Tamaduni Music tatizo lao ni nini?

Daah siku hizi pia nakosa muda wa kuwasikiliza

Kuna mpya ya one nimeipata juzi bado anafanya poa sana!
Ipi hiyo?..Sijasikia kazi yake mpya kitambo..Nimemuona tu kwenye project kama mbili hivi za featuring hapa karibuni
 
Ipi hiyo?..Sijasikia kazi yake mpya kitambo..Nimemuona tu kwenye project kama mbili hivi za featuring hapa karibuni
Nimejaribu upload hapa naona ni kubwa kidogo mkuu

Ila youtube ipo pia inaitwa "adoado mixer one ft jaco beat" nimeipata week kadhaa nahisi sio ya muda sana
 
Hii ndo feedback

nakupa report kwa big track,

Jifiche kwa OPP, kote na big mac,
Haikwepeki risasi, kasi ya mota kusota kwa nafsi basi kisasi kiasi inatosha,

Kaa na mavi unuke au marashi unikie,

Kazi kuwa star, wazi we ni trash kwangu mie,

Plus umeshabugi, makali dugi sio queen lady,

Sina penzi kwa mala.ya ndo ubaya wa slim shed,

Lango la jiji.. washamba..wajanja wanazama,

Mama kama bibi mbona umezama kwa kujua drama,

Am so sorry kwangu huna story, shawry umebuma,

Umegeuka tolori, huendi mpaka ushikwe nyuma,

# feedback by nikki mbishi

Tamaduni boresheni muziki wenu, mtafika mbali zaidi...
 
Nikki nomaa pia sana

Kuna mtoto anaitwa Ghetto Ambasador pia ana vimaneno flan vya kiswahili kama malenga wapya
 
Huo mziki wanaoimba ni #oldskulHipHop. Kwa dunia ya sasa soko hauna. Mcheki Ngosha na walk it off. Hip Pop laini
 
Uko sawa mkuu nimeona bandiko lake youtube ni Nov 2015 mihangaiko tu mpaka nachelewa kuwapata vijana wangu...
Hahaha, hawa jamaa hususani nikki, one, zaiid nawaelewa sana kuanzia flow, uandishi na kila kitu...they know how to stick on the beats though beats zingine wanazingua.
 
Bashiri unavyoweza, au beza inapostahili
Au tabiri kama pweza, jeneza linamsubiri
Na eneza mashairi mithili ya injili ya ebeneza
Kiswahili, kiingereza nacheza mahiri naweza
Nawapa somo wana, bila kikomo nachana
Media zinabana promo, na mdomo bado umeachama
Katuni tupa kapuni, na kupa kanuni
Supa kapuka hazivumi, shtuka, zinduka na utamaduni
Mbishi ni oversize, nivae nikuvuke
We ni mayonnaise kwenye mkate, ngoja uchakae baadae wakutupe
Ndani ya kilinge nitinge, chui ni vimbe
We hujui mbinde, Msondo huijui ngoma ya sikinde
Na survive na vibe za live bendi
Mi na mengi ya ku-describe, sio pride ya ku-drive range
Hii ni wazi, nina hadhi ya wako role model
Na sio stori ndogo, ka una maradhi twende loliondo
We ni James Bond toy, mi ni James Bond mtu
Wanarespond, lecture ka za Desmond Tutu
Siyo choo cha kike, hiki ni choo cha mashoga
Sina uoga napo flow, na hii siyo show ya mapouka
 
Tamaduni Music, Maybach Music
Since way back mi naplay track 'move bitch'
Njiwa ana makinda, Spika Anna Makinda
Na yeye bado ni spika so anasikika
anapoimba
Pedeshee Ndama, mtoto wa ng'ombe
ndama
Mpaka napagawa kwa drama za hivi zama
Upepo ni kimbunga, mchawi ni kimbunga
Oyah nakupungia jamaa na wewe punga
Nash MC, P the MC wapo kwenye joint na
ipi game hii
Ukienda beach Coco, hata Cherie coco
Kuna internation na pia kuna local
Kung fu Master, shule headmaster
Ukutani plasta, na kidonda plasta
P ni majani, chai ni majani
Wanyama na mimea ndio maana
hawafanani
 
Nikki Mbishi - Yote Sawa lyrics
[Intro]
Yeah! Noma Records
Kalulete..Tamaduni Music Forever
Unajua nini..
Rutuba kweli iko kitandani ndo maana
ukilala unaota
Yote sawa! (Zohan)
Tena ndoto nyingi mpaka zilizoloa sio
Ahh!
[Verse 1]
Tamaduni Music, Maybach Music
Since way back mi naplay track 'move bitch'
Njiwa ana makinda, Spika Anna Makinda
Na yeye bado ni spika so anasikika
anapoimba
Pedeshee Ndama, mtoto wa ng'ombe
ndama
Mpaka napagawa kwa drama za hivi zama
Upepo ni kimbunga, mchawi ni kimbunga
Oyah nakupungia jamaa na wewe punga
Nash MC, P the MC wapo kwenye joint na
ipi game hii
Ukienda beach Coco, hata Cherie coco
Kuna internation na pia kuna local
Kung fu Master, shule headmaster
Ukutani plasta, na kidonda plasta
P ni majani, chai ni majani
Wanyama na mimea ndio maana
hawafanani
[Hook]
Yoh mistari nachana, akili nywele nachana
Haina kubishana bwana yote sawa
Sauti zinafana, vina vinafanana
Ujuzi unaonekana bwana yote sawa
Mistari nachana, akili nywele nachana
Haina kubishana bwana yote sawa
Sauti zinafana, vina vinafanana
Ujuzi unaonekana bwana yote sawa
[Verse 2]
Wasanii wanasanda, maiti wana sanda
Wote wanashuka na wengine wanapanda
FM stereo, Bboy Stereo
Wanategemeana wakikutana scenerio
Tyson Mike, microphone mic
Mmoja bondia mwingine kipaza...right?
Mtutu bunduki, midundo bunduki
Nyundo juu ya nyundo mafumbo lundo la
chuki
Ukionewa kibonde, Ephraim Kibonde
Bora kuwa mbabe kuliko kuishi kinyonge
Mapangala Samba, Brazil samba
Mbishi anatamba na Sultan Tamba
Kutonya mtonyo, pesa mtonyo
Kusonya misonyo, pia waziri Sonyo
Wa uhuru mwenge, stendi ya mabasi
Mwenge
Mwenge mulika stendi ya mwenge wezi
wajichenge
[Hook]
Yoh mistari nachana, akili nywele nachana
Haina kubishana bwana yote sawa
Sauti zinafana, vina vinafanana
Ujuzi unaonekana bwana yote sawa
Mistari nachana, akili nywele nachana
Haina kubishana bwana yote sawa
Sauti zinafana, vina vinafanana
Ujuzi unaonekana bwana yote sawa
[Verse 3]
Eyoh! Mayweather boxer, nguo ya ndani
boxer
Kweli nabaki hoi kama cocacola poster
Jakaya Mrisho, Mpoto Mrisho
Ngasa Mrisho, mpaka Feruz Mrisho
Bomoa bomoa X, hata samaya X
Picha za ngono X, hata mpenzi wa zamani
ex
Kigamboni Tungi, nikiwapombe tungi
Naongea peke yangu inatoka sauti ya kundi
(aah achana na mimi)
Francis Cheka, bibi wa Temeke Cheka
Staili ni mateke, mapanga, makwanja fyeka
'You Dont Mess With The Zohan', Nikki
Mbishi Zohan
Kila nikirusha track mitaani nabaki
slogan..yeah
Malcom is like, "Hi dad! Sitaki pipi nataka
uniletee iPad"
Mzazi nadata nabaki, "My God! Nipe nguvu
za Bruce Willis ili ni'Die Hard'"
[Outro]
Eeh! Mkuki kwa uchungu kwa binadamu
nguruwe
Zohan
 
Hii naielewa sana, utamaduni by mbishi...
 
Wako vizur sana sema wanakosa management ya huakika kutoa video kali kama wakina Joh Makini ama weusi....
 
moko
Habari noko/Nina habari moko
Huwezi timiza kazi kama askar choko
Juu ya daftar ninatafakar msoto
Kwa mistar mitamu kawa cariban coco
Mi ni classic na move kama dancE
Nawapa hisia kali zaid ya muvi za mikasi
Kwenye chart zao wao ushndani mm nafasi
Sifanani nao mimi ni zao wao ni nyasi
Mwanaharakatikama kikosi na siasi
Mistari ina siri nzito kama boksi la risasi
Sipo copy npo confident conscious reaction
Kwenye boof niko lost kama part ya duratics
/Geneous nilifeli kupass Mathematics
Kama rap ni drugs mi na Habit kama addicts
Sipiti kama rabbit kwenye 8 mile
Love or hate it hard iki bet hii air tym classic
Verse balanced ka account ya fisadi
Kwako mlevi wa u star ka round za vinywaji
Dunda kavu au bounce na vinywaji
Skia biashara kwenye speaker leta sound ya miradi
Naujumbe mtam kama sound ya kingasti
Snitch hastaround niko down na illematics
Na spiti kwenye mic ka risas nipo kasi
So huwez pass around ka upo stack kwenye trafficks
Aah sibutui nashoot kasi
Tu hujui siku zote vipi unisumbue kilaza
Mdundo mweusi nausugua ka na msasa
Mpaka duke ateme slang kama movie ya kihustler
Hii kwa wote wanaoikubali sio flani na flan waipende
Mi ndo moko makutano ya mistar kama stend ya mwenge
Yafanya wengi waende mbali waache wachache wakae kizembe
Kaa mbali nasi au kaa sawa nikulenge
Sa kaa sawa snitch mi ni dawa ka Giv
Hawa wanadis lakini hawapo sawa kama sisi
Na kama mkavu hapa utanawa utakuwa mbichi
Money ni power respect 2naipata ukijua displine
Kama kiongoz wa dini nampenda mjinga na mtoaji
Mtaani wanga hunihofia kama bingwa wa uponyaji
Linda chako mjinga watu wanawinda hawako safi
Ukizingua unagongwa tako kama mznga wa konyagi
Nampenda haswa anahisi anapenda heshma
Daktar rudia darasa mimi ni ugonjwa usio na jina
Anashangaa dinner mara hawa mara huyu we ni buyu mi ni
moko sawa sawa
 
uno
Beat kali haifai bila vocal
Daily nakula dry, niko high kama popo
Fanya worldwide sio ku try kama local
Fake MC ukijikoki mi na squeeze kama fofo
Ah,
Verse baridi vaa koti
Salamu kwa wanangu wote sina ripoti
Bado mishemishe sapoti mwanangu opi
Kila biti natoboa kama juisi ya kijoti
Ni discipliner nawasimamisha wima
Minya rapper [Mi nyarapa] mpaka sura kama simu ya kichina
Mistari na vina, kwenye shari habari sina
Mchagga halali, macho kwenye salari daima
Zunguka kote hauna rafiki kama noti
Sista duu hauna mnafiki kama shosti
Tafuta deal uza hata pipi we bitoz
Tafuta njia haya maisha hayamuliki kama tochi
Chorus
Chap chap chap chap ni sawa
M-Lab, pure math, rap ni dawa
Chap chap chap chap ni sawa
Pure mathematics (dogo kapagawa)
x2
We unachana mi nachana mpaka basi
Niko booth nina bic, karama na karatasi
Sina hofu, nina speak salama kwa sala safi
Ila ukinivaa vibaya nakuchana kama vazi
Sanaa, gharama haramu chati
Harakati hii kubwa hupaswi simama kati
Verse inacheza Judo, kata na sarakasi
Baba mama mbarikiwe kusimama kaa wazazi
Pure namba, hapa zinajamba za kubuni
Mshamba kawa mjanja, mjanja ana ujanja wa kihuni
Banja kwenye beat weka ladha ya sabuni
We ni base ten log mi ni namba ya kirumi
Hii ni classic, hata isipotamba kama Dumi
Kasi ya ma-rapper ina sanda kama uchumi
Nina punchline na kick kama chuo kikuu cha ngumi
Pure mathematics, sina banda n’na kampuni
So
Chorus
Chap chap chap chap ni sawa
M-Lab, pure math, rap ni dawa
Chap chap chap chap ni sawa
Pure mathematics (dogo kapagawa)
x2
Kuna rapper mwenye akili na rapper batili
Rapper anayepata akisaka na asiyepata akisaka dili
Tofauti kati ya rapper wa kwanza na rapper wa pili
Wa pili anataka u-master huku hajapata umahiri
Fungua ukurasa kwenye darasa la hip-hop
Somo halisi tunaoandika kusikika anataka pomo
Midomo inasikika ikisema na mikono
Inashika makoleo na kuzika waliomo
Waliopotea njia wanataka kurudi nyuma
Wapotovu wamechuna, waovu wamenuna
Inawauma,
Wamepoteza mwelekeo,
Maendeleo yamegota watafanya nini leo?
Panapo matatizo tunataka suluhisho
Likizo inawekwa kando tunakaza mpaka kifo
Na tulivyo, sio watu wa matambiko
Tumeshiteka kambi na kupekua maficho
 
Ujue watu wanaehindwa kuelewa kitu kimoja.... hakuna mtu anayependa maisha magumu katika sehemu yake... music wa tamaduni ni mziki wa ambao ni mgumu na kwa maisha ya kawaida ya watz ni kazi sana kupendwa coz watu wanaouelewa ni wachache na wengi ni wanaume.... tatizo kwetu bongo kitu kikipendwa na waanawake na watoto ndo kinakuwa high zaidi kuliko uhalisia wakee. Tazama music wa wabingo fleva wengi umaarufu wanaupata kutoka wapi! Its from women and children! Lakini linakuja swala la hawa wanaoimba eti zinaitwa ngumu hawana umarufu sana sababu kubwa ni kwamba watu wanaouelewa mziki wao ni wachache na wasiopenda mauzoo!
by that way kipaji na ubunifu wa mtu ni furaha yake na kama weewe haukufurahishi ina maana HAUKUHUSU huo ubunifu so achana nao usiudharau!
mtu asiwadharau TAMADUNI kwa kigezo cha biashara na umaarufu akasahau kuwa kuna kitu ninaitwa falsafa ya fani.
Angalia mziki wa watu wa kongo haubadiliki na bado unawapa pesa nyingi na umaatufu hadi wasanii wengi nje ya kongo wanawafuata kwa ajili ya collabo...
Angalia mziki wa Nigeria na Wanaigeria wenyewe hapa naongelea akina Wizkid,Davido,P-Square,Yemi Alade,Kcee,Flavour na wengine mamia lukuki na style yao ya mziki ni Nigeria Identity! Cha ajabu zaidi sisi hawa hawa tusio na Identity ya kazi zetu tunaiga wanaigeria na hatuwakutii...
Angalia mziki wa Ghana, South Africa na kwingineko mziki wao ni ule ule na unawapa hela nyingi na umaarufu mwingi hadi tuaomba collabo naoo!
Swali langu ni kwamba sisi ni nani?
Mtu utamkuta anang'ang'ana mwanamziki fulani abadilishe style ya uimbaji ili atoke! Hiyo ni kama kumwambia mtu ila afanikiewe aikatae familia yake... ni ujinga!
Ushauri wangu kwa celebrity wafanye vitu bila kuiga ila kwa bidii tuu hata kama group fulani la watu hawatapenda kazi yako kuna watakao ipenda hata kama ni wachache hao ndo watakupa hela na umaarufu... Shika ulicho nacho!
Watanzania tunapenda vitu vya kuiga sana ndo maana tunakosa Identity na vitu vyetu vya kujivunia.... tunakuwa watumwa na wafuata upepo kwenye vitu vya wenzetuu.
Tamaduni wafanye kazi zao kwa bidii tuu na wengine wafanye kazi zao kwa bidii tuu!
We need our Music Identity ili Music wetu ukue zaidi!

#HipHop 4life#
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…