Taliban wamewawewesesha Wazungu

Taliban wamewawewesesha Wazungu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wazungu wako bize kutuma madege kuhamisha "watu wao" kutoka Afghanistan baada ya Wataliban kuiangusha serikali yenye askari waliofunzwa vizuri kwa miaka 20 na kupewa silaha nyingi za kisasa na ujuzi wa kuzitumia. Kinachowauma na kuwashangaza wazungu ni:

1. Kwanini Askari wenye silaha bora walishindwa kienyeji na wataliban kiasi kile
2. Silaha zao za kisasa kutekwa na kuangukia mikononi mwa Taliban
3. Wataalam waliofunzwa vizuri mbinu za kijeshi na matumizi ya silaha hizo kuangukia mikononi mwa taliban kindezindezi

Ukweli ni kwamba ndege zile sio tu wamekwenda kuwaondoa wazungu wenzao bali Waafghanistan waliopewa ujuzi wa hali ya juu ili wasiangukie kwenye mikono ya watalibani, na huenda wengi wao wakauwa.

Funzo hapa ni kuwa kuna wakati ukifika hata wanajeshi waliofunzwa vizuri na kupewa silaha za kisasa watawageuka watawala wabadhilifu, madalali wa nchi yao wanashirikiana mabeberu kuinajisi nchi yao na wasiowalipa vizuri maslahi yao. Kuna siku wanajeshi pia watawaelewa na kuungana na wale wote uwanaoibiwa kura wakati wa uchaguzi, wanaobambikiwa kesi na wanasiasa na wanaofuja rasilimali za nchi. Siku kama hizi haziko mbali.

Wataliban walipoulizwa kwanini hamkupata upinzani mkubwa kuichukua nchi kwa muda mfupi walijibu kuwa wananchi na wanajeshi walituelewa kile tunachokipigania na walituunga mkono. Alisema shida zetu ndizo shida zao, mavazi yetu ndiyo mavazi yao pia, tunavaa kama raia, shida za tozo ya miamala ndizo shida zao pia, ukosefu wetu wa maji na huduma ndio ukosefu wao pia, tabu zetu na wao wanazipata pia, na wasiwasi wetu ndio wasiwasi wao pia.

Wazungu hawaamini tena Waafghanstan tena, hawakuamini kama askari na wananchi watawageuka kiasi kile. Waligundua kuwa wale askari waliowapa mafunzo kumbe wote ni mataliban, hawezi kurudi kule hata siku moja.
 
Msubirini mbowe mtalibani wenu
Ni maswala ya wakati tu bro, anachodai Mbowe leo wewe huna uhakika kinaungwa mkono na watu wangapi na akina nani, nyamaza. Kuna siku nimewasikia vijana wakisema kuhusu CCM kuhodhi hata viwanja vya kuchezea mpira ambavyo hawavihudumii, yaani kuna siku wananchi watakinai kila kitu. HATA NYAMA ni mlo mzuri, lakini hakuna anaependa kula nyama kila siku na milele
 
Back
Top Bottom