tamasha la fiesta

Mkuu C.T.U naona umemkumbuka mzee wa Danza Kuduro. Kiuhalisia ni kweli kabisa ili kuweza kuwalipa wasanii wa nje, Fiesta huchukua wasanii ambao hawako kwenye chati.Hao wenyewe tu waliochuja wanachaji pesa mingi mpaka basi sembuse kumleta Don Omar?.
 
Umemaliza kila kitu, wapi kitufe cha like nikugongee! Aah kumbe natumia simu

Huwezi mlipa sawa Afande Sele na ROMA katika show hivi sasa!

Ludacris wa st. Lunatics sio wa sasa, kafulia tu hana jipya!

Hawana ubavu wa kumchukua msanii anayehit kwa sasa, maana CLOUDs wenyewe wanataka faida tu
 
thread inasema kushuka kwa chati ya fiesta, hilo halina ubishi kwani sasa hivi wameanzisha na bahati nasibu ya shinda gari....!
 
thread inasema kushuka kwa chati ya fiesta, hilo halina ubishi kwani sasa hivi wameanzisha na bahati nasibu ya shinda gari....!

Diamond alisema hapigi show bila 10m.Hao wengine wanadai bei gani? Mwisho itakufa ukizingatia ant virus ya Sugu heh heh
 
naona kila mwaka linazidi kupungua umaarufu wake mwaka huu sijui watamleta superstar gani wa ulaya aliyefulia

mkuu sina kumbukumbu kama kuna tamasha la fiesta walishamleta hata mmoja wa superstar kutoka bara la ulaya mwenye kumbukumbu anijuze.
 
mkuu sina kumbukumbu kama kuna tamasha la fiesta walishamleta hata mmoja wa superstar kutoka bara la ulaya mwenye kumbukumbu anijuze.
Marekani nayo ni Ulaya Mkuu, hapa halizungumziwi bara. ni sawa na wachaga wote tunaambiwa wanatoka Moshi kumbe wapo wa Hai na Wilaya nyingine.
 
Marekani nayo ni Ulaya Mkuu, hapa halizungumziwi bara. ni sawa na wachaga wote tunaambiwa wanatoka Moshi kumbe wapo wa Hai na Wilaya nyingine.

Hahaha! Waswahili zaidi ya uwajuavyo.Yaani mswahili huwa hakosi sababu. Kuanzia handsome boy wa Magogoni mpaka Nyangema wa soko-Matola Mbeya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…