Jacob Mulikuza
Member
- Jul 15, 2021
- 16
- 61
Mwenendo wa mwanadamu katika maisha huchangiwa kwa asilima mia moja na mchango wa tamaduni, kwani hakuna mwanadamu asiyetokana na utamaduni fulani. Utamaduni unatofautina kutoka kwenye bara moja na lingine, nchi moja na nyingine na sehemu moja na nyingine katika nchi husika. Hivyo tamaduni hufanana na kutofautiana kwa namna tofauti sana kutokana na sehemu mtu alipo.
Tafsiri ya tamaduni ni pana sana ila kwa maana yangu ni mambo yote yaliyokubaliwa na jamii husika kutoa muongozo wa mienendo ya mambo yote mazuri na mabaya na pia ni kanuni ambazo zimekubalika kuadhibu endapo mambo kubaliwa hayakutendwa ipasavyo.
Zaidi ya yote, ni muhimu kufahamu ya kuwa tamaduni zinazaliwa kila mara kwenye jamii ndogo ndogo zetu na sio lazima tamaduni iwe ama ifikiriwe kama ndo makabila yetu kwani wengi wetu tunachanganya tamaduni na kabila. Ni muhimu kufahamu kuwa tamaduni ni zao la kabila au mkusanyiko wa watu husikia. Kwa uelewa zaidi, endapo kabila la wamasai wakiwa sehemu moja kwa pamoja wataweka tamaduni zao na kuzifuata. Ila wakiwa wamasai, wasukuma na wakurya kwenye sehemu moja kwa mchanganyiko wao huo watakuwa na tamaduni yao kwa makubaliano yao kwa wakati waliokaa pamoja ili hali kila mmoja wao kutoka kwao watakuwa na tamaduni zao waliokuzwa nazo.
Katika makuzi yetu mbalimbali ni wazi mwanamke amepewa nafasi ndogo sana kama sehemu muhimu ya maisha ya mwanadamu kwani mwanamke amekuwa akionekana kufanya mambo kama binadamu dhaifu and asiye na uwezo kamili.
Malezi mengi yemeonyesha nguvu kubwa inawekezwa katika mtoto wa kiume na nguvu ndogo kwa mtoto wa kike na hata ikitokea kwa baadhi ya watu, mtoto wa kike anapata fursa sawa na mwanaume jamii inayozunguka inamtafsiri vibaya kwa kiwango kikubwa.
Makabila mengi hususani Afrika ambako kuna makabila tofauti tofauti mtoto wa kike anafundiswha kufanya mambo tofauti kilingana na maumbile ya kibayolojia kama vile kuwa mama kwa mantiki ya kubeba ujauzito na kuwa mke kwani kwa maumbile ya mwanamke ni lazima tafanya haya. Ila makabila yetu mengi huwenda mbali zaidi na kutafsiri na kukubaliana, hapa ndipo utamaduni unapoingia na kumtafsiri mtoto wa kike kama yule ambaye hawezi kufanya kazi za nguvu, hawezi kushindana na mwanaume, hawezi kusoma kama mwanaume, hawezi kusoma masomo ya sayasi, hawezi kuwa kiongozi na kadhalika. Tukumbuke makatazo haya ya tamaduni hayana mahusiano kabisa na maumbile ya kibayolojia ya mwanamke bali hayo ni mtizamo tu.
Ni kwa mantiki hii ya ukuaji wetu uliochangiwa na tamaduni zetu tumekubali na kusadiki kuwa mwanamke hawezi kufanya mambo mengi kama mwanaume na ama hawezi kushindana na mwanaume kwa kisingizio kuwa ni mwanamke lakini hayana ukweli kutokana na maumbilie ya kibayolojia. Kwa msisitizo zaidi, ukingo wa mwanamke ni wa kibayolojia na sio zaidi ya hapo, kwa mantiki ya kwamba mwanamke ndio pekee mwenye uwezo wa kupata mimba na kuwa mke zaidi ya hapo hakuna kikomo zaidi ya hapo kwani uwezo wake ni sawa ama zaidi ya ule wa mwanaume.
Tunavyofanya mijadala ya usawa ama kumkomboa mwanamke ni muhimu tukazingatia ukweli husika na kupindua uongo uliojengeka katika tamaduni zetu. Na hili sio kwa Afrika tu, hata kwa Ulaya na Marekani kwenyewe ambapo msukumo huu wa usawa kwa akina mama umeanzia bado wanachangamoto hizi kwa kiasi Fulani inaweza isiwe kwa ukubwa kama ulivyo hapa kwetu lakini bado kuna changamoto kwenye kuamini uwezo wa wanawake katika uongozi, ujuzi na kufanya maamuzi.
Mfumo dume kama zao kuu la tamaduni unazidi kuchanua kila siku badala ya kudidimia, kusadiki hili tizama mazungumzo yetu tunayofanya kila siku nyumbani, kazini, vijiweni ama kwenye jamii utaona vile ambavyo kila mmoja wetu anaendeleza mfumo dume huu kwa kuwaona wanawake kama viumbe dhaifu wasio na uwezo na mbaya zaidi mpaka baadhi ya wanawake wenyewe wameamini kuwa dhaifu.
Hivyo ningependa kusisitiza ya kuwa ukandamizaji wa wanawake sio ajali kwani ni makubaliano ya jamii yaliofanywa na sehemu ya tamaduni zetu na kama ni kuondoa tatizo hii ni kurejea kwenye tamaduni zetu na kuanza kurekebisha mambo haya taratibu na kuwa na mtizamo mpya ambao ni chanya kwa wanawake na kuwa sehemu muhimu ya dunia hii sawa na wanadamu wengine.
Kwa kuhitimisha, mashirika, makundi ama serikali kwa ujumla tunapohangaika kumkomboa mwanamke tuanzie kwenye chanzo cha tatizo hasa katika maana ya mwanamke na majukumu yake kwenye jamii na mchango alionao kama mwanadamu na sio mwanamke na hapa ndipo suluhisho litakapopatikana. Kama tunatumia nguvu nyingi kumkomboa mwanamke kwa kumpa fursa lukuki za kumfanya kuwa sawa na mwanaume lakini bado hatuoni chanzo cha tatizo kunauwezekano mkubwa tusifanikiwe kwa kiwango kikubwa.

Upvote
2