Jumamosi ya wikii hii nilikuwa Mwanza nikasema ngoja namimi nikahudhulie kwenye tamasha, lakini kwa jinsi nilivoona muitikio ulikuwa mzuri na mapungufu pia yalikuwepo yakutosha, kwa lugha ingine Tamasha linazidi kupoteza mvuto siku hadi siku hii sijui inaletwa na Hari ngumu ya ki uchumi kwa wahudhuriaji au wahudhuriaji kulizoea tamasha.
Kwa mwaka huu hamjawatendea haki wakazi wa Mwanza kwa upande wa burudani, listi ya wasanii iliyotumbuiza asilimia kubwa ilikuwa haikubaliki na wahudhuriaji
mfn: Wakazi kwa baadhi ya wanaomfatilia ni msanii anaefanya vizuri lakini usiku wa jumamosi ilijidhihirisha kuwa wafuasi wake ni wana twitter na sio nzengo wa Mwanza, ilipelekea kurushiwa mawe na makopo ya maji, pia hii nakemea ni kama ushamba kwa wahudhuriaji
Anyway nifupishe, waandaaji wa matamasha Mwanza kaaeni mkijua kwa muda ambao nimeifahamu mwanza kwa juu juu tu Mwanza na Arusha ni Mapacha, listi ya wasanii haikuridhisha fanyieni kazi hilo malalamiko ni mengi tofauti na sifa zinazosikika..
wengi walitarajia angalau Dogo Janja, JayMo, Mr Blue, Maua Sama, Mesen Selektah, Chege, The Mafik, Zaiidi, Young Killer na Navy Kenzo wangekuwepo ila hao wote hawakuwepo, na waliofanya vizuri angalau Weusi na Fid Q, Rostam wajaribu kubadili shoo zao zimezoeleka na wanaonekana wakawaida
Kuna hili lingine nalo sio zuri, enzi zile watangazaji walikuwa wakipanda jukwaani kuhaipu na kutambulisha wasanii lakini mwaka huu imefikia wasanii wanajitambulisha wenyewe jukwaani, yaani ni mtangazaji mmoja tu alihaipu wakati tamasha linaanza anza baada ya hapo mambo yaliyoendelea Mungu ndio ajuae, Sound pia ilikuwa na mwangwi.
Naamini wengine pia humu walihudhuria wanaweza wakashusha walivoviona ili sehemu zingine isitokee