusiano yaliyokwisha haribika na talaka ni suluhu haswaa.

Tatizo wengi wanatoa au kuomba talaka kama fimbo ya kuwachapia wenzao hasa pale wanapoona wenzao hawana kipato cha kuwakidhi pindi ndoa inapovunjika. Haya ni matumizi mabaya. Ila kwa kutatua migogoro iliyoshindikana ni afadhali talaka.
 

Kisukari mfano wako nimeukubali, ila si unajua binadaamu hususan wanandoa tunapaswa kuwa na mioyo ya kusamehe hususan kwa tatizo kama la kupigwa?
 

...kuna neno umelisahau hapo....Linaitwa (KUKUBALI "KWA ROHO SAFI")....
huwezi sema wahusika wakae iwapo mmoja, au wote hawajaridhia.
 
As much as TALAKA sio kitu kizuri, Sometimes ni suluhisho..... Kuna vitu havivumiliki jamani.... Kuna vitu vinauma Mno!!!

...naaam, tena kwa msisitizo nakubali liwe suluhisho la mwisho kuokoa
"uhai" wa mhusika au wahusika.... Kinachouma sio njaa, kiu, au tumbo...

Kwenye mapenzi kinachouma ni ROHO!
 
Mhuuuu! imebidi nigune kwa urefu.
Hii ni ishu tata na tambuka.

Hata sijui kama ni suluhisho, jambo la kuogofya, au ni ujinga. Maana heshima ya kuwa na ndoa watu tunaipenda lakini yaliyoko huko ,ni utata mtupu na saingine watu hawana talaka lakini pia ndoa huna , kwa maana ya uhalisi wa maisha ya ndoa.

Sijui hata kama nimesema jambo lenye mashiko ( substance) hapo juu lakini ngoja tusikie wanazuoni wengine watasemaje.

Binafsi yangu, topic hii inanigusa kiaina maana....
 
Wanawake wamekili kuwa ni kweli wanatoa vipigo kwa sababu wengi wamekuwa wanaume wa kuvaa Suluali tu, hawana lolote kuanzia Chumbani hadi Sebuleni, na wengine wanaishia kwenye Ulevi na wanawake, wakisahau wajibu wao kama Baba wa familia. Hayo ni ya Nairobi, hebu jiulize Ndoa yako ikoje? Ungefanyika utaratibu wa kukusanya taarifa za kila Ndoa, tungeshangaa kuona unyanyasaji mkubwa zaidi ya huo wa wenzetu wa kenya. Watu usiku hawalali ni mizozo usiku kucha utafikiri Vuvuzela, Ukatili wa kupigana na kutukanana ni mambo ya kawaida, Uaminifu katika Ndoa unakuwa adimu, upendo wa kweli na Furaha vinapotea kila kunapokucha, Vitendo vya kutelekeza familia na kuhamia kwa nyumba ndogo vinaendelea kushamiri, hivi mnafikiri kununiana mnapokuwa mumekoseana ndiyo suluhisho? Hilo ni pepo la hasira, tunalikemea kwa jina Yesu litoke, ili tabasamu na vicheko virudi.


Mtumishi wa Mungu Paulo anasema “Tukijua neno hili ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike” Wewe mwanaume na mwnamke unayejiita Mtu wa Mungu, Sulubisha miguu yako isipige mateke wenzio wala kunyatia nyumba za wageni kwa Zinaa, Sulubisha Midomo na Ulimi visitoe matusi na kupiga kisi makahaba na wezi wa mapenzi pia visulubiwe ili visilambe Vileo, Sulubisha macho yasiwe mepesi kukonyeza wake na waume za watu na yasione yasiyofaa, Sulibisha mikono isiwe myepesi kupigana na kukumbatia vifua vya asiye mpenzi wako, Sulubisheni Moyo usijae tama mbaya ya zinaa, hasira, chuki, kiburi, ukaidi, Roho mbaya, visasi n.k. Viungo vyote vya siri vinavyowaka tamaa mbaya ya mwili vinapaswa kulubishwa. Neno linasema “Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha MWILI pamoja na MAWAZO yake mabaya na tama zake” Wagalatia 5:24. Matatizo yote yanayozikabili Ndoa za siku hizi yanasababishwa na wanandoa kutokuwa na Yesu katika maisha yao. Kusulubisha mwili ni kuua Utu au Tabia za Kale za Dhambi na kuzaliwa katika Kristo kwa Imani ili tuwe na Upendo ambayo ni tabia ya Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…