Mtawa Leon
New Member
- Aug 26, 2022
- 2
- 5
Kati ya maswali mengi ambayo watu wengi wanaweza wakawa wanajiuliza kila iitwapo leo ni;
Na maswali mengine mengi sana ya namna hii
Kabla ya yote naomba kukumbusha jambo moja kwamba, hatua yoyote ya mafanikio duniani hasa ya kiuchumi, mahusiano, kisiasa hata kielimu huanza na mtu kuwa ‘hamu ya kupata mafanikio hayo'.
Hili ni jambo la muhimu sana na linapaswa liwekwe kichwani bila kupuuzwa. Hii ikimaanisha kwamba, tamanio dhaifu hupelekea matokeo dhaifu. Hivyo basi, mwanzo wowote wa mafanikio yako, katika nyanja zote, huanzia pale tu unapoamua kwamba unahitaji kuwa na mafanikio ya kiwango fulani.
Kuwa na Hamu ya mafanikio ndiyo hatua ya kwanza ya kufanikiwa lakini, huambatana na UVUMILIVU na KUENDELEA BILA KUKATA TAMAA. Vitu hivi hutengeneza muunganiko wenye nguvu kufikia malengo yoyote binafsi.
Ushindi kwa mtu yeyote siku zote, unapatikana pale tu, mtu huyo “atakataa kuacha kupigania kile anachokiamini na kutamani kitokee kwenye maisha yake.”
HAKUNA kushindwa, kwa mtu yeyote aliyekataa kukata tamaa, japo mafanikio yanaweza kuchelewa kwa muda mfupi tu, kitu cha kuzingatia ni kuwa na imani kwamba mafanikio ya aina yoyote yale yapo njiani na yatafika muda wowote ule.
Nguvu na ukuaji huja tu kupitia juhudi na mapambano endelevu.
Dhiki, kushindwa, na magumu mengine anayopitia mtu, yamebeba "mbegu" ya mafanikio makubwa sana mbele yake. Karibu watu wote waliofanikiwa kimaisha, wamekuwa mashahidi wa kupitia madhira haya hapo kabla, habari njema ni kwamba waliweza kuvuka kipindi hicho cha mpito.
Hakuna anayetamani kukutana na shida wala changamoto, na hawatakiwi kupitia haya yote, lakini ukweli ni kwamba kwenye changamoto nyingi na maumivu ndipo kwenye fursa zaidi. Na mtu yeyote anayekata tamaa kupigania kile anacho anakitamani maishani mwake, basi mtu huyo AMECHAGUA KUFELI. Anaweza akawa hataki kuteseka kupitia vipingamizi na vizuizi, au kuishi na aibu ya kushindwa jambo flani, lakini ni hakika kwamba ataishi na kitu kibaya zaidi ya vyote hivyo, nacho ni MAJUTO.
Jambo la msingi la kuzingatia hapa ni kwamba, kama mtu atakataa kukata tamaa na kuendelea kupambana, basi kitu kimoja cha uhakika ni, sio kwamba atafikia ndoto zake tu, lakini pia atapata kitu cha thamani sana ambacho ni ‘ujivuni’ kwa kujivunia mafanikio yake yaliyotokana na jasho lake.
Je, unawezaje kujua maisha yako hasa ya kiuchumi, yatakuwaje baadae?
Jaribu kujitathmini kupitia shughuli zako za kila siku, namna unavyotumia pesa unayoipata, au unavyotumia muda wako wa ziada. Mambo haya huwa kama viashiria muhimu sana kujua kesho yako. Kama mienendo yako inakujenga kufanikisha malengo yako, basi bila shaka, lazima utatimiza malengo hayo.
Lazima uwe na kusudi la namna unavyotumia pesa yako na muhimu zaidi muda wako. Tengeneza mpango wa kila siku, ambao utakufanya uzidi kusogelea malengo yako uliyojiwekea. Kumbuka ndoto lazima uiwekee ukomo, nikimaanisha hii ni kumaanisha kwamba lazima uweke mipango yenye ukomo. Mfamo; orodhesha mipango ya malengo yako mpaka ifikapo Januari mwaka 2025 (inaweza ikawa zaidi au chini ya hapo, kulingana na malengo yako). Hii itakusaidia kujua ni kiasi gani cha nguvu utakiwekeza ili kukamilisha malengo yako uliyojiwekea.
Nikukumbushe kwamba, kuwa na malengo ni jambo la muhimu sana, lakini malengo yasiokuwa na mipango wala ukomo, hubaki kuwa matamanio hewa tu. Ndoto zinaweza kutimia kama utakuwanazo makini. Na hatua ya kwanza ya kuwa makini na malengo yako, ni kupangilia ukomo wa muda unaotaka kufanikisha lengo hilo.
Lengo lako lisipotimia kwa muda ulioupanga, chukulia kama kiashiria kwamba mipango uliyoipanga ilikuwa na kasoro kadhaa. Haitakiwi kukata tamaa, bali pitia upya mipango uliyoweka mwanzo, anza kupanga tena, mara hii kwa kugawanya gawanya malengo yako kwenye makundi madogo madogo yatakayokuwezesha kufikia malengo makuu kirahisi.
Ikumbukwe kwamba, Mtu yeyote anaweza kushindwa kufikia malengo yake aliyojiwekea kwa mara yake ya kwanza, na wengi wao hukata tamaa, usiwe kama wengi wao. Jaribu kutumia kushindwa kwako kama chachu ya kuanza upya na kurekebisha makosa. Kupitia kitabu chake cha "Think and Grow Rich, Napoleon Hill" anabainisha kwamba, “Chochote ambacho mtu anaweza kukiwaza na kukiamini, basi bila shaka anaweza kukipata”.
Tafuta watu Sahihi wa kuambatana nao
Epuka kuamini maneno ya walioshindwa na kukata tamaa, wakitaka kukukatisha tamaa pia, haijalishi ukaribu wako kwao. Kama malengo yako hayajawahi kufikiwa na mtu yeyote kati ya hao basi amini kwamba wewe unaweza ukawa wa kwanza kuyafikia. Mawazo yako na imani yako juu ya mawazo hayo ni mtaji mkubwa sana katika kufikia malengo yako.
Kama unahitaji maisha mazuri, kuwa na mwili wenye mvuto, au kuwa kwenye mahusiano yenye afya basi uwamuzi ni wa kwako mwenyewe. Serikali itakutoza kodi na tozo kwenye vitu vyote lakini haiwezi kukutoza kodi na tozo kwa wazo lako. Hilo ni mali yako, na ni juu yako kulifanya wazo hilo liwe na uhalisia, haijalishi wazo hilo ni kubwa kiasi gani.
Tafuta watu sahihi kwenye harakati zako wakusaidie kutimiza malengo yako. Watu wenye mtazamo chanya, ambao wapo tayari kuwekeza kwenye wazo lako kiushauri hata kifedha. Tafuta marafiki au watu ambao wamefanikiwa kupitia wazo kama hilo ulilonalo kichwani. Waulize maswali muhimu, kama; wamewezaje kufika hapo walipofika?, changamoto gani wamezipitia? Namna ya kizikabili changamoto walizozipitia.
Jishushe na kuwa tayari kujifunza kitu kipya kila kukicha. Tafuta maarifa mapya kupitia vitabu, na machapisho kadha wa kadha yanayoelezea wazo kama lako kutoka wa watu waliofanikiwa. Maarifa yatakusaidia kuimarisha kesho yako au yatakuonesha njia ya kufikia malengo yako.
Anza kufanya sasa, kamwe usisubiri kuanza kesho, muda si rafiki wa mtu yoyote yule, useme utakusubiri.
Anzaia hapo hapo ulipo, tumia vifaa hivyohivyo ulivyonavyo hivi sasa hata kama ni vidogo au vimechakaa, kwa maana vifaa vikubwa na vizuri utavikuta mbele.
View attachment 2342643
- Je ni nini siri ya kupata kile unachokitamani ikiwa hauna uwezo wa kipata?
- Je ni kweli kwamba kuna watu wamezaliwa na nyota zao za bahati zinazowawezesha kupata chochote wanachokitaka bila hata kuhangaika?
- Kwanini mimi sifanikiwi kwa kila jambo ninalolifanya au ninalolitaka?
- Nifanye nini ili nifanikiwe?
- Ni nini sababu ya kuwepo kwa utofauti mkubwa wa maisha na mafanikio ya kiuchumi kati yangu na jirani yangu, wakati wote tunajishughulisha na shughuli sawa?

Upvote
3