Talaka yazua gumzo na kupelekea utajiri nchini Korea Kusini ,Je ni sawa?

Talaka yazua gumzo na kupelekea utajiri nchini Korea Kusini ,Je ni sawa?

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Mahakama ya Korea Kusini imemuamuru bilionea wa teknolojia na Mwenyekiti wa SK Group, Chey Tae-won, kumlipa aliyekuwa mkewe, Roh So-yeong, won bilioni 944, sawa na takribani dola milioni 640, (Shilingi za kitanzania Trilioni 1.69) katika moja ya kesi kubwa zaidi za talaka kuwahi kushuhudiwa nchini humo.

Uamuzi huo ulitolewa na Mahakama Kuu ya Seoul baada ya mapambano ya muda mrefu ya kisheria kati ya Chey na Roh, ambaye ni binti wa aliyekuwa Rais wa Korea Kusini, Roh Tae-woo. Vyombo vya habari nchini humo vimeipa kesi hiyo jina la “talaka ya karne” kutokana na utajiri mkubwa unaohusika pamoja na ushawishi wa familia hizo mbili katika siasa na biashara.

Soma zaidi:Aliyekuwa waziri wa sheria Korea Kusini aburuzwa miaka 25 jela

Kiasi hicho ni kidogo kuliko won trilioni 1.38, takribani dola milioni 940, (Trilioni 2.4 za kitanzania) ambazo mahakama hiyo hiyo ilikuwa imeamuru Chey alipe mwaka 2024.

Mahakama ya Juu baadaye iliagiza sehemu ya mgawanyo huo ipitiwe upya, hatua iliyosababisha malipo kupunguzwa hadi $ milioni 640.

Mbali na mgawanyo wa mali, Chey alikuwa tayari ameagizwa kumlipa Roh won bilioni mbili, sawa na karibu dola milioni 1.3, kama fidia inayohusiana na kuvunjika kwa ndoa yao.

Mahakama iliamua kuwa mali zilizopatikana wakati wa ndoa yao, zikiwemo hisa za SK Inc., zilitokana na juhudi za pamoja za wanandoa hao.

Ingawa Roh hakuhusika moja kwa moja katika kuendesha kampuni, mahakama ilitambua mchango wake katika familia na shughuli za kijamii zilizosaidia hadhi na ukuaji wa kundi hilo la biashara.

Hata hivyo, Mahakama ya Juu ilikataa hoja kwamba fedha zilizodaiwa kutoka kwa baba yake Roh, aliyekuwa Rais Roh Tae-woo, zilisaidia kuijenga SK Group.

1785838084578.png


Madai hayo hayakujumuishwa katika hesabu mpya ya mali baada ya mahakama kusema hayakuwa na msingi wa kutosha wa kisheria.

Roh alikuwa ameomba sehemu kubwa ya mali za Chey, ikiwemo karibu nusu ya thamani ya hisa zake katika SK Inc

Source:Simulizi na sauti
 
Back
Top Bottom