Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Tiketi za tamasha la Chris Brown ‘Breezy in South Africa’ katika Uwanja wa FNB, Johannesburg, zimeuzwa zote, huku tukio hilo kubwa likitarajiwa kufanyika tarehe 14 Desemba. Hili ni moja ya matukio yanayosubiriwa kwa hamu, ambapo mashabiki wamenunua tiketi kuanzia shilingi 94,000 hadi 800,000.
Tamasha linakuja wakati ambapo kuna maswali kuhusu maisha ya msanii huyu maarufu. Taarifa zinasema kuwa kutakuwa na documentary inayopangwa kuonyeshwa kwenye Investigation Discovery, ikiangazia matukio ya kikatili yanayohusishwa na Chris Brown.
Kwa muda mrefu, amekuwa kwenye kizungumkuti cha madai mbalimbali, baadhi amekiri na kuomba msamaha, huku mengine akiyakanusha bila ushahidi wa kutosha, lakini yote haya yameibua mijadala kuhusu tabia zake na maisha yake binafsi.
Kwa mashabiki wa Chris Brown nchini Afrika Kusini, tamasha hili linatoa fursa ya kipekee ya kumshuhudia staa huyu wa R&B akifanya onyesho live, licha ya changamoto za kisheria zinazomwandama.