SoC02 Tamaa ya 'upekee' na 'kuweka kumbukumbu' inasababisha ubinafsi katika taifa!

SoC02 Tamaa ya 'upekee' na 'kuweka kumbukumbu' inasababisha ubinafsi katika taifa!

Stories of Change - 2022 Competition

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Habari wanaJF?

Nami nimeona nishiriki katika jukwaa hili la soc kwa kutoa mawazo yangu kuhusiana na mada tajwa hapo juu.

Kumekuwepo na tabia ya watu wengi sana katika familia, jamii, kazini, shuleni serikalini na kwingineko; kupenda kutumia neno mimi pekee yangu nilifanya hili au lile, mimi pekeyangu niliweza kufanikiwa katika haya na yale!

Kwa mfano katika ngazi za kiserikali utamsikia mtu akisema "mimi ndiye mwanamke pekee niliyechaguliwa" au mimi ndiye mtanzania pekee niliyefanikiwa kupata kitu fulani.

Hata kama watu hao hawatajisemea wao binafsi, basi watasemewa na watu wengine.
Suala la msingi hapa sio huo upekee, bali kinachotatiza ni namna upekee huo unavyoonekana kama ufahari!

Kwa namna yoyote ile, jambo linaloonekana kama ufahari, husababisha ushindani na ubinafsi. Baadhi ya watu hushikwa na tamaa ya kuendelea kuwa pekee ili waweze kuweka kumbukumbu isiyovunjwa.

Hali hii pia husababaisha (hasa kwa siku za hivi karibuni) baadhi ya watu hasa viongozi, kutoa takwimu au historia sizizo sahihi ilimradi tu waonekane wa kipekee.

Kauli za 'hili halijawahi kufanyika, huyu ndiye wa kwanza kulifanya, hiki ni kitu kipya katika nchi yetu' zinasababisha mkanganyiko wa historia zilizokuwepo hapo kabla!

Jambo hili si tu kwa taifa la letu, bali hata kwa mataifa mengine. Mfano utasikia taarifa ya mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani akitokea taifa fulani ilihali kwenye mataifa mengine kuna wenye umri mkubwa kuliko huyo.

Sasa basi, ili kuondoa utata huu wa ubinafsi na tamaa ya kuweka kumbukumbu, ni vema kila mmoja wetu akatenda kadri ya anavyopaswa kutenda. Hakuna sababu ya kutafuta kushindana ikiwa hakuna uhalisia au umuhimu wa mashindano hayo. Na ikiwa ni kweli haijawahi kutendwa au kuwepo kwa jambo fulani; kwa atakayetenda au kusababisha kuwepo kwake, asichukulie kama ufahari bali aone kama ni jukumu au kusudi la uwepo wake duniani kwa nafasi aliyopewa!

Ni afadhali sana kupata watu wengi wanaotenda vizuri au kufanikiwa katika hali fulani; iwe kimasomo, kisiasa, kifamilia, kikazi nk, kwani itasaidia sana kuondoa chuki na ubinafsi!
 
Upvote 0
Back
Top Bottom