Wakati nasoma A-Level Tambaza... ilikuwa ni balaha kwa watu kama mimi ambao tulitoka Private School ambako tulizoewa kupikiwa na kuwekewa mezani... hadi namaliza O-Level, sikuwa na sababu ya kwenda tution!
Nafika Tambaza, nakumbuka hadi tunamaliza Form V, tulikuwa na Mwalimu mmoja tu, wa Adv. Mathematics... hatukuwa na Mwalimu wa Physics wala Chemistry... mwaka mzima! Tunaingia Form VI, yule wa Mathematics akahama... tukapata wa Physics ambao alikuw ahodari wa kunong'ona na ubao... miezi kadhaa baadae, tukapata walimu wa field wa Chemistry!! Nakumbuka jinsi ambavyo walichanganyikiwa manake muda miezi ilikuwa imeshakatika lakini hatujasoma chochote... jamaa wakawa wanashindwa hata pa kuanzia!!!! Taabu ilikuwa zaidi kwetu ambao hatukuzoea mambo ya tuition coz' wenzetu kutoka shule kama Azania au Kibasila, walikuwa tayari wameshajipigilia minondo mara baada ya kupiga paper ya form IV.
Pamoja na yote hayo, watu tuliweza kupambana na kufaulu... thanks God, wakati ule hapakuwa na Facebook wala Twitter! Si hivyo tu, wala Ligi Kuu ya UK na Europe hatukuwa nazo! Sehemu pekee ya ku-socialize ni maskani!! Jambo pekee ambalo enzi zile lilikuwa likituweka macho ni mpambano wa Mike Tyson... ambao kwa mwaka mzima, ungekuta ni mpambano mmoja tu!!!!
Hapa nimeuliza kuhusu Mzizima Sec. School... jamaa walikuwa wabaya kufuru lakini na wenyewe siku hizi, balaha tupu!!! Na kule mitaani kwao kulivyojaa tablets, sipati picha!!