Tamasha la leo 8.Aug.2026 Simba inahujumiwa kwenye Azam Tv

Hebu tutajie orodha ya wote walio hojiwa ili tuone kama kweli ilikuwa ni hujuma au lengo lilikuwa ni zuri, isipokuwa wewe mtazamo wako ndiyo uko tofauti na wa hao Azam.
 
Huyu kanji huyu dahhh
Majigambo meengi lakini sioni mikakati ya kushinda makombe

Anasema ataleta makocha watano wa Kijerumani watembee pote Tanzani waibue vipaji vya vijana

Hilo ni jambo zuri hatukatai, lakini kushinda makombe hasa ya Afrika kwa sasa watuletee wachezaji angalau watatu wengine wenye viwango vya juu ili timu iwe na uwiano na kuweza kushindana na mabingwa wengine wa Afrika

Tunaona timu inazidi kushuka katika viwango vya timu bora Afrika. Sote tumeshuhudia ubutu wa safu yetu ya ushambuliaji tangia kwenye michuano ya Kagame

Wafanye usajili wa maana, timu ipate matokeo mazuri uwanjani, ibebe makombe hapo hata biashara za hao wadhamini zitafanikiwa
 
Kwani Azam Day ni lini inafanyika?
 
Usajili wao haukulenga kuziba mapungu yaliyokuwepo, sikuona sababu ya kusajili einga wakati tulikuwa nao wa kutosha huku tatizo kubwa lilikuwa mshambuliaji wa kati.
 
Mudi ni mwanasiasa..
 
Usajili wao haukulenga kuziba mapungu yaliyokuwepo, sikuona sababu ya kusajili einga wakati tulikuwa nao wa kutosha huku tatizo kubwa lilikuwa mshambuliaji wa kati.
Nafikiri lengo ni kumtoa Mpanzu kabisa kutoka winga kuwa centre forward. Nafikiri lakini.
 
Ndugu, mashabiki walishachoka na janja zao, kilichobaki ni kutokwenda uwanjani, tunaelekea huko,
Sisi wenye roho ndogo tushanyoosha mikono juu, hata mda wa kuangalia mechi hatuna kabisa,
 
Hapa badala ya kuonyesha mambo ya Yanga wanaonyesha goli alilofungwa jana Simba..nakubaliana na unachokisema.
 
Waiboresha Simba tv ipatikane kwenye visimbuzi vyote ili iwe rahisi kupeleka mambo yao jinsi wanavyopenda, waache kutegemea Azam TV kwa kila kitu the same kwa Yanga, Azam ibaki kuonyesha mechi za ligi kuu
Hizo simba tv, Yanga tv, azam fc tv sio channel za TV bali ni vipindi tuu vya like nusu saa au lisaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…