Taliban Washerehekea Miaka 3 ya kuitwanga na kuifurusha Marekani nchini mwao

Taliban Washerehekea Miaka 3 ya kuitwanga na kuifurusha Marekani nchini mwao

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Taliban wmefanya gwaride kubwa kwa kutumia magari ya deraya na silaha kibao walizowateka Wamarfekani miaka 3 nyuma.

Ikumbukwe kuwa Taliban waliingia vitani na Wamarekani kwa miaka 20 mfululizo baada ya Wamarekani kuwashmabili na kuwataka kuiondowa serikali ya wanafunzi (Taliban) kwa mabavu baada ya Taliban kukataa katakata kumsalimisha Osama BinLaden kwa "kosa amablo hawalijui" kwa usemi wao.

Marekani kwa kujimwambafai wakapeleka majeshi yao wakishirikiana na Majeshi ya Uingereza na NATO nzima. Taliban wakasema hatujawahi kushindwa na yeyote duniani na Afghanistan haijawahi kutawaliwa na nchi yoyote ya nje toka iumbwe dunia, haitotokea hilo kwenye utawala wetu.

Taliban Wakatimiza hilo baada ya miaka 20 ya kuwanyuka Wamarekani na NATO nzima. Licha ya Wamarekani na NATO kuwa na voifaa vya kisasa na zana za teknolojia bora kabisa za kivita,Taliban walikuwa wanawatandika kiaina yake na ushujaa wa hali ya juu, huku wakisema silaha ni sisi wenyewe saiyo hizo toys zenu.

Taliban walitumia silaha za kujiundia wenyewe na wanazoziteka kutoka majeshi ya Marekani na NATO. Wakawatembezea kichapo Wamarekani mpaka Wamarekani wakati wa Obama wakapiga marufuku vyombo vya habari kuonesha picha za masandauku ya maiti ya wanajeshi wao zinazorudi kutokea Afghanistan.

Matokeo, Wamarekani wakakiri kushindwa kimya kimya kwa kutoka nduki na kuwacha nyuma silaha na vifaa vinavyokadiriwa kua na thamani ya US Dollars Billion 7.

Kishujaa na kwa kutamba kabisa, juzi na kila mwaka kuanzia wapate ushindi, wamefanya sherehe za paredi kwa vifaa vya kijeshi na silaha za Wamarekani.

Jionee sherehe hizo...

View: https://youtu.be/RZYZONPhqZ8?si=uW2_4Ky2GXXaBw2g
 
hawa jamaa ni mafia waliishi porini miaka 20 hatimae wakaja kuganikiwa kushika dola
Taliban wameidhihirishia dunia kuwa Marekani na NATO wanapigika kiulaini na wameifundisha dunia namna ya kuwapiga hao mashetani. Mbinu hizo hizo ndio kwa sasa zinatumika Ghaza, Syria, Iraq na Yemen. Marekani na mashoga zake wanadonyolewa kidogo kidogo. Wakikasirika wanakuja na dege na mabomu ya tani 2000 wanapiga weee watu wapo mapangoni, wakitulizana, wanakuja vijana wanadonyoa wanarudi mapangoni.

Umeona walichoonesha hezbollah juzi?
 
Talibana wmefanya gwaride kubwa kwa kutumia magari ya deraya na silaha kibao walizowateka Wamarfekani miaka 3 nyuma.

Ikumbukwe kuwa Taliban waliingia vitani na Wamarekani kwa miaka 20 mfululizo baada ya Wamarekani kuwashmabili na kuwataka kuiondowa serikali ya wanafunzi (Taliban) kwa mabavu baada ya Taliban kukataa katakata kumsalimisha Osama BinLaden kwa "kosa amablo hawalijui" kwa usemi wao.

Marekani kwa kujimwambafai wakapeleka majeshi yao wakishirikiana na Majeshi ya Uingereza na NATO nzima. Taliban wakasema hatujawahi kushindwa na yeyote duniani na Afghanistan haijawahi kutawaliwa na nchi yoyote ya nje toka iumbwe dunia, haitotokea hilo kwenye utawala wetu.

Taliban Wakatimiza hilo baada ya miaka 20 ya kuwanyuka Wamarekani na NATO nzima. Licha ya Wamarekani na NATO kuwa na voifaa vya kisasa na zana za teknolojia bora kabisa za kivita,Taliban walikuwa wanawatandika kiaina yake na ushujaa wa hali ya juu, huku wakisema silaha ni sisi wenyewe saiyo hizo toys zenu.

Taliban walitumia silaha za kujiundia wenyewe na wanazoziteka kutoka majeshi ya Marekani na NATO. Wakawatembezea kichapo Wamarekani mpaka Wamarekani wakati wa Obama wakapiga marufuku vyombo vya habari kuonesha picha za masandauku ya maiti ya wanajeshi wao zinazorudi kutokea Afghanistan.

Matokeo, Wamarekani wakakiri kushindwa kimya kimya kwa kutoka nduki na kuwacha nyuma silaha na vifaa vinavyokadiriwa kua na thamani ya US Dollars Billion 7.

Kishujaa na kwa kutamba kabisa, juzi na kila mwaka kuanzia wapate ushindi, wamefanya sherehe za paredi kwa vifaa vya kijeshi na silaha za Wamarekani.

Jionee sherehe hizo...

View: https://youtu.be/RZYZONPhqZ8?si=uW2_4Ky2GXXaBw2g

Taliban wamidhhirishia dunia kuwa Marekani na NATO inapigika na wameifundisha dunia namna ya kuwapiga hao mashetani. Mbinu hizo hizo ndio kwa sasa zinatumika Ghaza, Syria, Iraq na Yemen. Marekani na mashoga zake wanadonyolewa kidogo kidogo. Wakikasirika wanakuja na dege na mabomu ya tani 2000 wanapiga weee watu wapo mapangozni, wakitulizana, wanakuja vijana wanadonyoa wanarudi mapangoni.

Umeona walichoonesha hezbollah juzi?
Je, wewe binafsi unafurahia Utawala wa kidhalimu wa Hawa Watu ambao wamewapiga marufuku kabisa Wanawake wenzako huko Afghanistan wasifanye kazi yoyote ile zaidi ya kukaa ndani tu usiku kucha na mchana kutwa??
 
Kipindi Trump akiwa Madarakani aliona Marekani haina sababu ya jeshi kuendelea kubaki Afghanistan, kama ni kushinda vita walishashinda kwa kuichomoa serikali ya Taliban, hakukuwa na sababu ya kuendelea kubaki.

Trump alimchimba mkwara kiongozi wa Taliban wakiwa kwenye kikao alimpa karatasi inaonyesha sehemu familia yake inaishi, Akaondoka kikaoni bila kuongea cha ziada, kwa miezi 18 mfululizo mpaka anapoachia ngazi, Taliban hawakuthubutu kuua wala kumgusa Mmarekani yeyote.

Taratibu zilianza za kuliondoa jeshi kwa heshima (Leaving with honor) kuwaachia wa Afghanistan nchi yao wajiongoze kwa serikali iliyokuwepo, Walibaki wanajesi wamarekani wachache wanaokamilisha mambo ya kurudisha silaha Marekani, kuziharibu, n.k.

Biden kaingia Madarakani mipango yote ya kuondoka kwa heshima ikavurugika, Taliban ilimuona Biden ni kama mdori ikapindua serikali na kuanza kuua wanajeshi wamarekani, walipora jeshi la Marekani silaha zilizobaki zenye thamani ya dola bilioni 80, Biden alichukulia poa tu.

Trump ni chuma kinachohitajika kurudi white house sio hawa kina Biden na Kamala.
 
Je, wewe binafsi unafurahia Utawala wa kidhalimu wa Hawa Watu ambao wamewapiga marufuku kabisa Wanawake wenzako huko Afghanistan wasifanye kazi yoyote ile zaidi ya kukaa ndani tu usiku kucha na mchana kutwa??
mkuu Julian asange alitoa report 2010 huko miaka 14 iliopita kuwa jamaa watatumia feminism kuhalalisha uvamizi wa Afghanistan
Wikileaks, founded by Julian Assange, who is still in prison, recently reminded me of the CIA report he disclosed in 2010.

According to the report, if the Netherlands withdraws its troops from Afghanistan, other NATO countries are likely to follow. The U.S. Central Intelligence Agency (CIA) appears to suggest using feminism to legitimize its invasion of Afghanistan, which was in its 10th year at that time, in the eyes of the European public.

sasa hivi kila chombo cha habari kinarepoti hayo mambo na kukupa wewe na wengine wasiojua kinachoendelea Afghanistan perception tofauti. ngoja nikurudishe mwaka 2001 kwanza,

kabla ya marekani kuvamia hapo Taliban walikua wakipigana na waasi wanaitwa Northen alliance, baada ya USA kuingia wakawapindua Taliban na kuwaweka Northen Alliance madarakani, Taliban walikua wakipingana na madawa ya kulevya na Northern alliance walikuwa ni Drug dealers.

source hii hapa ya 2001 toka chombo cha habari cha marekani

fast forward sasa hivi Taliban, kila watu watatu basi mmoja ni teja, nchi nzima watu wanabwia unga, si wanawake si wanaume, unaendesha vipi nchi ikiwa na nguvu kazi ambao wana arosto muda wote? hii ni legacy kubwa ya USA hapo Afghanistan kuua taifa lote na kuhakikisha kila mtu ni teja akishirikiana na hao jamaa.

hapa kabul
afghan.png

kitu cha kawaida sana kuwakuta hao jamaa wamekaa wanavuta hizo opium.

mpaka watoto wameathirika
_121796558_oct14-gettyimages-1235875213.jpg

hio ndio situation yao kubwa ya sasa, na ndio taifa waliorithi toka kwa machampion wa Demokrasia, ili kukutoa kwenye reli usielewe mambo kama haya zinakuja hizo hoja za wanawake.

turudi kwenye hizo haki za wanawake na watoto.
afghanistan kuna kitu kinaitwa "bacha bazi" aka boy play ambayo Askari na watu wakubwa huko Afghanistan walikua wanafanya, unakuta mtoto wa kiume anafungwa kibwebwe anafosiwa kumkatikia Askari hadi wanabakwa, maelfu ya watoto wamebakwa na Usa na washirika wake, Asange ana leaks zake na kuna report nyingi New york times na wengineo, Clinton na Pentagon kwa ujumla walikua wakizua information zisitoke

hizi isue zilikuja kuwa connected na watoto wa Haiti na ring nyengine za pedophile duniani ambazo hao hao kina Clinton wanahusika.

sasa mkuu niambie, assume wewe ndio kiongozi wa Afghanistan kwa sasa what will be your priorities?
 
Walivyotangaza Wamarekani ni Pakistan, Lakini ukweli ni kuwa Osama alishakufa kwa amri ya Mungu siku nyingi, Wamarekani wakatumia advantage ku act kama wamempata. Ulisikia wapi mtu anatolewa nchi kavu kwenda kuzikwa baharini?

Wamarekani waongo sana.
Kwanini umeamua kuwa mwongo?

Talebani walifanya mazungumzo na marekani wakakubaliana kuachiwa nchi yao.

Marekani hakukimbia,walielewana.

Acha Uongo.
 
Taliban hawana uwezo wa kumpiga Marekani hata dakika moja, usijidanganye, na kudanganya wasiojua ukweli.

Kilichotokea ni hiki; baada ya Marekani kukaa Afghanistan na kutoa mafunzo ya kijeshi kwa jeshi la Afghanistan, ikiwa ni pamoja na kuwapa silaha, lakini bado askari wa Afghanistan ni waoga waliokimbia vita na Taleban baada ya Marekani kuondoka huko.

Ndio nchi ya Marekani wakaona tunapoteza nguvu zetu bure, tuachane nao hao jamaa, hapo ndio Taleban wakajiachia. Lakini kama Marekani angeamua kurudi Afghanistan kuwatimua hao ndugu zako katika imani, ilikuwa wapotezwe dakika moja tu.
 
Ndo kupigwa kwenyewe huko.
Sasa kama malengo yako ya kijeshi hayakufanikiwa kwa miaka 20 na umetumia zaidi ya dola trilion 8 na adui bado yupo sasa hapo umeshinda vita au umeshindwa vita?
 
Taliban wamidhhirishia dunia kuwa Marekani na NATO inapigika na wameifundisha dunia namna ya kuwapiga hao mashetani. Mbinu hizo hizo ndio kwa sasa zinatumika Ghaza, Syria, Iraq na Yemen. Marekani na mashoga zake wanadonyolewa kidogo kidogo. Wakikasirika wanakuja na dege na mabomu ya tani 2000 wanapiga weee watu wapo mapangozni, wakitulizana, wanakuja vijana wanadonyoa wanarudi mapangoni.

Umeona walichoonesha hezbollah juzi?
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 akili zako hazija mature, marekani bado inaiongoza talibani. Na talibani ni simba asiye na meno
 
Back
Top Bottom