Tamaduni Music tatizo lao ni nini?

Kujua wanajua, hatukatai na ninapenda uandishi wao..ila inabidi waanze kufanya vitu serious....wanaishi kwa shida hawa jamaa...nikki nilikuwa naishi nae mtaa mmoja pale kinondoni manyanya, kiukweli jamaa alikuwa ana njaa though ana kipaji sana kuliko wasanii wa hip hop almost ote...penye ukweli inabidi tuseme, inabidi waanze kujibrand kama wasanii wa hip hop. Mimi kama shabiki yao nahitaji kuona hip hop yao ikifika mbali zaidi ya east africa.
 
Kama wanataka kuendana na soko la mziki wa sasa...inabidi wabadilike, wasiache uandishi wao ila waboreshe midundo(beats), videos na waache ujuaji wa kijinga.
ndio maana anaitwa tamaduni,wanafata tamaduni za hiphop
Kuwaambia wabadilishe tamaduni kisa soko ni kuharibu tamaduni
 
Wakenya wa wapi hao ilhali wakenya hawaelewi kiswahili cha TZ sijui wanawapenda vp tamaduni. Kupendwa na wakenya hakumaanishi TZ utapendwa pia. Muziki ni zaidi ya kukaza mashairi.
Inamaana wakenya wanasema hawa jamaa ni wakwao au........
 
Tungo zangu kifungo na funzo kwa wapumbavu
nguzo zangu za tungo ni funzo kwa tungo kavu
Matunzo ya zangu tungo ni gumzo ndo mana mkavu..twendeeeeee!!!!!

Snitch akiniboa namchojoa nampa mbata
namkoboa namzodoa nampa doa nampa chata
Nikikohoa roho inapoa inatakata
Moko poa niko safi niko haswa

Mi ndo One the Incredible
 
uzuri wao wote wana elimu kichwani na nadhani hawafanyi mziki kwa maslahi kiivile!! moja ya ngoma yao ni implecable wamechana kwa lugha ya malkia mwanzo mwisho na one the incredible ana lafudhi safi kabisa ya kimombo
 
Nawakubali sana hawa jamaa..
Wanafanya aina flani ya hip hop kali sana.. fid q kupitia cheusidawa ent. Alijitahidi sana juwatambulisa sema ndo vle wabongo wengi hawakuwaelewa..
Kazi wanaijua na wameshajenga misingi, wanachotakiwa ni namna ya kujibrand vizuri ili wauzike..
watafika sana mbali..
Nawaelewa sana coz huwa nahudhuria kilinge msasani..
' unga waya kwenye spika, kisha weka faya kwenye riffa ntaftie mal**ya sinyorita, mguu mdogo ntakupwaya kama snika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…