Wanawake wamekili kuwa ni kweli wanatoa vipigo kwa sababu wengi wamekuwa wanaume wa kuvaa Suluali tu, hawana lolote kuanzia Chumbani hadi Sebuleni, na wengine wanaishia kwenye Ulevi na wanawake, wakisahau wajibu wao kama Baba wa familia. Hayo ni ya Nairobi, hebu jiulize Ndoa yako ikoje? Ungefanyika utaratibu wa kukusanya taarifa za kila Ndoa, tungeshangaa kuona unyanyasaji mkubwa zaidi ya huo wa wenzetu wa kenya. Watu usiku hawalali ni mizozo usiku kucha utafikiri Vuvuzela, Ukatili wa kupigana na kutukanana ni mambo ya kawaida, Uaminifu katika Ndoa unakuwa adimu, upendo wa kweli na Furaha vinapotea kila kunapokucha, Vitendo vya kutelekeza familia na kuhamia kwa nyumba ndogo vinaendelea kushamiri, hivi mnafikiri kununiana mnapokuwa mumekoseana ndiyo suluhisho? Hilo ni pepo la hasira, tunalikemea kwa jina Yesu litoke, ili tabasamu na vicheko virudi.
Mtumishi wa Mungu Paulo anasema Tukijua neno hili ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike Wewe mwanaume na mwnamke unayejiita Mtu wa Mungu, Sulubisha miguu yako isipige mateke wenzio wala kunyatia nyumba za wageni kwa Zinaa, Sulubisha Midomo na Ulimi visitoe matusi na kupiga kisi makahaba na wezi wa mapenzi pia visulubiwe ili visilambe Vileo, Sulubisha macho yasiwe mepesi kukonyeza wake na waume za watu na yasione yasiyofaa, Sulibisha mikono isiwe myepesi kupigana na kukumbatia vifua vya asiye mpenzi wako, Sulubisheni Moyo usijae tama mbaya ya zinaa, hasira, chuki, kiburi, ukaidi, Roho mbaya, visasi n.k. Viungo vyote vya siri vinavyowaka tamaa mbaya ya mwili vinapaswa kulubishwa. Neno linasema Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha MWILI pamoja na MAWAZO yake mabaya na tama zake Wagalatia 5:24. Matatizo yote yanayozikabili Ndoa za siku hizi yanasababishwa na wanandoa kutokuwa na Yesu katika maisha yao. Kusulubisha mwili ni kuua Utu au Tabia za Kale za Dhambi na kuzaliwa katika Kristo kwa Imani ili tuwe na Upendo ambayo ni tabia ya Mungu.