Tamaa!khaaaa!!!

Tamaa!khaaaa!!!

Samawati

Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
90
Reaction score
71
Kakuambieni nani kuwa tamaa ndio hufanya watu kuwa na mahusiano nje ya yale walio nayo ( ndoa, uchumba n.k)??
Nachoka kusikia kila mara mkisema ...kapata mtu mwingine shauri ya tamaa.kwani binadamu kupenda mtu mwengine ni ajabu? Mi sidhani ni tamaa..au mnifafanulie tamaa maana yake nini.
 
Tamaa = Kutamani
ndio unaweza ukapenda mwingine lakini mara nyingi ni kutamani kile ambacho hauna... hence unakitaka hicho... You can love One person at a time lakini kuwa nao wawili watatu au wanne....... ?? Am Sorry hapo ninaona kuna katamaa kidogo kanachangia...., (the grass is always greener on the ather side)
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kutamani na kupenda... Huwezi kupenda zaidi ya mtu mmoja, ila unaweza kutamani hata 10. N tamaa mara zote huletwa na fikra, mfano unamuona mwanamke ana hips nene unaanza kuwaza hivi mziki wake utakuwaje kwahiyo hata ukimpata ni kwasababu ya tamaa yako ya kutaka kujaribu na kuona kama mambo iko. Tamaa siku zote huwa ina sababu, ina chanzo tofauti na mapenzi ya kweli!!!
 
Mtu anaecheat ni tamaa tu inamsumbua!Kama ni swala la kupenda kweli amwache alie nae ili aende huko anapopenda!Kutamani ni kutaka huku na huku...yani kutoridhika na kitu kimoja..in this case mtu mmoja!
 
mi nakubaliana na mawazo yenu kuwa ni mawazo yenu.

KWANI unapokuwa na mtu....akakuumiza sana na huna namna ya kumwacha.... yeye hakupendi tena na WEWE pia humpendi tena...huwezi kumpenda mtu mwingine?Ukimpenda mtu mwingine itakuwaje TAMAA?
 
Hata asipokuumiza Love can grow and it can die.., kwahiyo circumstances zitafanya pendo lako life, au hata kama mwanzo hapakuwa na upendo kuwe na upendo kwahiyo katika kila instant unaweza ukawa unampenda sana mtu mmoja.

Kwahiyo ili tuepuke upendo wetu kufa ni bora tujijengee kuvumilia na ku-concentrate kwenye mazuri yote ya wenza wetu..., sababu bila kufanya hivyo maudhi ya kwenye relation yanaweza kuua pendo letu na tukaamie pengine ambapo mwanzo kutakuwa na upendo lakini baada ya maudhi na hapo upendo ukaisha...
 
Mi hua nna mawazo tofauti kabisa. Kwanza sikubali kwamba eti mtu huwezi kupenda zaidi ya mtu mmoja kwa wakati mmoja. Unaweza! Na wala si tamaa, ni nature. Hii mentality ya kupenda mtu mmoja ni man-made na ndio maana most of the times inawashinda watu. (Hii tabia ya kuchanganya kiswahili na kingereza inani bore kama nini!)
 
I support you for your post,Hiyo kitu imeumbwa kwa kila kiumbe kiitwacho dume na hakuna tamaa ni urijali tu,kwani kuna mtu yeyote aliyewahi kuona mitamba ikipigana kugombea dume?Lakini yaweke madume japo mawili tu pamoja uone yatakavyotifuana.......
 
Mmmmmmh huu ukweli unauma!! Hebu ngoja nijaribu kuumeza kama nitaweza!!!!
 
Mi hua nna mawazo tofauti kabisa. Kwanza sikubali kwamba eti mtu huwezi kupenda zaidi ya mtu mmoja kwa wakati mmoja. Unaweza! Na wala si tamaa, ni nature. Hii mentality ya kupenda mtu mmoja ni man-made na ndio maana most of the times inawashinda watu. (Hii tabia ya kuchanganya kiswahili na kingereza inani bore kama nini!)
:confused2::confused2::confused2::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
 
Kakuambieni nani kuwa tamaa ndio hufanya watu kuwa na mahusiano nje ya yale walio nayo ( ndoa, uchumba n.k)??
Nachoka kusikia kila mara mkisema ...kapata mtu mwingine shauri ya tamaa. kwani binadamu kupenda mtu mwengine ni ajabu? Mi sidhani ni tamaa..au mnifafanulie tamaa maana yake nini.

Tujiulize, mfano una mwanamke/mwanaume wa nje halafu siku unakaa unajiuliza "HIVI KWELI TAMAA NDO IMENIFANYA NIKUBALI KUWA NAE YULE?? MBONA HANA ALICHONITAMANISHA?? . . . . . HAPANA, SI KWELI. YULE ANAJUA KUSOMA HISIA ZANGU KULIKO HUYU WANGU, HALAFU HANIFOKEI, ANANISIKILIZA PIA, HUYU WANGU HANIFANYII HAYO YEYE AKIRUDI NYUMBANI AMESHALEWA"

Sio tamaa aisee. Unaweza ukapenda watu tofauti kutokana na mambo tofauti wanayokufanyia ambayo mwingine hakufanyii
 
Exactly ni tamaa ya kuwa na maisha ya mtu anayekuelewa vema anayesoma hisia zako na ambaye hakufokei... kwahiyo upendo wako kwa A unaweza ukafa na ukaanza kumpenda B.... lakini mara nyingi kumbe B alikuwa anakuvutia bila kuonyesha true colours baada ya kukaa nae unagundua kwamba kumbe B ni kama A sasa unaanza kumuangalia C....

Before you know it umefika Z na unagundua kwamba kumbe A ni Bora...
 
kwa wengine si tamaa, ila ni kuwa kwenye uhusiano na mtu ambaye huelewi nafasi yako kwake... So inafika kipindi unaona ni bora nipate pa kujishikiza ili siku nikila kibuti maumivu yawepo ila pa kupoozea nako kupo...
 
Back
Top Bottom