Bichwa ndani ya dryer
Member
- Sep 22, 2026
- 64
- 124
Nimekuja kugundua kwamba tamaa ya ngono ni miongoni mwa tamaa hatari zaidi ambazo mwanadamu anapaswa kujifunza kuzidhibiti. Tamaa hii isipodhibitiwa inaweza kuwa chanzo cha mashaka, hofu, matumizi mabaya ya fedha, migogoro ya kifamilia, ajali, kupoteza heshima katika jamii, na hata kusababisha mauaji au vifungo visivyo vya lazima.
Mtu anapojifunza kuitawala tamaa hii badala ya kutawaliwa nayo, anajipa nafasi ya kuishi maisha yenye furaha, utulivu na amani ya akili. Ni aina ya uhuru unaokufanya usiwe mtumwa wa hisia na misukumo yako.
Sisemi haya kwa sababu nimejiunga na kundi la kataa ndoa. La hasha! Ninapinga vikali falsafa ya kukataa ndoa kwa sababu ya tamaa au sababu nyinginezo zisizo na msingi. Ninachomaanisha ni kwamba watu wafunge ndoa, wapendane na waheshimiane, lakini pia wazingatie ushauri wa Biblia: kuoa na kuishi kana kwamba hawajaoa.
Kwa maana nyingine, ndoa isiwe sababu ya kupoteza nidhamu, kujitawala au mwelekeo wa maisha. Jifunze kuitawala tamaa yako, usiiruhusu ikutawale.
Kumbuka: Mwanadamu mwenye nguvu si yule anayeweza kutimiza kila tamaa aliyonayo, bali ni yule anayeweza kujizuia pale inapohitajika.