Tamasha la mwaka huu Mwanza, wananzengo hamjawatendea haki

mayowela

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,753
Jumamosi ya wikii hii nilikuwa Mwanza nikasema ngoja namimi nikahudhulie kwenye tamasha, lakini kwa jinsi nilivoona muitikio ulikuwa mzuri na mapungufu pia yalikuwepo yakutosha, kwa lugha ingine Tamasha linazidi kupoteza mvuto siku hadi siku hii sijui inaletwa na Hari ngumu ya ki uchumi kwa wahudhuriaji au wahudhuriaji kulizoea tamasha.

Kwa mwaka huu hamjawatendea haki wakazi wa Mwanza kwa upande wa burudani, listi ya wasanii iliyotumbuiza asilimia kubwa ilikuwa haikubaliki na wahudhuriaji
mfn: Wakazi kwa baadhi ya wanaomfatilia ni msanii anaefanya vizuri lakini usiku wa jumamosi ilijidhihirisha kuwa wafuasi wake ni wana twitter na sio nzengo wa Mwanza, ilipelekea kurushiwa mawe na makopo ya maji, pia hii nakemea ni kama ushamba kwa wahudhuriaji

Anyway nifupishe, waandaaji wa matamasha Mwanza kaaeni mkijua kwa muda ambao nimeifahamu mwanza kwa juu juu tu Mwanza na Arusha ni Mapacha, listi ya wasanii haikuridhisha fanyieni kazi hilo malalamiko ni mengi tofauti na sifa zinazosikika..

wengi walitarajia angalau Dogo Janja, JayMo, Mr Blue, Maua Sama, Mesen Selektah, Chege, The Mafik, Zaiidi, Young Killer na Navy Kenzo wangekuwepo ila hao wote hawakuwepo, na waliofanya vizuri angalau Weusi na Fid Q, Rostam wajaribu kubadili shoo zao zimezoeleka na wanaonekana wakawaida

Kuna hili lingine nalo sio zuri, enzi zile watangazaji walikuwa wakipanda jukwaani kuhaipu na kutambulisha wasanii lakini mwaka huu imefikia wasanii wanajitambulisha wenyewe jukwaani, yaani ni mtangazaji mmoja tu alihaipu wakati tamasha linaanza anza baada ya hapo mambo yaliyoendelea Mungu ndio ajuae, Sound pia ilikuwa na mwangwi.

Naamini wengine pia humu walihudhuria wanaweza wakashusha walivoviona ili sehemu zingine isitokee
 
Hayo mambo anayaweza ruge!
Nadhani kutetereka kiafya kwake kumefanya waliobaki kushindwa kuandaa kwa ufanisi ule ule!
 
Duuuh wanawapa nafasi upande wa pili ngoja tusikilizie
 
Fiesta yenyewe imejaa wasanii magarasa wa bei cheeeee unategemea nini. Fiesta ya mwaka huu ingeeenda na VYUMA VIMEBANAA maaana ndio uhalisia
 
Fiesta yenyewe imejaa wasanii magarasa wa bei cheeeee unategemea nini. Fiesta ya mwaka huu ingeeenda na VYUMA VIMEBANAA maaana ndio uhalisia
wa bei ghali ni wakina nani?
 
ManDojo, Fid Q, Nandy, Mensen Selekt et all

Wale wa bei cheee ni WCB, KIBA, MAVOKO, V MONEY, JUX, JIDE ET al
WCB wamekwisha acha kuwapandisha kitambo inajulikana wazi hawawezi wapandisha wana mgogoro, Kiba walimpandisha tanga, V money ana ratiba yake tight kama walimpandisha kwenye jiwe la mwezi wasingeshindwa kumpandisha, Jux atapandishwa tu fiesta haijaisha, Jide huyo walishaachana naye kitambo, Mavoko kapandishwa arusha au hata hufuatilii. Mensen selekta wimbo wake wa kinanda ulikuwa hit ndiyo maana wamempandisha, Nandy kwa sasa huwezi taja wasanii wa kike pasipo kumtaja achilia mbali wasanii wa kike huwezi taja wasanii 5 wanaofanya vizuri kwa sasa pasipo kumtaja, Ngosha huyo bwana mpe heshima yake bwana na kila Fiesta lazima apande tu.
 
Zamani kulikuwa na nyumba ndani kulikuwa na mbwa wa kali,alafu nje kuna bonge la bango "HATARI KUNA MBWA WAKALI".Sasa hivi wale mbwa wakali,wengi wao hawapo kwa hiyo sasa hivi limebaki bango "HATARI KUNA MBWA WAKALI" lkn ndani hamna kitu.

Jamaa lazima wajitafakari upya najua ni ngumu kuporomoka kwa siku moja,lkn wakiendelea na hizi sera zao wataliua tamasha lao wenyewe kwa ujinga wao ,kwani wametengezeza matabaka ambayo mwisho wa siku wao ndio wanaumia.Mimi niliambiwa na jamaa yangu dereva wa malori hata tamasha la Moro halikuwa zuri na kwa baadhii ya picha nilizoziona za Mtwara jamaa walichemka,ila sijui hiyo mikoa mingine.

Zamani hits zote za mwaka husika wasanii wana ziperform katika ktk FIESTA ,ila sasa hivi waliodominate game kwa 80% kwa mwaka huu una beef nao matokeo yake tamasha linakuwa bovu na watu wanaingia sababu tu ya mazoea,lkn si kwa ule ubora wake wa kila mwaka.
 
wana beef na WCB tu, nje ya WCB ambaye kadominate ni nani ambaye wna beef naye? Fiesta bado inatamba na ukitafakari kwa undani ni kwamba ile show hawaingizii ela, ela inatoka kwa mdhammini ambaye ni tigo maana unakuta sometimes show kiingilion 7,000 sidhani show hata kama inaingiza watu 20,000 ili wapate 140,000,000. sasa hiyo milion 140,000,000 watoe ela ya kuwalipa wasanii, usafirishaji wa sanii, marathi, kufunga stage, promo na kama unavyojua watangazaji kila mara wanapanda ndege kama wanaenda kariakoo mfano show ya mwanza clouds nzima ilikuwa mwanza na jumapili wote walirudi kwa usafiri wa ndege.
Fiesta bado haijapata mpinzani mpaka sasa ngoja tusubiri wasafi festival tuone. Ila kuandaa show siyo mchezo ukitaka kujua hilo waulize Jux na Vanessa
 
Show kuandaa ni rahisi kama ukipata wadhamini hamna kinachoshindikana . Alafu kaa ukijua ardhi inapata joto pole pole na kupoteza joto lake pole pole, najua ww kwako huoni sign lkn zishaoneka kubali kataa ni swala la muda hata huyo Jux na V money nahisi hawapo vizuri na CMG, najua utasema walikuwa na tour yao lkn ukitazama tour walifanya mikoa minne, lkn sasa hivi kwenye list ya Fiesta hawaonekani, kesho unaweza sikia washatibuana. Unaposema show hawaingizi hela sikuelewi, show ina wadhamini bado Kuna viingilio alafu useme hawapati faida au ww ni auditor, yaani huyo Ruge na Prime times wakubali kufanya tamasha ambalo halina faida, tusidanganyane.
 
CMG bado sana maana ilipokuja EFM ilisemekana itaifunika sasa ni miaka bado iko vile vile trend za kila kitu bado vituo vina copy CMG ukwei ni bado sana kuifunika.
Kuandaa show siyo rahisi, umesema ni rahisi ukiwa na wadhamini ofcourse yes, sasa mpaka uje upate hao wadhamini ndipo shida ilipo maana inabidi uwe na cha ziada cha kuwashawishi mpaka wakupe udhamini.
Jiulize kwanini vituo vingine havifanyi show Tanzania nzima kama Fiesta, Ofcourse siyo Tanzania nzima ila ni show inayofika sehemu kubwa? Au unahisi wengine hawataki? Jibu ni kwamba siyo rahisi na ndiyo maana hata mawingu waliamua kutengeneza kampuni ya Prime Times ndiyo iwe inasimamia show ya fiesta baada ya kugundua ni kitu kinachohitaji kuwa handled vizuri zaidi.
Kuhusu suala la ela huenda hujanielewa rudi usome vizuri nilicho kisema labda utaelewa.
 
Wewe ni G Habash au B Dozen? Mnona unajiweka mstari wa mbele sana kusafisha Miguu ya bata?
 
Naona unayakataa maneno yako,hebu kasome ww ulichokiandika, umesema mwenyewe "jamaa hawaingizi hela" . EFM unawaona wale baada ya mwaka tamasha lao la KOMAA CONCERT, litapata wadhamini na litakuwa kubwa sasa wanatengeneza ile trust, wadhamini waamini na washafanikiwa sasa hivi wa Biko, hatujui mwakani na Majizo huko nyuma pamoja na vigisu alizokuwa akifanyiwa lkn alikuwa anaandaa matamasha (Likizo tyme, matamasha ya kwa fujo Dj's) makubwa, tena kwa ufanisi mkubwa. Baada ya miaka mitatu tutaongea kuhusu Fiesta, Komaa concert na Wasafi, sasa hiyo list ya wasanii wako wakupiga show kwenye kipaimara, unaipeleka ktk tamasha kubwa kama la Fiesta , Fiesta itapotea pole pole na mtapotea tu labda mbadilike. Sasa CMG mpaka wameunda prime Times alafu unasema hawaingizi hela, tusidanganyane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…