tamasha la fiesta

tamasha la fiesta

Mkuu C.T.U naona umemkumbuka mzee wa Danza Kuduro. Kiuhalisia ni kweli kabisa ili kuweza kuwalipa wasanii wa nje, Fiesta huchukua wasanii ambao hawako kwenye chati.Hao wenyewe tu waliochuja wanachaji pesa mingi mpaka basi sembuse kumleta Don Omar?.
 

drake yuko juu kwa sasa kuliko luda hilo halina ubishi marekani si sawa na bongo marekani mtu akiwa ana hit kwa sasa sio wa kumshika kwa kweli ngoja nikupe mfano mdogo ludacris ana charge usd 75,000 per verse ukitaka kumshirikisha wakati juzi niliona twitter ya kanye west anasema ukitaka kumshirikisha 2-chainz ni usd 100,000 per verse wkati ya luda na 2 chainz nani msanii mkubwa ? Iweje 2 chainz achaji more kuliko luda?? JIULIZE? Unakumbuka ugomvi wa piers morgan na madonna ni kuwa piers morgan alikataa kumualika madonna kwenye kipindi chake akiogopa kuwa hatapata watazamaji kwanini piers morgan alisema "we have lady gaga now" ?? JIULIZE tusishabikie vitu tusivyovijua ila ukweli ndio huo waendelee kumleta shaggy u.s.a unafikiri nani anataka kumsikiliza shaggy? wanakwambia we have don omar now hawana hela ya kumleta don omar, fabolous ana nyimbo gani ya hit?? Mdau aliyesema kuwa billboard sio inshu namshauri aendelee kusikiliza bongo flava asiongee vitu usivyovijua matokeo yake unaongea pumba mbele ya hadhira

Umemaliza kila kitu, wapi kitufe cha like nikugongee! Aah kumbe natumia simu

Huwezi mlipa sawa Afande Sele na ROMA katika show hivi sasa!

Ludacris wa st. Lunatics sio wa sasa, kafulia tu hana jipya!

Hawana ubavu wa kumchukua msanii anayehit kwa sasa, maana CLOUDs wenyewe wanataka faida tu
 
thread inasema kushuka kwa chati ya fiesta, hilo halina ubishi kwani sasa hivi wameanzisha na bahati nasibu ya shinda gari....!
 
thread inasema kushuka kwa chati ya fiesta, hilo halina ubishi kwani sasa hivi wameanzisha na bahati nasibu ya shinda gari....!

Diamond alisema hapigi show bila 10m.Hao wengine wanadai bei gani? Mwisho itakufa ukizingatia ant virus ya Sugu heh heh
 
naona kila mwaka linazidi kupungua umaarufu wake mwaka huu sijui watamleta superstar gani wa ulaya aliyefulia

mkuu sina kumbukumbu kama kuna tamasha la fiesta walishamleta hata mmoja wa superstar kutoka bara la ulaya mwenye kumbukumbu anijuze.
 
mkuu sina kumbukumbu kama kuna tamasha la fiesta walishamleta hata mmoja wa superstar kutoka bara la ulaya mwenye kumbukumbu anijuze.
Marekani nayo ni Ulaya Mkuu, hapa halizungumziwi bara. ni sawa na wachaga wote tunaambiwa wanatoka Moshi kumbe wapo wa Hai na Wilaya nyingine.
 
Marekani nayo ni Ulaya Mkuu, hapa halizungumziwi bara. ni sawa na wachaga wote tunaambiwa wanatoka Moshi kumbe wapo wa Hai na Wilaya nyingine.

Hahaha! Waswahili zaidi ya uwajuavyo.Yaani mswahili huwa hakosi sababu. Kuanzia handsome boy wa Magogoni mpaka Nyangema wa soko-Matola Mbeya.
 
Back
Top Bottom