Tarehe 28 Januari ni mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China. Kama ilivyo desturi, saa 2 kamili usiku kwa saa za Beijing, tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China ambalo linaandaliwa na Shirika kuu la utangazaji la China CMG linalojulikana kama “Chunwan” linarushwa hewani kwa ajili ya watazamaji wa kote duniani, ambapo vyombo vya habari karibu elfu tatu kutoka nchi na sehemu zaidi ya 200 vinatangaza moja kwa moja au kuripoti kuhusu tamasha hilo.
Mwaka mpya wa jadi wa China ni moja ya sikukuu muhimu zaidi za jadi za taifa la China, ikijumuisha maana za kitamaduni za familia kujumuika, utulivu wa taifa na watu, na masikilizano kati ya binadamu na mazingira ya asili, na pia ina mizizi ya kihistoria. Mwishoni mwa mwaka jana, sikukuu hiyo iliorodheshwa kama urithi wa utamaduni wa binadamu usioshikika. Ili kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China wa kwanza ambao sasa ni 'urithi wa utamaduni usioshikika', tamasha la mwaka mpya wa jadi wa China wa CMG limeandaa vipindi vya aina mbalimbali vikihusisha nyimbo, ngoma, opera na Wushu, na pia watu wa kawaida kutoka sekta mbalimbali pia wamealikwa kuwa wahusika wakuu katika maonesho. Tamasha hilo la mwaka huu kwa mara ya kwanza limetoa matangazo ya matoleo maalum kwa ajili ya watu wasioona na watu wasiosikia, na kutumia mafanikio ya uvumbuzi lililopata Shirika Kuu la Utangazjai la China CMG ya teknolojia za "5G+4K/8K+Akili Bandia AI", na kutoa “chakula cha jioni cha kitamaduni” kwa watazamaji wa kote duniani kwa lugha 82.
Tangu mwaka 1983, kila ifikapo mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China, Televisheni ya Taifa ya China hufanya tamasha linalojumuisha maonesho ya aina mbalimbali ya kitamaduni. Katika miaka 42 iliyopita, kutazama tamasha hilo kumekuwa desturi mpya ya mwaka mpya wa jadi wa China baada ya kubandika karatasi za baraka, kutengeneza Jiaozi, na wanafamilia kujumuika mpaka siku ya kwanza ya sikukuu na kutoa heshima kwa mababu. Tamasha hilo linabeba hisia za kupenda nyumbani na taifa walizo nazo Wachina wote duniani, kuonyesha mvuto wa kipekee wa utamaduni wa China, na kuwa kipindi cha televisheni kinachotazamwa na watu wengi zaidi duniani wanaposherehekea ujio wa mwaka mpya.