Toxic Concotion
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 5,760
- 20,837
Ni upumbavu zaidi kuliko tamaa.Tamaa iwaue tu
Tamaa mbele Mauti nyuma!!Inasikitisha kuwa vijana hawajifunzi kila siku kupelekea kurudia makosa hayo hayo.
Imekuwa mtindo sasa vijana kuwekwa rehani kwa suppliers wa madawa ya kulevya Pakistan na Iran na 'matajiri' kuchukua mzigo kwa mali kauli.
Mwisho wa siku waliowekwa rehani wanatalekezwa, waliochukua mali maisha yao yanaendelea kwa raha uraiani.
Kuna haja serikali ikawa strict zaidi hasa kwa hao wanaoweka wenzao rehani na kuwatelekeza. Wakigundulikana wachukuliwe kama wauaji tu.
View attachment 2482381
View attachment 2482382
Chacha na da fatuma wamekunja mtonyo wao hawana habari ya ng'ombe zao walizoweka rehani.Dah! Utu unauzwa kienyeji sana.
Huyu chacha akafirwe mbele
Kuna tamaa na roho mbaya. Hao kina chacha ni makatili kuuza utu wa wenzao.Mimi Nina tamaa sana lakini siwezi kenge yeyote yule labda Mimi ndo nmweke rehani
Hayo ni mateso ya kujitakia.Daah! Wanaume mmeumbiwa mateso ila sio kama haya.
Hakika Mkuu.Hayo ni mateso ya kujitakia.
Ukute walitamani maisha ya wauza unga wakaaminishwa kuwa wakiwekwa rehani na wao watakuwa ma don kutokujua ma don wanatajirika kupitia majuha kama wao.Hakika Mkuu.
Waliweka tamaa mbele.
Na hamna kingine hapo Mkuu zaidi ya hilo kujua wakitoka hapo na wao wametusua.Ukute walitamani maisha ya wauza unga wakaaminishwa kuwa wakiwekwa rehani na wao watakuwa ma don kutokujua ma don wanatajirika kupitia majuha kama wao.
Leo wananing'inizwa kama mbuzi machinjioni na pengine wakiachiwa wasipewe hata mia.
Kuna wengine sio hata wa kuonewa huruma. Ugumu wa maisha sio sababu ya kuwa mpumbavu. Hao ni wajinga wa mwisho kukubali kufanywa bidhaa na wenzao.so sad, Nawaombea wachomoke. yawezekana chanzo ikawa hali ya kimaisha imewafanya kuwa mapunda wa watu
Hilo la malezi ndio la muhimu.Hi vita ni nzito tofauti na tunavyodhani.
Mtandao wa wauzaji ni mkubwa sana na unanguvu kubwa pia wengi wanashawishika na malipo wanayoahidiwa. Tuwalee watoto wetu katika njia ya kumhofia mwenyezi Mungu