Tamaduni zetu za kisasa kwenye jamii na madhaifu yake

Tamaduni zetu za kisasa kwenye jamii na madhaifu yake

DMmasi

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
561
Reaction score
900
SEHEMU YA KWANZA

Habari zenu wana jamii wenzangu natumai muwazima wa afya, kwa walio na changamoto mbalimbali poleni sana niseme tuu ikiwa tunaishi tumaini lipo tusikate tamaa.

Baada ya salamu ningependa kutoa ufafanuzi mfupi juu ya uzi ninaokwenda kuushusha. Kwanza huu ni mtizamo binafsi kulingana na mambo yanayo tokea katika jamii yetu yaleo katika nyanja mbalimbali.
Nitaongelea matukio kadhaa na mapokeo yake katika jamii.

MALEZI NA UMOJA KATIKA JAMII
Katika jamii ya sasa mahusiano ya kiumoja katika jamii yamepungua, mzazi hulea familia yake mwenyewe siyo rahisi kukuta mzazi mwingine akimwonya mtoto wa mwingine juu ya jambo fulani.

Sababu hakuna aliyetayari kukosana na mwingine sababu ya watoto "naam" huo ndiyo utamaduni wa sasa. Nimarachache pia kuona watoto wakijumuika pamoja kucheza watakutana shuleni watacheza muda wa mapumziko dakika 30 jioni watarudi kwa basi nyumbani mwisho wa wiki ni mafunzo ya dini wakirudi ni televisheni muda wakuchafua nguo hawana tena KWISHA HABARI YAO!!

Ulaji wa vyakula pia ni changamoto sababu ya malezi mtoto hukosa mlo bora
*mamy taki uji ataka sambusa
*mama yuko kwa wazazi wake na mwanae baba wa mtoto yuko kwa wazazi wake anazuga. Mama uvivu wakulea mtoto anamlisha crips na embe juice, biskuti na energy drink
* ugumu wa maisha unafanya tunakula kilichopo hakuna lishe bora
( siumelelewa kijijini wewe hatakama kipato nikidogo shamba halita watupa chini. Basi kuna dada uko mjini kila kitu ananunua hadi umbea unauzwa)

Pesa sabuni ya roho bhana ila tambua ili "Pesa itakupa kitu chochote, ila pesa haitokupa kila kitu"
Sikiliza nikwambie mjomba wazazi wanatafuta pesa wawape watoto wao maisha mazurii, wanachoka hadi wanakosa muda wakukaa na watoto.

Mtoto bega lake lakuegemea muda mwingi ni dada wa kazi au anko na anti uko day care.

Watoto wanakwenda na wakati bhana mtoto hajui watoto wanaangalia nini katika televisheni, watoto wanakaa katikati ya watu wazima. Mtoto kushiriki mambo ya watu wazima imekuwa kawaida.

Nini kifanyike angalau kuinusuru hii hali
1. Ruhusu mwanao akacheze na wenzake
Hii itamsaidia kufungua akili zaidi sababu akifika uko kwa wenzake anakuta mwenzake katengeneza kitu chakuchezea basi nayeye atajifunza pia. Akiweza itamwongezea ujasiri

2. Kuwa karibu na rafiki zaidi kwa mwanao
Itakusaidia kugundua changamoto zinazo mkabili. Tenga muda wakuongea na mwanao siyo unaongea nae na chakula mdomoni

3. Ruhusu mwanao awe mtoto wa jamii nzima
Ukilitewa tuhuma juu yake zipokee na uzifanyie kazi kama mzazi na mwanajamii
4. Mpe mtoto kile kinachohitajika kuendana na uhalisia wake
Usikubali mtoto awe juu yako, siyo kila kitu apate sababu ametaka bali fuata uhalisia(nature)

YANGU KWALEO NI HAYO TUU KARIBUNI KWA NYONGEZA AU HOJA. TUTUMIE LUGHA RAFIKI

UPENDO, AMANI NA MATUMAINI VIWE NGAO KWETU.
 
Back
Top Bottom